Ni kweli kabisa!.. Kama hujawahi kutoka nje ya mipaka ya nchi hii huwezi kuona tofauti, huwezi kuona uchafu wala harufu na mazingira machafu. Huwezi kuona harakati za maisha katika miji yetu yenye kelele kama kero. Watu kuitana kwa miruzi kama wachunga ngombe ni jambo la kawaida.... Ukweli unabaki kuwa, sehemu yoyote katika Dunia hii inaweza kupangwa ikawa sehemu bora ya kuishi kama ilivyo Ulaya. Tatizo kubwa ni watu na malezi yao, mitazamo ya kijima, kurithishwa ujinga na ubishi unaoambatana na kiburi cha kuto- kutii sheria hasa kwa watanzania.
Huhitaji kwenda mbali sana kujifunza jinsi wengine wanavyothamini kuishi maisha bora, vuka mpaka ingia Rwanda utashangazwa na jinsi watu walivyojipanga na kufuata sheria katika mazingira yale yale kama ya hapa kwetu. Usafi unazingatiwa kupita maelezo, nyumba zinajengwa kwa viwango na barabara hali kadharika. Watanzania karibu wote ni kina "Hambiliki" tabia zetu ni chafu kuliko uchafu wenyewe na hatuoni taabu kukaa kwenye uchafu. Kukojoa popote na kujikuna panapo ni kawaida kwa kisingizio cha kubanwa.
Ukitengeneza mazingira ya kuvutia kwako, unavutia watu kuja kubarizi na kupiga "Selfie" stori hazikauki hapo. Kila mtu ni mjuzi asiyependa kukosolewa. Ukienda kinyume na utamaduni wa hovyo ambao ndio unaosifika kuwa nyendo za kimjini mjini, basi utaambiwa una roho mbaya kuliko Rucifer, sio mtu wa watu au sio mtanzania!. Nchi hii tulidai uhuru tu wa kujitawala, baada ya kuupata uhuru hatuna mpango na kujenga au kuboresha chochote, hata tukijaribu ni kwa kulipua maana hapa Duniani tunapita tu..... Duu!!.