Nilitaka kupigwa Kalynda ila nikastukia

Nikikumbukaga ya D9 hata uniletee fursa ya online nakuangalia tuu[emoji849][emoji849][emoji849]
 
Wasomi wetu ni wakukariri hawataki kutumia akili kufikiri
 
ingawa stori yako umetunga tu kifupi ni chai,ila watanzania tujifunze
 
Hiki ndio kilinikuta D9 , best wangu alinishinikiza sana, japo nilikuwa najua ni Scam sikuweka mapesa mengi ila nilipigwa.
Walipigwa watu hapa usipime, sirudii tena haya makitu.
 
Mbona unapigwa maeneo mengi hustuki? Kuoigwa kupo tu ila tofauti ni njia
 
Umenikumbusha yaliwah kunikuta kama haya,niliingia chuo ni kawa mtu pekee anaebet,wengi walikuwa hawajaanza kubet,mwanzo nilkuwa nabet kwa siri ila ikatokea dogo mmoja akanisanukia akaomba nimwelekeze na mpaka nikamfungulia na acc basi kadir siku zilivyoenda madogo wengine wakaibuka walijifunza kwa yule niliemfundisha mwanzo,maana baada ya yeye kujua alianza kuyafanya haya mambo ya betting kwa uwazi

Sasa ikawa siku za wkend asubuh tunakaa pamoja watu kama sita hv tunaanza kusuka mikeka,kuna siku dogo mmoja akapiga laki 7 sasa chuo kizima kikajua,na ikaonekana mwalimu wao ni mimi

Lecture mmoja akanifata ili nimtengenezee mikeka mitatu ya maana na akaweka stake kubwa kwenye kila mkeka,aisee kilichotokea nilitamani kukimbia chuo,huyu lecture alikuwaga na hela sana ila akawa hajui afanyie biashara gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…