Niliporudi kutoka Uswisi baada ya kukaa kule wiki mbili niliona Dar ni chafu sana

Niliporudi kutoka Uswisi baada ya kukaa kule wiki mbili niliona Dar ni chafu sana

Anachokifanya Lema ni ulimbukeni wa kuishi nje ya nchi. Anaonekana hakuwahi kuvuka boda kwenda ng'ambo before.

Tangu arudi kutoka Canada anaona Bongo Kama tupo motoni/jehanamu. Kila kitu kwake ni uchafu na umasikini.
Nilidhani na kelele zote, ubunge sijui utajiri jamaa kasafiri kumbe ukimbizi ndio umemfikisha first world.
 
Nilikaa ulaya miaka mingi niliporudi bongo nilipokulia nikajishangaa kupachukia sana, Africa kuna kelele mno, watu kibao Kila kitu kugombania, Kuna uchafu Kila mahali, kuna harufu Kali sio poa, umeme shida, maji shida, usafiri shida, kufuatiliana Kila ulicho nacho lazima wabongo waongee wananiboa kinoma, watu ni wavivu mno, watu hawalipi kodi, viongozi wanatukana raia, misafara kibao tunazuiwa Barabarani, viongozi wanaibia raia , Kuna trafiki wa kuongoza magari na taa zinawaka ushamba mkubwa wananiboa kinoma, wanawake kibao hawajielewi wanaomba omba badala ya kufanya kazi, wake za watu wanadanga, Yani Africa kero tupu!

Hatari afrika ilo la misafara ya viongozi
 
Nilidhani na kelele zote, ubunge sijui utajiri jamaa kasafiri kumbe ukimbizi ndio umemfikisha first world.
Wanaosema watu wa chuga ni washamba Unadhani wanakosea? Hawa Jamaa udhaifu wao umejificha katika tabia zao za ununda na usela sana Ila ni washamba kuliko wanaoitwa washamba wasukuma kina Shimba ya Buyenze .
 
Nilipata safari nikaenda Uswisi kwenye miji ya Zurich na Bern ila niliporudi baada ya wiki mbili niliona Dar ni chafu kupitiliza.

Ilifika mahali nikaanza kumwambia yule dereva teksi aliyenibeba pale JK Nyerere airport kwamba natamani nirudi ulaya maana huku kunatisha.

Baada ya muda nilizoea tena maisha yetu.
Acha tu unaona kama unaingia kijijini, hasa mda wa kutua dar nikama kakitongoji kachafukachafu hivii, nlitamani nipande ndege nirudi nlikotoka
 
Men! Siyo siri Bongo ni kuchafu! Harufu mbaya manoise kibao, majungu na kufuatilia mambo yasiyowahusu.

Men! siku moja nimeenda bush kumuona babu, kukawa namsiba kwa jirani. Tumeenda kwenye msiba tukakuta wanachimba kaburi.
Naona watu wananyang'anyana tools za kuchimbia, nikadhani wamelipwa kuchimba kumbe ni kazi ya kijamii.

Kumbe wameninote, jioni baada ya kuzika nikawekewa kikao kwamba nimedharau wazee sikuchimba kaburi, na hata kuzika maana hata kwenye mazishi bado watu walikuwa wananyang'anyana tools kuzika.

Wakanilipisha gallon 10 za pombe na kilo 10 za sukari, nikaleta gallon 20 za pombe na sukari kilo 20, bado wakawaka tena eti nimewadharau.
Wafala sana.
 
Nilipata safari nikaenda Uswisi kwenye miji ya Zurich na Bern ila niliporudi baada ya wiki mbili niliona Dar ni chafu kupitiliza.

Ilifika mahali nikaanza kumwambia yule dereva teksi aliyenibeba pale JK Nyerere airport kwamba natamani nirudi ulaya maana huku kunatisha.

Baada ya muda nilizoea tena maisha yetu.
Ungesindikiza na kapicha ka zurich na Bern tujionee huko ulaya kulivyo
 
Dar inanuka sana. Unajua mji mkubwa kama huo sehemu kubwa ya watu kutumia mashimo ya maji taka na si kuunga kwenye drainage system lazima unuke sana. Hewa na fukuto kwenye yale mashimo lazima itoke. Sehemu zenye mfumo wa drainage nazo unakuta zinazidiwa. Kila siku raw sewage inafumuka na kutapakaa. Mbeya nayo uswahili unakuta kuna vyoo vile vya kulenga. Mtaa mzima unanuka. Mwanza wale wa milimani ukipita kunanuka kinyesi tupu, watakuwa wanachimba tuvyooo saizi ya goti. Sema Dar imezidi, kama hujatembelea muda mrefu laizma ujihisi kutapikatapika. Na kichefuchefu na kutapika ni mwili unakuwa umesense sumu imeingia mwilini.
 
Nenda Moshi,the city is amazingly clean,sijaweza kufananisha na miji mingine ya Tanzania,nimepita kama mara mbili,Moshi ni pasafi sana pale mjini...
Tatizo moshi wasambaa wanaaribu moshi. Sio wasafi.
 
Ulaya mbona mbali Sana, Ishi Arusha miezi sita halafu nenda Dar, unaona mji mzima una fukuto la uchafu na vumbi.
Hewa ni nzito sana. Asubuhi ya saa 12 ukiwa unaenda posta maeneo ya magomeni, kuelekea jangwani, kwa juu kuna kitu kama moshi mzito unaofanya hewa iwe nzito sana

Sent from my STK-L21 using JamiiForums mobile app
Mji wa viwanda lazima iwe hivyo
 
Back
Top Bottom