Hii hubadilikabadilika siyo January tu na wala siyo Tanzania tu ni worldwide, hiyo Venus imeanza kuonekana upande wa Magharibi baada ya jua kuzama tangu mwaka jana 2024 October, na kama ukiwa location nzuri hata Mecury ungeweza kuiona mida hiyohiyo na itafika kipindi sayari hizo mbili zitaonekana upande wa Mashariki alfajiri kabla ya jua kuchomoza, na hata wakati mwingine kutegemeana na hali ya hewa Venus huonekana hata kabla na baada ya jua kuzama au kuchomoza iwapo utafuatilia location yake kwa makini.
Mwezi hauko fixed, unahama kwa speed maalumu, hivyo ukitazama leo hutauona pale kwenye sayari ya Venus
Hizi sayari zinaonekana hata bila binoculars, kwa mfano muda huu toka nje katazame upande wa Mashariki Kaskazini utaiona Jupiter inang'aa sana, kuna majira siku si nyingi zijazo utaweza kuona lineup ya sayari nyingi zaidi ikiwemo Saturn na zile zingine mbili za mwishoni kule japo hizo huonekana kwa shida sana