Nilipata Tsh 2.5m kwenye Betting, mpaka sasa nimebakiwa na Tsh 1.4m

MOSHI UFUNDI

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2022
Posts
526
Reaction score
1,222
Mwezi ulioisha nikiwa nabet na kampuni la 1xbet, nilifanikiwa kukusanya pesa mpaka ikafika 2.5 million. Baada ya mwezi kuisha upepo ukakata mpaka sasa nimeliwa na imebaki 1.4million.

Najuta sana maana mwanzo kabisa niliwaza nikafungue playstation ila nikawa najivuta kutokana na kuwa busy na kikazi changu cha 200k kwa mwezi.

💣USHAURI KWA VIJANA WENZANGU

👉Pesa ya kamari ukiipata ingiza kwenye vitu vinavyoeleweka haraka iwezekanavyo na kamari acha kabisa narudia kwa herufi kubwa ACHA KABISA.
🤎Kubet sio njia sahihi ya kupata maisha ukipata pesa ya kamari kimbia Usigeuke nyuma.
 
Kabetie yote utapata 2.5bil.🤸🤸🤸
 
Nipostie Mikeka Yako,nione ulikuwa unampigaje Mrusi
 
Kamari ni uraibu..
Hiyo pesa hifadhi mbali kabla haijarejea yote huko ulikoipata!
 
Kuacha no kila mtu na upepo wake wenzio twaendesha maisha kwa kazi hiyo hyo
Hapa kwetu familia nzima tunafanya betting. Tukiamka asubuhi baba a nachukua elfu kumi kisha .anatugawia buku jero kila mtu. Halafu tunatengeneza mikeka. Jioni tunaangalia nani kamtaffuna mhindi

Kila siku tunateketeza elfu kumi kwenye betting. Lkn inatulipa, kwa wiki tunaingiza 1M mambo yakiwa mabaya sana, lknyakienda vizuri mpk 10M
 
Mhhhh! Not easy at all
 
pesa ya kamri haifanyiwi biashara, Nunua ps5 na tivii yako inch 32 weka gheto. utanishukuru baadae
 
Umeshtuka kumeshakucha my friend😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…