Nilikuwa sahihi kwa huyu kocha uchwara Pep Guardiola

Kumbe ni mshabiki wa Arsenal πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ dah nilikua najisumbua bure tu
🀣🀣🀣 ndio na juzi kati tumeshinda makombe ma2 kwa dabali. FA cup na nafasi ya Europa. Na msimu huu tunafanya yetu. Wewe man U msimu umeisha umepata nn. Au hustoria ndio inawabeba
 
...yaani uliposema tu kuwa Guardiola ndiye muasisi wa TikiTaka, tayari nikajua hujui kuwa hujui!
 
Hebu Tuangalie Timu za Italy Alipokuja Conte ilikuwaje kule champions league
2010/11 inter walifika Robo na Ac milan round ya 16
2011/12 Timu 3 za italy Zinafuzu Mtoano na Ac milan wanafika hadi Robo na Kutolewa na Barcelona.

Kafanye Homework yako Vizuri kipindi Conte anaanza kubeba ubingwa 2011 bado Ac Milan na Inter wapo vizuri, ukumbuke Ac milan alikuwa ndio bingwa Mtetezi, kikosi chao kina watu kama Nesta, Ibra, Gatusso, Thiago silva, pato, na mastaa wengine kibao.

Conte kuchukua Epl na Chelsea yenye Eden Hazard..Fabregas and the likes halafu unamtumia Victor Moses kusema kikosi kilikua na average players? Pliiiz! Si ni kikosi hichohicho Mourinho alichukulia ubingwa? Umetudanganya.
Ni Kweli kikosi cha Mou cha ubingwa kilikuwepo kwa Conte ila kuondoa Addition zake kwenye kikosi pia na wewe unaonesha bias zako, hawa Waliongezeka
1. David luiz
2. Marcus Alonso
3. Ngolo kante
4. Victor Moses

Hao ilikuwa piga ua wanaanza na walikuwa na mchango mkubwa tu.


1. Hapo juu sijamtaja kokote Lukaku usinilishe maneno
2. kabla ya kuperform Inter young Amefanya Nini miaka ya Karibuni?

Ndani ya Nusu msimu Chini ya Conte Serie A jamaa amecheza mechi 13 ana Goal 4 na Assist 4, nitajie ni mwaka gani young ana hizi data? Mara ya mwisho young kufunga Goli 4 ama zaidi ni 2011 na mara ya mwisho young kutoa hizo assist ni 2014, tena hizo ni data za msimu mzima. Mchezaji kupata form ya miaka 6 iliopita kwako si jambo zuri?

3. Sanchez naye pia ni hivyo hivyo ameanza Mechi 10 na Assist 8 tayari msimu uliopita. Mara ya mwisho Sanchez kupata Assist zaidi ya 8 ilikuwa ni Msimu wa 2016/17, msimu wa mwisho Arsenal sanchez hakucheza vizuri na hata Man U hakucheza Vizuri, je kocha anaemfanya Mchezaji arudie form ya miaka 3 ama 4 iliopita ni mbaya?


Kwani ukisajili sana Ndio hutumii Average players? Unaweza sajili wachezaji 3 tu na wakawa world class na unaweza sajili wachezaji milioni 1 na wakawa average players.

Ukimtoa Lukaku ambaye amesajiliwa kwa 65m waliobakiwa wote ni bargains za free transfer ama gharama ndogo chini ya $25m.
 
Hujui unachoongea.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Kama unauwezo wa kusema AC Milan ni bingwa mtetezi mwaka 2011...na unawapa robo fainali kama standard yao wakati wakiwa ni mabingwa Mara saba nyuma tu ya Real...halafu unaniambia nikafanye homework?Mimi ni nani wa kubishana na wewe...2011 Milan bingwa mtetezi umeweka na kikosi kweli? like seriously? Mpaka nimekosa nguvu ya kujibu hayo mengine as you totally exposed your self.
 
Tehe tehe heh
 
Hao hapo mabingwa Serie A


2010/11 bingwa ni Ac milan na 2009/10 bingwa ni Inter, kauli yako kwamba walikuwa wamejichokea si sahihi, 2009 mpaka 2011 mara mbili juve ameshika nafasi ya 7, timu inayoshika nafasi ya 7 ndio imejichokea, Na Conte ndio akaitoa Timu nafasi ya 7 na kuwapa ubingwa.

Lete na Wewe ushahidi wako Bingwa wa Serie A 2011 hakuwa Ac Milan.
 
Nilidhani unaongelea UEFA...maana unachanganya mada Mara robo fainali...Mara bingwa mtetezi...be specific unapoongelea UEFA na unapoongelea Ligi...one step at a time.


Point yangu ni kwamba AC Milan kwenye ubora wake..ilitisha mpaka UEFA so ninaposema iliporomoka ninamaanisha hats ulaya iliporomoka pia...Conte hajaishusha Milan kwa kuipandisha Juve series A...Milan imeporomoka hata Ulaya hii siyo siri ndugu...
 
milan 2011 haikuwa mbaya kikosi chenye thiago silva, nesta, gatusso, ibrahimovic, seedorf, pato, el shaarawy, flamini, na wengineo sio kibaya, ibrahimovic alimaliza kama mfungaji bora huo mwaka na Ac milan pia walishika nafasi ya pili nyuma ya juve point 4 utofauti.

milan ilikuja kudrop baadae walipoondoka hao mastaa wao.
 
Kwahiyo management nzima ya Man City pamoja na wamiliki wa Man City ni wapuuzi kwa kuendelea kung'ang'ania kumuongezea mkataba Pep?
Unamaanisha Barcelona na management yao pamoja na zaidi ya nusu ya mashabiki wa Barcelona ambao wanaomba kila kukicha Pep arudi kuifundisha timu yao wote ni wapuuzi!?
Unataka kusema management nzima ya Juventus ni wapuuzi kwa kitendo chao cha kuifukuzia huduma ya Pep Guardiola kila msimu?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hapana kweli!!!
Mimi nadhani wewe ndiye mpuuzi.
 
Mpuuzi ni yule anae amini mawazo ya Wengine kuliko kile anacho kiamini yeye

Hao viongozi wa barca wasinge kua wapuuzi timu yao isingekula 8 na kuparanganyika kama inavyo paranganyika sasa walio kua sio wa puuzi ni Bayern ndio maana aliona chaka sio lake akafunga virago
Juve wanahaha wale hawajui nni wanatka washa ajiri mpaka sari masigara sembuse pep

Alaf kimsingi unaonekana hujaelewa mada soma upya ndio uje kupang'ang'a bila hoja

Si barca wanamtaka kama yeye kocha kweli aende sasa akaijenge iwe tena tishio.
 
Vp Johan Cryff unawezaje kumzungumzia kuhusu TIK TAK?
 
teh teh teh
kuna member ukiweka nao mjadala juu ya hoja fulani kama huna references za kutosha utadhalilika..
ngoja niendelee kumsoma Chief-Mkwawa

Hahaha, jamaa anajua sana kutumia reference, binafsi mtu kama huyo siwekagi league, ila naomba tu anipe ufafanuzi.

Kuna mwamba hapo juu kawekewa majibu naona kahamisha magoli.
 
Hahaha, jamaa anajua sana kutumia reference, binafsi mtu kama huyo siwekagi league, ila naomba tu anipe ufafanuzi.
Kuna mwamba hapo juu kawekewa majibu naona kahamisha magoli.
kuna siku niliingia kwenye 18 zake nikiwa mtupu (thread ya man utd),
teh teh teh nusura anipe kichapo raundi 1.
tokea siku hiyo alinipa funzo kubwa sana
chief mkwawa na malcom lumumba (kataskapos) ni ndugu wawili wasiojuwana
 
kuna siku niliingia kwenye 18 zake nikiwa mtupu (thread ya man utd),
teh teh teh nusura anipe kichapo raundi 1.
tokea siku hiyo alinipa funzo kubwa sana
chief mkwawa na malcom lumumba (kataskapos) ni ndugu wawili wasiojuwana

Mimi namwelewa sana, infact kwenye jukwaa lenu kule ni mtu nikiona ameshusha gazeti nachemsha chai nakaa kabisa ili nisome kwa utulivu.

Maana anaandika kwa kuweka references na haachi kitu.

Kwenye hii post niliuliza top 3 ya makocha nikimlenga aliyeanzisha thread, naona anaruka ruka tu kama mbaazi zilizogoma kuiva, hataki kulijibu hili swali.

Lakini jibu la Chief-Mkwawa ni very comprehensive.

Nilichogundua, mwanzisha thread bwana mwanaspotiapp ni aina ya watu ambao ni conservative, wanaweza kuponda au kuzungumzia negative side ya kitu fulani, ila ukiwaomba wakupe maelezo kwa upande chanya hawawezi. Na always, kuponda ni rahisi kuliko kuelezea positive side.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…