Mechi zetu NBC L tunashinda kwa michongo; kwa kuwahonga Marefa na wachezaji wa timu pinzani. Hili hapa analisema Kikwete kuwa, tunashinda kwa njia ambazo hazitusaidii kwenye mashindano ambayo hatuna mtu wa kuongea naye.
Tunapohonga timu nyingine ziikamie Simba, tunawanoa Simba zaidi na kujifubaza wenyewe. Tuacheni Utoto. Tuchezeni mpira uwanjani, haya ya kuwatumia marefa na wachezaji wengine kuturahisishia mechi zetu.
Your browser is not able to display this video.
"Mnashinda lakini mnashinda kwa maarifa siyo, hayasaidii kutoa mchango wa ninyi kuendelea. Ndiyo maana mnashinda hapa hapa tu, mkiingia huko mkafika round ya kwanza, ya pili, NJE! Ni kwasababu ushindi wenu hautokani na kuwekeza katika kuuendeleza mchezo.
Mkikutana na watu msiyowajua, hamna wa kuzungumza naye basi, moja kwa moja mnafungwa"
hapo ndo Simba anapotoboaga,Simba akisimama na kauli mbiu yake kwa Mkapa hatoki mtu alafu akishinda au kudroo ugenini mechi moja au mbili tayari anatinga robo.
Kuna wakati tunazodoana mitaani kiwivu na kishabiki lakini kiukweli ukikaa mafichoni kama taifa unaumia moyo.yanga walituliza mpira sana jana ila ndo r.i.p tena.
Ni Sawa na jinsi Simba sc walivyowafunga Orlando Pirates goli 1 hapa nyumbani wakenda kututoa kwa penalty kule kwao. Ile game tungewafunga magoli Hata 2/3 tungeingia nusu fainali ya CAFCC
Ni Sawa na jinsi Simba sc walivyowafunga Orlando Pirates goli 1 hapa nyumbani wakenda kututoa kwa penalty kule kwao. Ile game tungewafunga magoli Hata 2/3 tungeingia nusu fainali ya CAFCC
Ukiangalia Simba alianza taratibu msimu mmoja kabla alitolewa na Shandy raund ya pili kabisa CAFCC,baada ya hapo tukafuzu makundi ila tulipigwa sana 5 zile away baada ya hapo msimu uliofata tuliuwasha sana unaona kuna maendeleo kabisa na ndio maana saiv Simba hashangilii makundi anawaza Robo na Semi..Mashabiki wa Yanga acheni kuipa presha timu yenu mna timu nzuri sana Kinakosekana ni uzoefu tu ..mkitulia mkaiamini mtafika mbali CAFCC punguzeni Expectations Kuwa na timu nzuri haina maana timu yako ni bora ..