Nilisafiri kwa pikipiki Dar mpaka Tabora

Nakumbuka mwaka 2015 Mwezi 9 baada ya kujichanga changa kidogo nikawa nimesave pesa kiasi nikasema hizi hizi Boxer BM 150 wakati huo ndio zimeanza kushika kasi nikaenda niaenda kuinunua pale mitaa ya Tazara...
Boxer za Mo zipo magori Sana mkuu pia Ni comfort kuliko old model..Zimepanda hewani ki design... Moto Ni ule ule.

Mi naishi Mwanza Saut. niliifata Boxer ya Mo 2019 November Kondoa mkoa wa Dodoma Nilijaza full tenk(32,000) Safari nilianza Saa2 asubuh coz nilikuwa nakamilisha baadhi y nyaraka za ununuzi.

Nilipitia njia ya Katesh nikaibukia Singida Mara kadhaa nili loose direction ila kwenye watu hakiaribiki kitu..Nilikula Singida chamchana saa6 maji nikanywa Nzega saa11 jioni..Singida adi Nzega Ni parefu Sana about km200 hv. nikachapa bati adi mida ya saa1 jioni nipo shinyanga..kutoka Shy adi mwanza Ni km160 Safari nikaichukia kuanzia hapo parefu afu Giza Nene baridi Kali licha ya kuvaa makoti yakutosha na helmet. Nilifika mwanza saa 5 usiku..Umbali wa Km 600 about 400 Miles.

Changamoto na angalizo.. Safari za masafa marefu kwa pikipiki hususa Ni nyakati za usiku si nzuri kwasababu Malori mengi ya mizigo yanaanza Safari saa12 jioni hadi 2 usiku Kashi kashi zinakuwa nyingi upepo mkali Madereva wengine Wasengerema Hawapunguzi mwanga wa taa zao full ikitokea hivo Ni mwendo wa kujipigiza kwenye vidimbwi vilivyopo road.

all in all nilii nilienjoy Sana safari boxer is ma best favorite ever seen ingekuwa Mchina walahi nisingefika Ule mtetemo tu njaa Kila dakika na kufeel kauchizi chizi kwa mbaaali coz adi ubongo ungetikisika.

Ila suala la mkao Apo ndo kiuno full kukibinua kitaludi nyuma Mara utapeleka mbele kidogo utakalia tako la kulia Mara kushoto Ni kwasababu ya uchovu..
 
Hahahaha mikao changamoto balaa kwa pikipiki hasa ukiendesha kwa muda mrefu, kingine wewe ulichoka mapema kutokana na muda ulioanza safari. Ila hizi za mo bado sijajaribu kwenda nazo safari ndefu
 
Nina boda boda wangu akishika piki piki anakuuliza unaenda wapi, unamtajia

location,anakwambia bei zipo mbili kuna bei ya 1500 na bei ya 1000 kwa hyo

location uliyomtajia,utamuliza tofauti ni nini? anakujibu tofauti ni mwendo

1000 (express) 1500 (kawaida),jichanganye mwambie twende kwa express

sijawahi mshika kiuno boda boda wa kiume ila hiyo siku nilimshika mwamba kiuno.
 
Four wheels move the body...

Two wheels move the soul... ✌
 
Hongera sana kwa hiyo adventure, but kama uliifosi sana, ingekuwa vyema ungelala shinyanga kesho yake uamshe tena Mwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…