Nilimpiga Mwalimu akahama shule

Duh!,hii adhabu ni kiboko
Nimekumbuka chuo tuliwah kuwa na Rais mvuta bangi,watu wa mlengo huo tuliinjoy maisha sana
 
Jamiiforum
 
T
Tuendelee,mpaka wale wakurupukaji wa kubwabwaja huko mwanzoni wafiche nyuso zao matak o n
 
T

Tuendelee,mpaka wale wakurupukaji wa kubwabwaja huko mwanzoni wafiche nyuso zao matak o n
Inaeeendeleeeea!!!
Kweli club kulifana sana,walijaa wahuni wa kila pembe za arusha,baadhi niliyokuwa nawajua chajop,John mabala,Ebenezer,Ringo akiwa na ndugu yake mojaa,Chingori mshikaji mmoja wa ungalimited aliyekuwa fit sana kwenye kick boxer,watu walimuogopa sana pia alikuwa amefuatana na dada ake ambaye pia alikuwa fit sana kwenye ngumi..na wengine wengi wahuni,vibaka,majambazi..

Tulikunywa pombe club huku tukicheza mziki mpaka mida ya saa 11 jioni club ikafungwa,kimbembe ikawa mda wa kurudi town sasa,maana kuna umbali mpaka ufike kwenye hiace za kwenda Town ni kilomita za kushanta zisizopungua 10.kwa kukadiria..

Tulipokuwa tunatembea kuelekea kupanda gari za Town,John mabala(arusha sec) alikuwa na bifu na ebenezer(arusha sec),toka kitambo walikuwaga marafiki sana,walipozinguana wakatengeneza visasi kwa kila mmoja wao..

Basi tukiwa tunatembea huku tumelewa,tupo wengi barabarani John mabala akamfuata Ebenezer, akamwambia kama vipi leo tumalize ugomvi huku huku,mpaka tujue mbabe nani,aisee huyo John mabalaa alikuwa sio powah jamaa alikuwa fiti sana kwenye mateke,na ukicheki mshikaji wangu ni Ebenezer pia yeye alikuwa fiti sema.sio sana..

Huyo mabalaa akampiga Ebenezer round kick ya shingo,Ebenezer akaweweseka mpaka nilipokuwa nimesimama mimi,nikamzuia kwa mkono,nikamwambia kausha kausha mabalaa,mabalaa akanifuata akaniambia wewe ndo nilikuwa nakutafuta siku zote sasa nimelianzisha ili ujae,umewazingua madogo sana shuleni wakivuta kaya unawang'ang'anya,unajifanya kaka mkuu wa shule leo hii nataka kupigana na wewe,tupiganeeee aliongea kwa nguvu tena kapandisha mzuka..

Ile na tahamaki jamaa karusha right hook,nikakwepa ile nakaa sawa akanipiga wash ya usoni, nikajisemea moyoni leo hii nimekutana na jet Lee.


Kusema la kweli sikujua kama ingetokea ugomvi siku hiyo,kumbe watu walikuwa na bifu nami toka kitambo sana,kitendo cha kuwa kaka mkuu kimenitengenezea bifu kwa watu,sio wavuta bangi tu mpaka wauzaji ambao wanaogopeka mtaani.

John mabalaa akachomoa kisu,ile anataka kunichoma kisu msela angu Ebenezer akanikingia kisu akachomwa cha mbavu,akamchoma tena visu vya paja kama mara tatu,John mabalaa alikimbia baada ya kuona damu inamtoka sana Ebenezer..
Itaendeleeea nikipata mda wa kuandika tena
 
Kuna msela kwao kulikuwaga na pesa sana,nakumbuka tulikuwa tukiwa likizo alikuwa anapenda kwenda arusha,na baadae alianzisha kuandaa matamasha na mziki picnic,tulikuwa tunakutana huko wanafunz wa shule mbalimbali wanafunz walikuwa wanakunywa pombe sana siku hiyo na mziki ulikuwa unapigwa mpaka saa mbili usiku hz mambo zilikuwa zinafanyikaga jumamosi,naona haya mambo aliyatoa huko Arusha.

Ila nasikitika huyo jamaa kwasasa amekuwa teja yaani ukikutana nae hadi huruma kawa chizi nasikia alikuwa akienda Arusha anajihusisha na matumizi ya unga na unga mwingine alikuwa anakuja nao kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…