Nilisafiri kwa pikipiki Dar mpaka Tabora

Nilisafiri kwa pikipiki Dar mpaka Tabora

Hizi adventure asikudanganye mtu, ni tamu sana, mi nishasafiri sana na boxer sema sahv chombo yangu naionea huruma mana ina miaka mitano sipendi kuitumia sana labda mpaka ntakaponunua nyingine safari zitaendelea kama kawa.

Kiufupi unaenjoy sana, kikubwa tembea kwa tahadhali na usilazimishe kufika kwa muda unaotaka wewe, ukichoka pumzika kula maisha, ukijisikia freshy unaendlea na safari. Wenzetu wazungu huwa wanatumia pikipiki kubwa ambazo zinahimili safari hata za kuzunguka dunia nzima. Sio siri inapunguza sana stress!
 
Dah hongera mkuu ,hii kitu naiogopea magari makubwa njiani namna yanavyokupita ,unaweza jikuta mtaroni na huwa hawathamini pikipiki ,

Vp hii changamoto ulikabiliana nayo vp ,maana ujanja wangu pikipiki mwisho mjini,
hahahaa!huo upepo wake ni hatari
 
Kila kitu kinawezekena sema sisi watanzania ni woga sana..
Mmi nimesafiri mara nne kwa pikipiki kutoka mbeya -bukoba via tabora na kwakuwa barabara ya sikonge ni mbovu majuzi nmenyookea singida-dom-iringa. chombo kikiwa ni pikipiki ya kichina aina ya SINORAY 150.

Sent using Jamii Forums mobile app
sinoray haitetemeshi mapumbu kweli? usije ukaua uzazi mkuu kwa uroda wa bodaboda.
 
babukijana,
Mkuu kama ulikuwa Mbeya kuna Mzee alikuwa anaitwa fundi Chris maeneo karibu na Meta Secondary. Huyu alikuwa ni fundi mbobezi wa pikipiki na alikuwa anaichezea kadri anavyotaka.

Huyu alikuwa kabobea ufundi wa pikipiki miaka hiyo kuna pikipiki Za kijapani na ulaya. Mpaka yule Mzungu wa Mbalizi Rena akamchukua kufanya nae kazi.

Huyu alinifanya nipende pikipiki ila jamaa yangu Nabiru aliniangusha na Honda XL 125 akanitia woga wa maisha.

Miaka ya 2011/12 nilikuwa gereji ya pikipiki nilipata kuchezea pikipiki ya mchina, hivyo mpaka leo nimeishia kuziendesha na kuijua nje ndani nitasafiri nayo popote mimi nikiwa fundi na dereva.
 
Boxer X150 (Gear 4). Chalinze - Dodoma - Babati - Arusha - Tanga then Chalinze tena.

Tulikuwa Pikipiki 4. Tumetalii kwa siku tano (usiku minne).

Oil badili baada ya KM1000 japo wao wanasema baada ya KM1500.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sinoray haitetemeshi mapumbu kweli? usije ukaua uzazi mkuu kwa uroda wa bodaboda.
Mkuu mitetemo kwenye pikipiki ya mchina ni kawaida, kama una safari ndefu ukifunga vizuri tarpets,siti, chain,bush za mkasi na hub ya nyuma na engine mount mitetemo itakuwa kidogo.

Pikipiki ya mchina watu wanaidharau kwa kejeli, Boxer itafanya vizuri Highway ukienda Rough road mchina hatakuacha vizuri.

Kuna jamaa yangu kila weekend anapiga Tanga kwenda Dar kwa mchina Huoniao kupitia njia ya Pangani ,Saadani mpaka Bagamoyo.
 
Ina mvuto sana mimi nimepata funzo kumbe unaweza safiri na pikipiki safari ndefu.Pili mtoa mada ametuelimisha tahadhari za kuchukua oil ya akiba na chain adjustment.Tatu boxer ni pikipiki ya nguvu sijui SUNLG ingekuwaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sunlg ingefika vizuri kama Hiyo Boxer.
Boxer kapewa sana promo, kwenye hizi za Mo kaongeza gia zimekuwa 5, urembo wa tanki na USB ya kuchajia simu.

Bora Boxer ingebaki kama toleo lile la BMX125/150 watu waliziita mdomo wa mamba, hizi zilikuwa rafiki kwa mazingira ya Barabara zetu za Tanzania.
 
Ndo mana sipendi pikipiki ambazo ziko chini na hazina nguvu ..imagine una yamaha FZ 09 haka ka kitu ni 3cyl kama ka passo😁 nan anakupita hapo bara baran sipendi piki piki ndogo kwa jinsi unakuta imeminywa wee afu haiendi kiasi kwamba bus hizi zina vts lkn huzikimbii wanakupita wanavoweza hilo ndo tatizo lkn ukiwa na kitu cha maana li kisbo likikupita unaliungia nyuma
Hivi madereva wa Kisbo huwa wanatumia kilevi gani?
 
Back
Top Bottom