Nilimshirikisha mama yangu mafanikio yangu nikadhani amefurahi, baada ya muda kila nikiwasiliana naye ananiambia isijekuwa naenda kwa waganga

Ningeshangaa sana kama mama na ndg zako wengine wangeshangilia kama mazezeta ili hali zama hizi ndg wanatolewa kafara kama mbuzi
 
Ningeshangaa sana kama mama na ndg zako wengine wangeshangilia kama mazezeta ili hali zama hizi ndg wanatolewa kafara kama mbuzi
Maadamu mimi sio mtoa kafara nabebeshwa mzigo wa punda sina budi kujiondoa kwenye familia ambazo zinalipa wanafamilia wao ubaya
 
Weka mkeka tuone basi mkuu
Ndugu mambo ya hela ni sensitive sana sio ya kuanika hadharani, siwezi kuwavua nguo kampuni yangu pendwa ya betting, hata kama ni kuwatangaza nitatumia namna nyingine lakini sio kuanika hadharani
 
Kaa chini ongea nao waonyeshe mkeka ulioshinda
 
Dah yaani kuweka kascreenshoot tujue kuwa mwenzetu sio mshirikina umeshindwa kabisa unaishia kusema eti siwezi kuianika kampuni yangu pendwa ya kubeti ? Hapana Sina Imani na wewe ,wewe sema tu ukweli mbona sisi wengi tuna Mali za ndagu na hatufichi Kaka ?
 
Asante sana mkuu, imebidi nionane na ile kampuni ya betting tumekaa chini tukaongea sana kwakweli wamesikitika sana wakanambia sina bahati ya mama, nimezaliwa familia mbaya

Nlikua nmeamini story, hadi nlivofika hapa ndio nikagundua.....nahitaji na chapati mbili.
 
Mpaka sasa sjaona mkeka wa muhindi. So kuna mawili

1. Story ni chai
2. Wewe ni mchawi kweli
Ndugu yangu unahangaikaje kuwathibitishia watu mali zako ni kuwaacha watapike wamalize, binadamu hata umfanyie wema kiasi gani bado atakusema
 
Naona hapo ni kuwaambia tu ukweli hela umepata wapi? Umeficha wao watajuaje?

Kwa uzoefu wa wazazi wako na ndugu zako kwa mafanikio ya gafla wamefikiria hivyo, hawakuwaza betting.
 
Shukuru amehisi ni mchawi kuliko angehisi umesaliti kiumeni.

Muhimu: Betting ni kamari kama kamari zingine.
 
Shukuru amehisi ni mchawi kuliko angehisi umesaliti kiumeni.

Muhimu: Betting ni kamari kama kamari zingine.
Alitakiwa atulie nimweleze sio kuanza kunitusi mshirikina wakati hana uhakika, je ningekuwa mwizi nakashaniita mchawi nayo imekaaje, maisha ya bongo fanikiwa ndio utajua
 
Alitakiwa atulie nimweleze sio kuanza kunitusi mshirikina wakati hana uhakika, je ningekuwa mwizi nakashaniita mchawi nayo imekaaje, maisha ya bongo fanikiwa ndio utajua
Kuanza kufikiria kwamba mama yako hapendi ufanikiwe na ni mbaya kwako basi ujue akili yako haina akili.

Kwa umri uliokiwa nao unahisi mama yako atakuwa anaelewa hayo maswala ya betting au unakaza fuvu tu na kujiona tayari umefanikiwa?
 
Amepata wapi nguvu ya kuniita mchawi wakati mimi ananijua tangu ananizaa, vilevile alikuwa ananidharau kipindi sina akaona mm ni mbwa ndio maana hata kufanikiwa kwangu anathubutu kunitusi na kukataa mafanikio yangu kanakwamba mimi ni mbwa nimewezaje
 
Ni mchoyo kupindukia alidhani watamuomba ndio maana anafanya mambo yake kimyakimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…