Nilipofika Wilaya za Kishapu, Maswa, Meatu, Magu, Busega, Bunda, Tarime na Butiama nilishukuru sana kuishi Dar

Nilipofika Wilaya za Kishapu, Maswa, Meatu, Magu, Busega, Bunda, Tarime na Butiama nilishukuru sana kuishi Dar

Hayo maeneo ni vijiji vya ajabu kabisa. Ni aibu kuiita miji. Yaani maisha ni duni na ya kale sana.

Sikuwahi kujua kwamba Tanzania ina maeneo yapo nyuma kiasi hiki katika maendeleo...
Ndio maana wenyeji wa huko wote wamekimbilia Dar wameshaondoka kwao, ndio nyie hamtaki tena kurudi kwenu.

Acheni kurundikana Dar, kila Raia anataka akae Dar aone madaraja.

Rudini kwenu nyie mkapaendeleze, nyumbani ni nyumbani tu hata kama ni porini😝

Mbona wachaga wanawekeza kwao na husikii wakipaponda nyumbani.

Nyie makabila mengine ndio mna matatizo sana yasiyoisha.
 
Kwa mikoa ya Tanzania ni kweli Dar ndio kila kitu husibishe, kwani huoni Ata wabunge wenu mkisha wachagua wanakuja kuishi Dar
Ishi Dar ukiwa na maisha mazuri,sio ugombanie Mwendokasi na Madaladala kila siku,sio uishi Chumba kimoja na majiko na mitungi ya gesi,sio uishi nyumba kwenda kuoga ni kwa foleni,ni kupoteza muda

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Akili za mwandishi hazina ufikiri mzuri, endelea kudhani na kuyaamini mawazo yako kwa 100%.

Unapima maisha ya mtu kupitia barabara kuwa ya lami? Mungu nisamehe badala yake mwandishi.
 
Nilipita Kiangazi Na Kuna Shida Ya Maji Sana
Nilipita Kishapu, Meatu, Maswa, Itilima, Simiyu, Busega, Bunda, Serengeti, Tarime, Rorya, Mara, Nikarudi Mwanza, Ilemela, Misungwi ?Ngudu, Ukerewe
Aiseeh kuna watu mnatembea mimi kuishi kote Kahama ila hayo maeneo siyajui zaidi huwa nanyoosha barabara had Mwanza nageuka tena.
 
Aiseeh kuna watu mnatembea mm kuishi kote Kahama ila hayo maeneo siayajui zaidi huwa nanyoosha barabara had Mwanza nageuka tena
Inategemea na majukumu yako ndugu. Mie nchi hii nimebakisha Mtwara na Mara pekee, ndiko sijagusa ardhi yake. Kwingine nimefika mpaka wilayani na vijijini kabisa
 
Kuishi kwako Dar una Salio shilingi ngapi kwenye Akaunti yako ya Bank au ndio walewale walamba lips kusindikiza wengine?huko unakokukandia ndiko kuna watu darasa la Saba tu au Form Four lakini akikuonyesha balance yake Bank unaweza ukajikojolea,acha ushamba wa kudhani Dar ndio kila kitu

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Ujinga mzigo sana, hapa jamaa hajaongelea kipato cha mtu mmoja mmoja. Ameongelea uhalisia wa maisha ya watanzania.

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Hayo maeneo ni vijiji vya ajabu kabisa. Ni aibu kuiita miji. Yaani maisha ni duni na ya kale sana.

Sikuwahi kujua kwamba Tanzania ina maeneo yapo nyuma kiasi hiki katika maendeleo.

Baadhi ya sehemu unapita vumbi na unakuja kukutana na lami uchwara pale wanapoita katikati ya mji.

Safari ya maendeleo bado ni ndefu sana nchi hii.
Wewe nawe una majungu tu! Tarime ipi hiyo unaisema ina maisha duni? Mbona hata wilaya ya Busega iko barabara kuu ya Mwanza Musoma ambapo pia kuna mji mdogo wa kibiashara unaitwa Lamadi!

Wilaya ambayo ungeongea nami nikakubaliana na wewe ni wilaya ya Kishapu maana ina tatizo la ukame sana! Ila Wilaya ya Bunda hasa pale mjini pako vizuri tu na kuna lami nyingi!

Tatizo la watu wengi wa Dar ni kujiona wako vizuri zaidi ya watu wa mkoani wakati hata Mwanza tu hapo inaweza kuwa na maendeleo makubwa kuzidi baadhi ya maeneo hapo Dar!
 
Back
Top Bottom