KERO Nilipata huduma mbaya katika Hospitali ya Mkoa Kigoma (Maweni), wajirekebishe

KERO Nilipata huduma mbaya katika Hospitali ya Mkoa Kigoma (Maweni), wajirekebishe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Kigoma Mjini, napenda kutoa malalamiko yangu kuhusu huduma niliyoipata katika Hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni wakati nilipompeleka mke wangu kujifungua.

Tulipofika hospitalini majira ya saa 3:00 asubuhi, hali ya mke wangu ilikuwa mbaya sana, hakuweza hata kusimama. Nilipowaomba wahudumu msaada, badala ya kumsaidia mara moja waliniambia niende upande wa pili wa geti nikachukue gari la kumbeba, huku nikiwa nimemshikilia mgonjwa katika hali ngumu.
AEkURDwhFUj7-qgV-ca2wUVG4MWzjagF3XFB12K0x3FlvmAwxjzebsovlM5VpdCL4WM0cwdRlFStwsbKp6iG-BxBiFL8dR...jpg

Screenshot 2026-06-02 120423.jpg
Baada ya muda, tulipewa kitanda, lakini madaktari walifika saa 5:00 asubuhi kwa ajili ya uchunguzi na vipimo. Baada ya vipimo, walieleza kuwa mke wangu anahitaji kufanyiwa upasuaji, jambo ambalo nililikubali kwa kuwa tayari alikuwa amewahi kujifungua kwa njia hiyo miaka miwili iliyopita.

Hata hivyo, licha ya hali yake kuwa ya dharura, mke wangu alipelekwa chumba cha upasuaji saa 8:30 mchana, jambo lililonifanya nipate wasiwasi iwapo kulikuwa na ucheleweshaji usio wa lazima. Pia nilipata mashaka kama matumizi ya bima yalichangia huduma kuchelewa.

Cha kusikitisha zaidi, baada ya upasuaji, mke wangu alinieleza kuwa wakati wa operesheni baadhi ya madaktari walikuwa wakizungumza mambo yasiyohusiana na kazi yao, ikiwemo mijadala ya mpira wa miguu (Simba na Yanga), hali ambayo inaweza kuathiri umakini wao wakati wa kutoa huduma muhimu kama hiyo.

Naomba mamlaka husika zilichukulie suala hili kwa uzito unaostahili, zichunguze tukio hili, na kuchukua hatua stahiki ili kuboresha huduma kwa wagonjwa na kuhakikisha usalama wao unapewa kipaumbele.
 
Back
Top Bottom