Nilimtelekeza mke wangu, nimerudi nimekuta rafiki yangu kamuoa

Kila kitu kinatokea kwa sababu labda kutuandaa kwa level nyingine katika maisha au kutuweka karibu na Mungu Zaidi. Katika matatizo ndo unajua urafiki wa kweli na urafiki wa magumashi, katika biblia ukimtazama Ayubu kwani yeye alikimbiwa na mke. Mimi binafsi uliyoyafanya uliyafanya hakuna sababu ya kuendela kudhani kama ulikosea au hukukosea kwani yameishatokea na maisha hayarudi nyuma. Mimi sijajua umetulia kiasi gani katika maisha hapa namaanisha kujiimalisha kiuchumi. Kwani naona kama utadeal na mambo mengi kwa wakati mmoja kitu ambacho kama hujajiimalisha kiuchumi uchumi unaweza kuteteleka tena. Mimi binafsi sipendagi kudeal na watu sana napenda kuangalia mbele, kama unaweza jenga nyingine achana nao angalia mbele. Samehe yaliyopita kama nyumba utajenga nyingine kudeal na watu wa namna hio naona utapoteza muda mrefu sana, halafu hao watu ni jeuri sana. Cha msingi ukiweza samehe angalia mbele, Mungu atakupa maisha mengine mapya kabisa. Hayo maisha yanakujengea historia ya kusimulia, watu wanaopitia kwenye shida kama hizo wengi wanakuja kufanikiwa sana katika maisha halafu wanakua watu wa kutufundisha wengine. Hivyo usiwe na hofu Mungu wako hajakutupa, ukitaka maisha ya ushuhuda achana nao angalia mbele.

Angalia ayubu mwisho wake mke wake alirudi mwenyewe kwa aibu kubwa, maana ayubu mpya sio ayubu wa kale. Mungu alimuinua mpaka mke wake akasikia kua ayubu mambo yake yamekaa kwenye njia.


 
......that's deep, welldone!

Cc; Dark City, BAK, King'asti, Asprin


Huyu baba hana kosa lolote zaidi ya kushindwa kutumia vizuri wakati alipokuwa na fweza. Na pia ni upuuzi kumwendekeza mtu eti kwa vile no mzuri au unampenda sana.

Kwa sasa aendelee na kesi na hilo kosa la kufoji linaweza kuwakutanisha na Mramba!
 
Kosa ni lako mzee
1. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
2. Hukumsirikisha kabisa katika mkakati wako
3. Hukujali wataishi vipi pamoja na wototo
4. Umemtekeleza kwa miaka mingi bila kujulikana uko wapi/hai
Wakulaumiwa ni wewe na si mwingine na ulichokifanya ni utoto sana
Usimalaumu rafiki yako kwani wewe ukisusa wenzako wala na vilevile amekulelea
Ningekuwa mimi ni wewe ningeachana na habari hiyo na kuanza upya
 
yani mkeo ni booonge la fwala
simlaumu kuolewa tena,hizo genye zake!
ufwala wake ni kunyang'anya watoto nyumba na kumpa basher wake!
mxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxiou!!
 
Mkuu lawama zote kwako ungempeleka hata kwenu tu yule mwanamke kabla hujasepa
 
Mkuu ulikosea kuchagua mke ila dah kupitia mkasa wako nimepata kujifunza wakati wa shida hakuna mtu atakaekupenda wala kukuthamini.
 
Mkuu ulikosea kuchagua mke ila dah kupitia mkasa wako nimepata kujifunza wakati wa shida hakuna mtu atakaekupenda wala kukuthamini.
 
ulikosea kukimbia bilahati au bila kumjulisha mkeo...pia labda hujakosea ila ulikosea kuchagua mke uliangalia uzuri sana bila kujali anapenda mali sana....
 
Jipe moyo, hiyo nyumba ni mali yako. Ila, kisheria mke mke ulimtelekeza maana sheria inasema ni miezi 6 tu. Kama alimpata mme ikiwa ni zaidi ya miezi 6 ukiwa umemuacha basi hakutenda kosa. Shughulika na nyumba ambayo ni mali yako, watoto pia ni mali yako..
 
Jamaa amemsitiri mkeo uliemtelekeza na watoto.

Ulitaka wawe machokoraa?
kwa makabila mengine hao watoto ni wako pia na huyo mke. pigania nyumba ya watoto kama kwenu hakuna kitanda hakizai haramu.
 
Pole sana mkuu, pia Hongera kwa kupambana na maisha, Kuitwa mwnaume si kazi dogo,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…