Niliposema Mayele ni overrated na ni striker wa kawaida mlidhani natania

Sioni anapokosea,zilikosea ni kanuni hawaja ziweka,mbona msimu uliopita kulikuwa kuna kanuni zinazo ongoza kumpata mfungaji bora,why msimu huu.Mayele Msimu iliopita alikuwa na na goli 16 kwenye ligi.

Ila msimu huu mpaka sasa Mayele anajumla ya goli 32,17 za ligi na 15 za mechi zote alizocheza CAF.

Kukosa magoli ni sehemu ya mchezo wa mpira,ila huwezi kusema mchezaji mwenye magoli 32 ni overated,labda kama mnataka mabishano ya kusogeza mda wa kula dona.

Ila ndio tunarudi palepale kila mtu ana uhuru wa kuongea, ila hata kichaa na mwendawazimu nao ni watu.
 
Watanzania ni wajinga kuanzia kwenye bandari mpaka kwenye soka, kwa io washabiki wa Simba ndo faraja mnayopata sio? Mo atakua anacheka sana, Raha sana kuongoza mijitu isiyojielewa
Lazima achekelee. We umewahi kuona wapi watu wanatapeliwa timu!! Inakubidi uwe mbumbumbu sana ahadi kutapeliwa timu.
 
Misimu miwili Mayele anaisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa NBCPL, kumhukumu mchezaji kuwa overrated or underrated ni mitazamo yenu hasa wale wenye roho mbaya. Kijana amepambana na ameleta mafanikio kwa waajiri wake nanyi pambaneni mlete mafanikio kwa waajiri wenu.
 
Ukitaka kuona tofauti ya magoli 17 ya Mayele, na magoli 17 ya Saidoo, subiria msimu ujao.
Saidoo tunamuacha, Yanga mkitaka mchukueni tena. Tulitaka tu kuwaonyesha ukubwa wa Simba kama chuo cha soka.
 
Msimu ujao wachezaji 3 wa Simba watamzidi magoli Mayele.
 
Saidoo tunamuacha, Yanga mkitaka mchukueni tena. Tulitaka tu kuwaonyesha ukubwa wa Simba kama chuo cha soka.
Kwa kupitia Saidoo, hebu niambie huo ukubwa wa Simba unaupima vipi?

Jibu kwa mantiki, na sio kishabiki.
 
Kwa kupitia Saidoo, hebu niambie huo ukubwa wa Simba unaupima vipi?

Jibu kwa mantiki, na sio kishabiki.

Ameweza kuwa mfungaji bora, na ana nafasi kubwa ya kuwa kiungo bora na mchezaji bora. Haya yote ni mafanikio aliyoyapata mwaka wake wa kwanza tu Simba kwa hiyo Simba ndiyo imempa huo ukubwa kwa sababu amekuwepo katika ligi hii muda wote huo na hajawahi kufikia mafanikio hayo. Ni mtazamo tu.
 
Mchezaji Bora msimu uliopita ni nani? Na ana muda gani kwenye hii ligi yetu?.

Kama Saidoo ana nafasi kubwa ya kuwa mchezaji bora, kwanini ulisema msimu ujao mtamuacha? Hamtaki walio bora?

Performance yake katika msimu wake wa kwanza, imeisaidiaje timu yake ya Simba?
 

Kwani tupo kwenye chumba cha mitihani? Toa hoja yako, punguza maswali bwashee.
 
[emoji23][emoji23]hawezi kujibu haya maswali magumu
 
Hoja inatolewa kwa mtindo upi? Hayo maswali yangu yametokana na ulichoandika huko juu. Naomba majibu

Nijibu maswali yako kwa mtindo gani wa essay au short notes? Na unanipa limit ya maneno au hata nikikupa kurasa kumi fresh tu? Na maswali yako yana maksi ngapi?
 
Nijibu maswali yako kwa mtindo gani wa essay au short notes? Na unanipa limit ya maneno au hata nikikupa kurasa kumi fresh tu? Na maswali yako yana maksi ngapi?
Jibu kwa essay, hakuna limit ya maneno, maksi ni 100.

Haya twende kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…