Kiukweli Jemedari hapa amepepesa na amemkosea heshima Mayele. Kwa misimu hii miwili Mayele ndiye amekuwa na mwendelezo wa ufungaji magoli katika ligi yetu ya ndani na msimu huu ameongeza kitu kwa kufunga katika mashindano ya Afrika. Kama ambavyo kulikuwa na enzi za Kagere, Okwi, Ambani, Mogela, Mohamed Huseein "Chinga one", na wengineo basi tukubali ukweli tu kuwa hii misimu miwili ilikuwa ni enzi ya Mayele.
Aliye karibu na Jemedari amwambie tu ukweli kuwa chuki kubwa aliyoitengeneza kwa Yanga inamuharibia sasa kiasi hata mambo yaliyo wazi kabisa anajaribu kuyapotosha kiasi anaanza kuonekana sasa kama mwandishi wa hovyo. Kwa kuwa tu ana ugomvi na baadhi ya viongozi wa Yanga basi hata yale mazuri anajaribu kuyapotosha yaonekane mabaya. Kila mtu amemuona Mayele kwa misimu yote miwili na kwenye kombe la shirikisho amefanya vizuri halafu Jemedari anasema eti mshambuliaji wa kawaida.
Kama Jemedari anamuona Mayele ni mshambuliaji wa kawaida atuambie ni mshambuliaji gani hatari kwenye ligi yetu hapa nchini kwa misimu hii miwili baada ya Kagere kumaliza enzi yake. Kwa tuliomwona Jemedari wakati anacheza hakuwa na uwezo hata robo tu ya uwezo wa Mayele alionao. Sasa anapata wapi ujasiri wa kuandika hayo anayoyandika.?
Jemedari apunguze wivu na chuki kazi yake ya uandishi itaenda vizuri tu kama zamani.
Ni mtizamo tu.