Waungwana kwema ?
Kweli ukiyashangaa ya Musa, usije kusahau kuwa kuna ya Firauni(Farao).
Kuna rafiki yangu alifiwa na ndugu yake wa karibu huko Temeke hospital yapata miaka 2 sasa. Ile namsindikiza mortuary kukamilisha hatua za kukabidhiwa mwili wa marehemu tulishikwa na mshangao jinsi maiti zilivyojaaa siku ile mpaka zingine kuwekwa chini.
Ile siku ndugu yetu mmoja mtumishi wa Temeke hospital anasema ndio siku iliyoongoza kwa vifo vingi kwa kipindi chote cha miaka 4 ya utumishi wake. Hiyo haikuwa takwimu rasmi ila alihisi tu kwa jinsi alivyotazama miili ikielekezwa mortuary.
Sasa cha kushangaza tunamwona mhudumu mmoja wa kiume akivuta jokofu na kutoa embe dodo kubwa bila wasiwasi kutoka kwenye jokofu lenye maiti. Bila wasiwasi alimwambia mwenzake kuwa embe lake limepoa na liko tayari kwa kuliwa.
Jamaa salute kwako, mpaka leo najiuliza hivi yule mtu kweli au zimwi, maana sio kwa ukatili ule.