Nilipogundua Subaru Forester unatumia Filter 2 nikauza gari kuepuka stress

Nilipogundua Subaru Forester unatumia Filter 2 nikauza gari kuepuka stress

Mkuu acha fix.
S class ya petrol engine 112 au 272 inatumia oil 8L ambazo ni zaidi ya 150,000
Oil filter si chini ya 30,000
Air cleaner ziko pacha beibrahisi sana labda 80,000
Umezungumzia hydraulic hio lita moja ni kuanzia 35,000 na utahitaji lita kama 7 hivi.
Hio service ya 150k unafanya vipi?
Ukimbana sana atakuja kusema ni hela ya garage, kila kitu anakuja nacho ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Ila ukiona service inakushinda basi jua wewe sio mtu wa mipango. Yaani gari private hadi 5000km zinafika haujafanya serving kwa ajili ya service.

Tuseme kila ukifika 100km unaweka 20,000/- pembeni kwa ajili ya service. Hadi zifike hizo 5000km utakuwa ushatenga pesa isiyopungua milioni 1. Sasa unashindwaje kuhudumia hilo gari?.

Kwa njia rahisi kabisa kama gari yako ni ya matumizi binafsi tu fanya uwe unaweka mafuta ya kilomita 100 then kila ukiweka mafuta ya kilomita 100 tenga pembeni hio hela elfu 20 ya service. Hakuna siku utashindwa kufanya service.
 
Mkuu acha fix.
S class ya petrol engine 112 au 272 inatumia oil 8L ambazo ni zaidi ya 150,000
Oil filter si chini ya 30,000
Air cleaner ziko pacha beibrahisi sana labda 80,000
Umezungumzia hydraulic hio lita moja ni kuanzia 35,000 na utahitaji lita kama 7 hivi.
Hio service ya 150k unafanya vipi?
Bado Labour Charges hiyo gari anaitaja kirahisi kama Passo
 
Alie muelewa huyu mtu tafdhali? Subaru forester 2008 inatumia โ€œfilterโ€ 2 ! Kama ana maanisha mjumuiko wa aina tofauti za filter kwenye gari hizo 2 bado ni chache !
Mimi sijamuelewa hadi sasahiv kwamba anatumia filter mbili za aina moja kwa service au mbili za aina tofauti..Ingawa najua kwamba kuna baadhi ya magari yanatumia filter mbili za aina moja kwenye service hasa magari ya Diesel,mfano Truck ya HOWO inatumia Oil filter 2,Diesel filter 1 na Water separator 1 na Engine oil lita 25
 
๐Ÿ˜๐Ÿ˜ huyu sijui kama anauzoefu na magari hata kwa 5%
 
Wenyewe Japan wanatumia bila shida na hakuna malalamiko....shida ni Sisi wenyewe wabongo hakuna service ya uhakika
Kuna jamaa yangu anayo SH5 namba DYY ameshabadilisha engine mara 5 (EJ20) hadi sasa. Mwingine ana SH5 namba EFB pia ameshusha engine ameweka nyingine (FB20). Mie yangu namba EEA lakini imeanza tabia ya kula oil.

Subaru siiamini hata kidogo, bora Crown na-enjoy kiukweli.
 
Ila hizi Forester SH5 zinazingua sana engine. Zina-knock muda wowote.
Wanasema Subaru ni gari sensitive kwa product ya Japan .... yaani ni gari ambayo inahitaji ufuate utaratibu sana kama vile wanavyofanya gari nyingi za ulaya. Ila tatizo linakuja watanzania sisi tunachukulia gari zote za Japan ni kama TOYOTA ambayo imetengenezwa kuhimili mazingira mengi magumu yaani haiko sensitive sana na mabadiliko ya vilainishi/oil au aina flani ya services.

Hivyo ukinunua Subaru aina yoyote kitu kikubwa ni kufuata sana schedules za services pamoja na kutumia vipuli na vilainishi/oil husika ya gari achana na mafundi wa kuungaunga. Hii ilinikuta nilipofanya service ya kwanza jamaa walizingua then niliposoma soma kwenye Website na community za Subaru ndo nikajua wapi nilikosea, japo still kuna vitu bado sijarekebisha ila nimejifunza sanaa.
 
Eti S class unafanya full service kwa 150k, huyu jamaa hajawahi miliki gari yoyote achilia mbali S class

S class lita za oil inakula
Lita 8 mpaka 9 (depending na engine displacement), kiufupi hio 150k haitoshi hata oil peke ake

Hio 150k huwa natumia kwny crown 2009, kwa service ya engine oil, filters, labor charge

Huyo mwingine anasema ametumia magari zaidi ya 3 na service haijawahi kufika 100k, labda kama hizi ndogo ist passo vits etc ambazo oil lita nne mpaka tano
 
Back
Top Bottom