Ugali siyo chakula cha maskini. Ugali ni chakula cha Waafrika wengi. Mimi siwezi kupitisha hata siku mbili bila kula ugali, ingawaje nina uwezo wa kula vyakula vingi vya Kitanzania. Kila watu wana chakula chakula cha asilia, na Waafrika wengi ni ugali unaotokana na nafaka mbalimbali. Mhaya chakula anachokipenda na anakila bila kuchoka ni ndizi laini, Mchagga ndizi mshale, watu wa pwani na Morogoro wanapenda wali na ugali wa Mhogo, zamani watu wa Mara walipenda ugali wa ulezi siku hizi ugali wa Mahindi, Mjaluo humuondoi kwa Ugali wa mtama, kusini mwa Afrika ukianzia Nchumbiji, Malawi, Zambia mpaka Afrika kusini ni ugali. Kwa hiyo kudai chakula cha jadi cha Waafrika wengi ni chakula cha maskini unaqukosea uafrika wako. Mimi hata wakati nilikaa Marekani nilikuwa nakula ugali na bamia au mrenda kuliko chakula kingine chochote.