Naona haya mambo wakati mwingine yana uzuri na ubaya wake, uzuri ni pale ambapo mtu analipwa kile anachostahili kilicho haki yake bila kudhulumiwa.
Lakini ubaya ni pale tunapoona kuna ukwepaji mkubwa wa kodi halali ya serikali, kwasababu tu mtawala aliyepo sasa ni "mama mpole na msikivu".
Bahati mbaya sioni watu wakikemea hili, bado naona wengi wamejibanza kwenye kivuli cha kumsema vibaya marehemu, hawa wanaweza kuwa ndio wakwepaji wa kodi wanaotuzubaisha na hizi nyimbo za ubaya wa marehemu, ili waendelee na michezo yao michafu.
Sasa naona vyema tujitazame kwa makini tusiwe wajinga, tunaoibiwa huku tunashangilia kwa mapambio pamoja na wezi, wapo wanaofaidi isivyo halali kwa sasa, waliowekeza kwenye kutuzubaisha kunsema vibaya marehemu ili wapate mwanya wa kuendelea kufanya mambo yao.