Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Habari zenu wana JF,
Nina mahusiano na bidada mdogo tu ambaye anamiliki mgahawa mdogo tu, lakini unamuingizia pesa si chini ya 20K kwa siku, ni mchapakazi kweli kweli na shughuli zote anazifanya mwenyewe kitu kilichonivutia kuwa naye! Mgahawa wake ndo ulikuwa chanzo cha mimi na yeye kufahamiana kwa sababu lunch huwa naifanyia pale!
Tumshukuru mama kwa kuwa mpaka sasa nimekwisha mgegeda mara mbili, siku tatu zilizopita aliniomba nimwazime kitita cha Tsh 90k, lakini siku ya jana nimemkabidhi na kumwambia haitaji kunirudishia, achukue jumla, kanishukuru sana bidada wa watu!
Leo saa sita mchana wakati naenda kupata ugali dagaa nikamkuta yuko anaongea sauti ya chini na miondoko ya mwili na macho na mteja mwenye uchebe na kitambi mbinuko! Nikaamua kuchukua seat pembeni, nikamuita, alipofika nikamwambia anikope ugali dagaa wa 1.5k ili jioni nikiwa natoka kazini nimpitishie pesa yake!
Binti kakataa kata eti nisimuharibie biashara yake! Nimetamani kumdai 90k yangu, sema tu utalbani umeniingia, ingawa nimetoka ndani ya huo mgahawa ndani ya dk 3 tu tokea kuingia, nimejikuta nachekwa na wananchi walio kuwa pale nje huku wakilishambulia chuzi la samaki wa kubanikwa, losti lililotengenezwa na yule bidada!
Hapa nilipo nina hasira! Sijui huyu binti nimfanye nini!