Nilimshirikisha mama yangu mafanikio yangu nikadhani amefurahi, baada ya muda kila nikiwasiliana naye ananiambia isijekuwa naenda kwa waganga

Ni mchoyo kupindukia alidhani watamuomba ndio maana anafanya mambo yake kimyakimya.
Sio kweli, kufanya kimya kimya ni muhimu mara nyingi, Kwa njaa za bongo wakijua una pesa au unapiga pesa inaweza ikawa ni hatari na unaweza kupoteza Kila kitu, ndugu na marafiki wanajiona Wana hati miliki wakijua una pesa, utaombwa na utaletewa bill za hospitali mpaka binamu wa sita ambaye hujawahi kumsikia
 
Ndugu mambo ya hela ni sensitive sana sio ya kuanika hadharani, siwezi kuwavua nguo kampuni yangu pendwa ya betting, hata kama ni kuwatangaza nitatumia namna nyingine lakini sio kuanika hadharani
Sawa Chief Godlove
 
Yaani maisha haya, mtu kampiga mhindi lakn anapewa pole huku
 
Huyu hawajui wabongo vzr, na aliyekuwa na kibarua chake anaacha hapohapo
 
Kulikuwa na mama wa kichaga mwanae alikuwa ni jambazi....lakini mama alimbariki mwanae kila siku....siku isiyo na jina mwanae akauawa......
 
Ndicho nilichokifanya, nashkuru sikuwahi kuwakaribisha kwangu, sitowahi kamwe kuwakaribisha kwangu nimeshafahamu ubaya wao
 
Screenshot mkeka ulioshinda, umtumie kama evidence
Haitasaidia kama mtu ameshakuwa na inani hizo maana wengine wamekosa timu hizo hizo.
Huyu amweleweshe taratibu aelewe.
 
Haitasaidia kama mtu ameshakuwa na inani hizo maana wengine wamekosa timu hizo hizo.
Huyu amweleweshe taratibu aelewe.
Ndugu yangu watu kama hawa hata uwafanyie nini na kuwaonesha nini bado watakuita mchawi, kamwe sitapoteza muda wangu ni kukaa mbali nao
 
Achana nao. Maana hawakawii kuwaitwa mamwela na kukusakizia wewe ni jambazi.
 
Asante sana mkuu, imebidi nionane na ile kampuni ya betting tumekaa chini tukaongea sana kwakweli wamesikitika sana wakanambia sina bahati ya mama, nimezaliwa familia mbaya
Tema mate chini mjinga wewe!
 
Niliyemweleza ni mama yangu, kwanza kabisa kitendo cha yeye kuthubutu kunipakazia maneno ya laana kama haya tayari nina mama mbaya
Unajiona umemaliza maisha sio? Unamkosoa Mungu na mzazi kwa kupiga mshindo wa betting?

Easy come, easy go...
 
Wako sahihi.

Na ikitokea mtu wa karibu akafariki katika mazingira haya,huchomoki.

Wanajua huna mishe ya kueleweka ni lazima ungewashirikisha na chanzo cha kipato hicho.

Na wao pia wanawaza kukutenga!
 
Waonyeshe malipo ya TRA,(Makato),yaliyo katwa kwenye hiyo betting ili uwe huru
 
Wako sahihi.

Na ikitokea mtu wa karibu akafariki katika mazingira haya,huchomoki.

Wanajua huna mishe ya kueleweka ni lazima ungewashirikisha na chanzo cha kipato hicho.

Na wao pia wanawaza kukutenga!
Nimeshanusa harufu ya ujinga wao wacha nikae mbali maadui za watu ni familia yake alikozaliwa sina muda wa kupoteza
 
Waonyeshe malipo ya TRA,(Makati),yaliyo katwa kwenye hiyo betting ili uwe huru
Issue sio evidence sijashindwa kufanya hivyo natazama jinsi gani familia yangu ina watu wabaya nasubiri watapike na kuhara iwe ndio mwisho wangu kukanyaga kule mana hapo nitakuwa nimesingiziwa nitakuwa sahihi ili dhambi na machozi yangu yawalipe
 
Ndio tena
Mama ndio adui?

Noma sana.

Sema hii chai yako inapanikisha
Ndio tena ni adui mkubwa amethubutuje kuniropokea maneno machafu kiasi hiki alishindwa nini kutulia nikamtafuta na kumwelekeza vizuri
Inaonesha dhahiri alikuwa akinidharau na hakuwai kutaka nifanikiwe ndio maana nilipofanikiwa bado anazidi kunilipa kwa maneno machafu kana kwamba mimi ni takataka ambayo haikustahili kufanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…