Habari Wakuu,
Kuna jambo nimejifunza kuwa kuna vitu ukivifanya vinaweza kuvunja au kudhoofisha urafiki au mahusiano.
Nina mshikaji wangu mmoja jana tumekutana tukawa tunapiga stori mbili tatu kisha akaniuliza kuhusu maendeleo ya jamaa yetu mmoja wa tangu sekondari, kiukweli ilinipa wakati mgumu kueleza uhusiano wetu kwa sasa maana haupo katika hali nzuri.
Huyu jamaa yangu wa kitambo mwezi wa pili mwaka 2024 alinipigia simu na kuniomba nimsaidie kiasi cha fedha Milioni 1 akidai amepata changamoto kubwa, nilipomuuliza ni changamoto gani hakuwa huru kueleza basi nami nikaona si vyema kumlazimisha ilhali hayupo huru.
Nakumbuka kipindi hicho mwenyewe nilikuwa katika hali mbaya lakini ilinibidi nikope kwa mtu mwingine laki 5 na mimi nikaongezea yangu niliyokuwa nayo laki 5 ikawa Milioni 1 kisha nikamtumia huyo jamaa yangu na alihaidi ndani ya mwezi 1 ambapo ilitakiwa iwe katikati ya mwezi wa 3.
Nilibaki mtupu kiasi cha kumtegemea Bi Mkubwa kunisapoti kufikia mshahara wa mwisho wa mwezi huku nikiamini ndani ya hizo wiki nne jamaa atakuwa amerejesha ile fedha.
Bila kujua mwezi 1 ingezaa miaka 2 sasa nilijikuta nalipa kule nilikokopa ile laki 5, jamaa mwanzoni alikuwa anashika simu anadai bado yuko vibaya imefika hatua nimechoka na nimekata tamaa hata kumtafuta, nimeamua nisijione mjinga bali nimwachie Menyezi Mungu nikiamini yeye aliyeniwezesha basi ataniwezesha tena kupata zaidi ya nilichopoteza katika karakati za kusaidia. Lakini inavunja moyo hata kutoweza kuwasaidia wengine ukidhani ni yaleyale yatatokea tena