Nilimwambia mshikaji wangu asitembee na viatu ndani lakini jamaa kasusa na kukasirika

Inaonekana hukutumia lugha ya kirafiki kumuelekeza (ulimfokea). Nadhani hicho ndicho kilicho mkasilisha.
 
Kweli JF imevamiwa
 
Nadhani umelelewa na single mother au 🌈
 
Kuna sehemu nilienda na jamaa akanipe sapoti ya kuingiza mizigo ndani. Sasa kufika ugenini wakafungua mlango wa mbele sebuleni. Ile sebule ni ya kishua balaa chini kuna zuria za manyoya. Nilivua viatu nikajua jamaa naye atavua. Cha kushangaza akazama na raba chafu balaa. Wenyeji walimkata jicho ila hawakusema chochote. Tulipomaliza letu tukiondoka nilimchana mwana kuwa siyo ustarabu, jamaa alinimaindi kuwa pale siyo kwetu wala kwangu ilitakiwa waongee wenyeji. Niliishia kumpotezea na kumuona nyau tu
 
Jau ilo ustarabu muhimu sana acha wenyewe wa seme usivue viatu
 
Ungemuacha tu maana ni mwana halafu muonyeshe kwamba unapenda usafi kwa njia nyepesi isioumiza inatosha, amekuja mle pamoja badala yake ikagonga mwamba itakua imemkata maini sio kususa ila chakula kisingepita na masimango
Sio mgeni akiwa anatoka mizunguki yake ana pitia hapo home ndio anaenda kwake
 
Ulimletea visa tu ili ule peke yako! Ila utoto raha sana.
 
Inawezekana, mambo mengi naona ni kupika pika tu, na si kawaida kwa me.
Hili ni jukwaa huru pia kila mtu anaonyesha ubobezi wake pia kuna ignore fanya ivyo ikiwa haikupendezi
 
Ikiwa una matatizo Kama hayo usiwe unaleta watu kwako kwakuwa Mgeni anayekuja na kuondoka hata akiingia na viatu I don't think Kama Anaweza kukukwaza.
 
Hata mimi sipendi.Ila mgeni akija kuwa mpole msome kwanza alivyo na mazingira ukiweka sheria sana Africa hii utakosana na watu sana iwe ndg au washikaji nk.

Mimi siwezi muambia siku hiyohiyo.
 
Aisee safi sana, napenda mtu mshenzi kama huyo...yaani anakuja kwako kutaka kukutawala kisha unamchamba anasusa na chakula...simuiti namwacha aondoke nile chakula changu kwa raha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…