Nilimruhusu msaidizi auze bidhaa zake ndogo ila zinamlipa kuzidi mshahara wake. Je, nifanye maamuzi gani?

Write your reply...mkuu usisahau biashara ni kipaji lakini pia unaweza kumiliki biaahara lakini usiwe na wateja au kuweza kufanya wateja waje kununua kwako kwani hujawahi kusikia kuna watu ukimwueka akuuzie biashara siku akihama au ukimuondoa basi anahama na wateja wengi au biashara haitokuwa nzuri sana kama kipindi alikuwepo yaani kuna watu wana damu ya biashara,wana kismati. .usikute hata hiyo faida unayopata ni vile tu nyota yake inang'aa kwenye biashara yako ndo hivyo faida nono inaonekana yaani mtu ana upepo wa pesa ambao unakunufaisha na ww pia ,badala umtumie vizuri kutengenesa pesa zaidi eti unataka mfukuze wakati unaweza tajirika kupitia kipawa chake kwa kutembelea upepo wake ni vile tu hujui hao watu ni lulu kiroho na ni vp unufaike nao.! haya mfukuze utapata tabu kuisimamisha tena biashara kama hutopata mtu sahihi anaendana na aina ya biashara yako kwani wengine wanapaswa kuwa wamiliki tu hawatakiwi kuwa waendeshaji au wauzaji wa biashara la sivyo itadoda au kufa kabisa sababu huendani nayo ww au muuzaji uliyemuweka.. hivyo acha kijana afanye kazi ukimtoa utaharibu
 
Hao kuku wanaokuambia roho mbaya ukute hawajawahi hata kufanya biashara...

Ngoja nikuambie, Mimi kitambo nilikua nauza duka la mtu, hivyo hivyo nikaanza kuweka bidhaa zangu kisiri siri(MALENGO), akija mteja nachukua namba, nampigia namuelekeza duka letu jingine(ROHO MBAYA), sehemu niliyokua nauza mimi kodi ilikua chini hivyo Bei ikawa ipo chini pia, ila pale kwa Boss sababu ni potential nikawa napatumia kutangaza biashara yangu ila delivery nyingi zinafanyika kupitia kwangu, (ROHO MBAYA PLUS).
Baada ya hapo mauzo yakawa yapo chini, ila kwa sababu bado ile sehemu naihitaji, lakini pia nisimzunguke 100% mtu alieniamini, bila yeye kujua nikamshauri tuweke mzigo wa jumla, ambao najua mimi sina uwezo nao..
Akazama mfukoni tukashusha Kontena,
BIASHARA IKAPANDA, akanishukuru sana kwa idea ile na Mimi nikapanda,
WIN WIN..

Wewe usihangaike na faida yake, hangaika na mauzo/faida yako, jipe muda, ukigundua inashuka sababu ya biashara yake, Mlipe kwa % au piga chini, ukiona inapanda(ilishuka kwa sababu nyingine) muache, hata akiingiza faida kama yako, kuna watu wana vismati, as long wote mnakula basi sawaaaaa..

Sasa wewe wasikilize hao ngiri eti roho mbaya, kesho ufunge biashara uje hapa wakugeuke...
Yaani nilipe kodi ya 500k, nikulipe 220k, nitoke kwenye faida ya 800k nije 300k, kwa sababu YAKO, nikuache eti kisa na wewe unatafuta? Nani asiyemtafutaji???
Kila mtu ashinde mechi zake.
Balance mambo yako twende sawa.
 
roho mbaya itaondoa baraka zako zote picha imejieleza maamuzi ya hovyo ukichukua kitakupata icho
 

Attachments

  • 1731615794672.jpg
    685.1 KB · Views: 4
Uki

Unapopiga goti kumuomba Mungu usisahau kumuomba moyo wenye huruma na unyenyekevu
 
Hii imekaa poa kabisa jamaa aache kuendekeza tamaa atakuja kujuta mbeleni
 
Kuna wadau wanasema una roho mbaya lakini siyo roho mbaya umakini unahitajika kwenye biashara,ni kosa kuanzisha biashara ndani ya biashara ya mtu mwingine haina uaminifu,fremu unalipa wewe,mshahara na posho unamlipa,ajiongeze na hela za malipo yake mwisho wa siku aache ajira yako afungue biashara zake.

Hiyo kitu ilinifelisha kwenye biashara kuja kugundua ananirudisha nyuma,aliomba aanzishe biashara yake ndani ya kwangu mwisho wa siku anajikopesha bidhaa zangu atumie kuendesha biashara yake humo humo,mwisho wa siku hata katon ya maji ataleta ataacha yako yake itoke kwanza ndo auze yake we unashangaa mbona bidhaa hazitoki kumbe ana zake humo anazitoa kwanza. Nikajiuliza mi nikikaa kwenye biashara siku sina kazi naingiza hela kubwa kuliko siku yeye akiwa mwenyewe.
 
Ilitakiwa amshauri Boss wake aongeze hizo biashara ndogo ndogo Ili mapato ya Boss yaongezeke. Hili nitatizo la wabongo wakipewa ajira wanaangalia namna ya kujinufaisha wao badala yakuongeza mapato katika biashara walizo ajiriwa.
 
Wabongo wengi hatuwezi kuajiriwa Wala kujiajiri. Mtu umepewa nafasi ya ajira, badala utumie nafasi hio kukuza biashara ya boss wako, sisi hutumia nafasi hio kuangalia namna ya kujinufaisha. Ni mpumbavu pekee anaeweza ruhusu kitu hicho. Vinginevyo awe ni mtu tajirii ambae kashajipata, ambae anataka kutoka kwenye uuzaji wa rejareja kwenda jumla.
 
Hii imekaa poa kabisa jamaa aache kuendekeza tamaa atakuja kujuta mbeleni
Hakuna tamaa hapo, yupo sawa nikosa kuanzisha biashara ndani ya biashara ya mtu mwingine. Ilitakiwa aangalie namna yakuongeza faida ya Boss wake, kwa kumshauri waongeze bidhaa hizo ndogo ndogo. Automatically na boss angefikiria kumuongeza bonas au mshahara kwa kuona kijana aliemuweka ni mbunifu. Kwa hali hii wa Tz tutaishia kuwa machinga tu.
 
Tena huyo kukuibia hawezi maana anajipambania mwenyewe pia
Nilitaka nimuambie kitu Kama hili.
Akimwambia asifanye hiyo biashara au akitaka wagawane hiyo faida ya mfanyakazi au achangie gharama za pango au umeme huyo kijana ataanza kumuibia bosi wake au ataacha kazi.
Akina mwingine hawezi kuwa Malini na muaminifu. Atahesabu hasara kila siku.
Tamaa mbaya.
 
Huo mshahara ni mdogo sana.
Mwingine angewza kumuibia bosi au kuacha kazi.
Angalau huyo kaomba hiyo nafasi ili abakie muaminifu kazini.
Hapo inatakiwa asifanye biashara ambayo inafanana bidhaa na mwenye duka.
Ikiwezekana kila anapoleta bidhaa zake mpya amjulishe mmiliki wa duka thamani na idadi yake.
Amuwekee kikomo Cha ceiling ya mtaji au ukubwa wa biashara yake huyo kijana. Ikifikia hapo wajadili partnership au aondoe au akubali iishiie kiwango hicho tu.
Amuwekee malengo ya kufikia biashara ya bosi wake. Mfano atakiwe kubuni bidhaa mpya za kufikia hayo malengo n.k.
 
Mindset za biashara nikua ukisharuhusu hicho kitu, basi kijana ataangalia biashara nyingine ambayo haipo dukani kwa boss wake ataongeza, mwisho wasiku atampoteza huyo kijana.

Kila siku tunasema wahindi wanapiga hatua kwenye biashara lkn hakuna muhindi anaweza kuruhusu uanzishe baishara ndani ya biashara yake. Kijana ilitakiwa aangalie namna yakuongeza faida ya Boss wake tu na boss akiona biashara inakua atamuongeza mshahara tu.

Mimi mahala napofanyakazi kama tukifanikiwa kuingiza faida nzuri kwa boss wetu, pindi unapo renew mkataba boss wetu anatupa bonas kulingana na performance ya mwaka huo. Kwahio Kila mtu hulazimika kufanya kazi Ili impact yake ionekane.

Mfano wakuta walipwa mil 1/2/3/4 kwa mwezi, lkn unapo renew mkataba wapewa bonas ambayo inazid accumulation ya mshahara wako wa mwaka mzima.

Tukubali kupokea mshahara tuliokubaliana, nakukuza biashara za waajiri wetu, na tukitaka kufanya biashara basi tuache kazi, tukaanzishe biashara zetu kuepuka mgongano wa maslah.
 
Mimi nazan
1:- Achangie gharama za uendeshaji wa biashara zako kwa 15_25% (TRA.KODI.UMEME. N.K ) Mshahara wake na posho zake ibakie hvyo hvyo

2. Ukate pato lake faid ya biashara yake kwa 20%

NB:- kama ulikuta biashara imefungwa na hayupo huo.sio.utaratbu ilipaswa akupe taarfa. Ukiona ana focus san na biashara yake m-pge chin ataharbu yako , au umuachishe
 
Mimi mahala napofanyakazi kama tukifanikiwa kuingiza faida nzuri kwa boss wetu, pindi unapo renew mkataba boss wetu anatupa bonas kulingana na performance ya mwaka huo. Kwahio Kila mtu hulazimika kufanya kazi Ili impact yake ionekane.
Watanzania weusi wenzetu wengi wagumu kufanya hiki kitu.
Anaona anakupa pesa yake ya bure wakati anakulipa mshahara. Hawajui motivation muhimu.
 
Mimi nadhani unakosea kwa options zote unazotaka kuchukua, hakuna hata moja imekaa poa.

Let her, wewe muache afanye kwa sababu inapunguza risks za yeye kuiba/kudokoa kwenye bidhaa zako, lakini pia unampa motisha wa kuendelea na kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…