Nilimkopesha rafiki yangu Milioni 1 akaahaidi ndani ya Mwezi anarejesha, ila ni miaka 2 sasa

Yani ukimkopesha mtu, ile hela usihesabie kama ni yako hadi utakapo ipata. Kiufupi usiiweke kwenye hesabu zako. Wanadamu ni waajabu sana sana, vinginevyo usikopeshe aiseee. Mimi simkopeshi mtu hela nimelizwa sana.
 
Unaongea nn na unatukana nini Sasa? Nilifikiri uislam hauna fungu la 10 Wala hauna mambo ya sadaka. Sema nyie is either hamna pesa au hamuwajibiki Kutoa sada misikitini ndio mana siku hizi mashehe wenu wameanza kulalamikia waumini wao hawatoi sadaka kama kwa uaminifu kama wagalatia.
 
Sasa hapa bongo watu wa dini gani ndio wenye mpunga zaidi ya waislam?

Hizo simba na yanga ambazo zinawapumbaza akili wafadhili wao wakubwa wote waislam! Matajir bongo asillimia kubwa waislam! Nyie akili hamna,mnaacha kuwapa dhaka masikini mnawapa matapeli wavaa majoho!
 
Unaanzaje kumkopesha mtu kiasi chote hicho cha pesa.

Na zaidi ya yote ukakopa tena ili umkopeshe yeye .

Na zaidi ya yote ukutambua ishara ya red flag ,
Alivyo kuwa hataki kukuambia anataka kukuambia atafanyia nini ili bidi ushtuke.

Wewe ni kondoo uliye kosa ufahamu
Mbwa mwitu wa janja wana kulalua.
 
Hivi kumkopesha mtu hela ni mpaka akwambie anataka kufanyia nini!!! Naona imekaa kimtego hiyo km masimango vile,,

Hata hivyo siungi mkono mambo ya kukopeshana mi mwenyewe nimeshalizwa sana
 
Heri wewe mkuu, mi nilimkopesha ragiki yangu 2million, baada ya muda akaugua sana.
Hatuna hili nablile akafariki.
Nikawa na misiba miwili.
 
Hivi kumkopesha mtu hela ni mpaka akwambie anataka kufanyia nini!!! Naona imekaa kimtego hiyo km masimango vile,,

Hata hivyo siungi mkono mambo ya kukopeshana mi mwenyewe nimeshalizwa sana
Nawewe bado unayo mengi ya kujifunza , pole yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…