Nilitapeliwa mpaka nahisi Dar es Salaam kila mtu ni tapeli

Nilitapeliwa mpaka nahisi Dar es Salaam kila mtu ni tapeli

Mimi waliniita lakini Mungu alikuwa upande wangu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… niliwasikiliza halafu nikawaambia sitaki πŸ˜…πŸ˜….

Nimefika pale wakamwita dada mmoja anajifanya alikuwa mwanachuo na sasa anamiliki gari kali baada ya kuuza madawa yao πŸ˜œπŸ˜…πŸ˜….

Nikamchunguza nikaona kama ni kikoti cha mtumba kavaa halafu kimenyooshwa sana πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… sikuishia hapo nikashuka kwenye kiskuna weee cha kuokoteza Mwenge. Nikawaambia asante. Nikaishia 😜
Good observation.
Miaka ile QNET imeingia Tanganyika sikuwa nikifahamu kuwa home town wapo tayari.

Sasa siku moja nikakutana na dada mmoja ni mtumishi wa umma kwenye taasisi ambayo niliwahi kunyia kazi pale. Alivyoniona tu akamuambia boda asimamishe pikipiki ili tuzungumize.

Neno la kwanza aliniambia umekuwa vyema tumeonana maana kuna fursa ni muhimu nami nihusike. Akaniomba tuonane kesho mitaa flani ila niende nikiwa nimevaa kiofisi.

Kesho yake asubuhi akanikumbusha tena.
Muda ulipofika nikaenda,ile nafika maeneo husika nikampigia simu aje anipokee simu haikupokelewa.

Sasa kwa nje kulikuwa na kijana mmoja kavaa kiutanashati,nikaona nimuulize yeye.
Jamaa akanishika mkono akaniambia umefika na huyu dada anakupenda sana kwani vinginevyo asingeli kujulisha.

Basi buana,tukaingia ndani na watu wote waliokuwemo mle ndani wakakusaxnyika pale sebuleni,nikamuona mwenyeji wapi na dada mwingine ambaye pia ni work met wa huyu mwingine.

Basi kila mmoja akanipa taarifa fupi ya mafanikio aliyonayo mara baaada ya kujiunga.
Sasa wakieleza ni kama hawafananiii kabisa.
Mtu anasema amewatoa ndugu zake wanne kazini na kweli maisha yao yamenyoooka lkn mkishikana mikono unagundua kua huyu anapiga kokoto.

Suti zao ni km wanazilazimisha tu.
Nikaelekwa chumba kingine nikapewa seminar na kucholewa hiyo michoro yao ya mafanikio,nikaoneshwa.

Mara baada tu ya kumaliza hiyo seminar tulikusanyika tena sebuleni.
Wakaja wooote waliokuwemo mle ndani nakuanza kutoa shuhuda zingine lkn baada ya utafiti wangu niligundua kuwa ni matapeli.
 
Ujue katika mapambano ya kutafuta maisha hasa kwetu vijana huwa tunajitahidi kupita maeneo mbalimbali kurisk ili mambo yetu yatuendee vema.

Katika harakati zangu za kutafuta maisha nilishawahi pita maeneo tofauti tofauti na kote huko nilipata experience mbalimbali zilizonikomaza kifikra na kiupambanaji

Nakumbuka kuna kipindi ilinibidi niingie makao makuu kupambana ambako nilienda baada ya kusikia serikali imehamia huko hivo niliona kama ni fursa nikazamia huko kujaribu bahati yangu.

Hakika nilionja joto ya jiwe Dodoma ni ya moto kweli kweli ukifanya masikhara unaweza kufa kwa njaa nakumbuka mapambano yangu ya mwanzo nikiwa sina mtaji wowote zaidi ya nauli ya kunifikisha kule ilibidi nijiingize kwenye biashara ya kuuza ukwaju na kwa kipindi kile ilikuwa inalipa kweli kweli japo muziki wake wa kutembea na lile begi kwenye jua kali biashara ile ilinipa weusi wa Iddi amin dada.


Baada ya kuona nimesave kiasi kadhaa kutokana na kuifanya kwa muda mrefu niliweza kuwa na akiba kama ya laki saba hivi kwenye akaunti yangu ya Equity nikajisemea hii pesa nitaifanyia makubwa.

Hapo ndipo watu wa Dar wakashika hatamu, Nakumbuka nilipigiwa simu na rafiki yangu tuliyesoma nae shule ya msingi ambae tulikuwa tunawasiliana na alikuwa anazielewa hustling zangu, Yeye alikuwa akiishi Dar na alikuwa mnadhifu kweli kweli mara moja moja nikiwa na bando basi nilikuwa nikiona akijitupia mtandaoni akiwa kapendezea sana na vazi la suti wakati huo mimi hata kujipost nilikuwa naogopa maana sura yangu na kiboko vilikuwa vyafanana kwa kiasi.

Nakumbuka aliponipigia simu akanambia ananionea sana huruma kwa jinsi navoteseka na mapambano yangu ya ukwaju ili hali kuna fursa ambazo naweza fanikiwa kwa kutumia nguvu kidogo tu.

Akanambia nifunge safari niende dar akanipe fursa ambayo itanisahaulisha mateso yangu yote na kwa kuwa nilikuwa natamani sana kufanikiwa kwa mara ya kwanza nilinyofoa elfu hamsini katika akiba yangu ambayo nilikuwa nimeiweka kwenye kadi yangu ya benki na kuamua kwenda dar es salaam kwa usafiri wa shabiby

Ilikuwa safari yangu ya kwanza kwenda dar hvo muda wote nilikuwa nawasiliana na rafiki yangu mpaka ninafika dar es salaam ambapo nilikuja kupokelewa huku nikishangaa shangaa mabasi ya mwendokasi na mighorofa ambayo niliitazama hadi shingo ikauma.

Nilipofika geto kwa rafiki yangu asee niliona mwenzangu kajipata maana alikuwa na tv kubwa, sound music ya nguvu na vtu vingine kama fridge ndogo na sofa bed kali sana ilikuwa ni master room nikapatiwa maji nioge akaplace order tukaletewa chips kuku na yeye akamimina mvinyo kidogo kutoka jokofuni mwake mimi nikaomba kupatiwa soda ya coca cola!!

Kisha akanambia kesho yake ndio siku atanipeleka kwenye fursa ambayo imembadilisha maisha yake kwani akanambia yeye hata chuo hakumaliza aliiacha na alitumia hela ya ada kujiunga na hiyo fursa ila hajutii kabisa, Hapo alinitia hasira sana nikasema hapa ndio penyewe plus nina akiba ya kama laki sita na hamsini hivi basi hamna ninachohofia utajiri huu hapa.

Kesho yake ilikuwa ni siku ya jumamosi akaniazima shati lake la mikono mirefu na suruali ya mtelezo ili twende kwa hao maboss ambao ndio wenye fursa wenyewe, basi bhana tukaondoka hadi kwenye jengo moja la orofa refu sana nje kulikuwa na magari ya kifahari na ya kuvutia nikajisemea hapa kutoboa lazima

Tukaingia mpaka ndani waliponiona naingia wakaanza kunipigia makofi i hope rafiki yangu aliwaambia atawaletea mgeni kisha wakanambia you are the next millionaire hapo kichwa kilikuwa kikubwa balaa na rafiki yangu akanitambulisha kuwa namleta huyu naye awe miongoni mwa ma millionaire wenzetu.


Basi pale lecture ikaanza ambapo walikuwa wanaelekeza kwa michoro na product zao pia connection walizonazo nchi mbalimbali huku wakifanya zoom meeting na wazungu wa huko singapore na kuelezea manufaa utayopata baada ya connection utayotengeneza wakataja na package zao na faida utayopata kutokana na kifurushi utachokichagua.

Na wakaniuliza nichague package zao wapo walionyoosha mikono kuchagua package hadi za milioni mbili , rafiki yangu akasema atachukua package ya milioni tano nilishtuka sana walipofika kwangu nikaona kuna package ya laki tano nikasema naombeni hii.


Bila kuchelewesha wakaniletea mezani kwangu na kunipa utaratibu wa kuilipia nikatoka nje kulikuwa na atm nikawithdraw nikawapa laki tano rafiki yangu akitabasamu na kunipa mkono kwa maamuzi niliyoyafanya huku akinambia hutojutia.

Nikapokea kale ka mkoba ambako ndani kalikuwa na kahawa na baadhi ya madawa madawa ya asili ambayo walisema nikiyauza tu nitapata faida mara mbili ila connection ya watu nitaowashawishi wajiunge na ile kampuni itanipa hela nyingi sana.


Nikapata moto akilini nikajisemea hapa nikiingia dodoma moja kwa moja ni kwenda udom huko nitawaunganisha wengi sana.

Kesho yake nikaingia dodoma nilivofika gheto ndio kama akili zikanirudia nikaanza kujiuuliza maswali ya msingi kuwa hivi ni rahisi hivo, nikasema ngoja niingie site aseeeee.....ile kazi ngumu kila ninayemshawishi ajiunge ananambia nyie matapeli nikijaribu walau niuze product zao wanasema bei kubwa kichwa kikaanza kuwaka moto.


Nikajikuta vile vikahawa ambavyo walisema hamna hamna unaweza kuuza hadi elfu hamsini navikoroga na kunywa mwenyewe gheto huku nikiwaza sana na kumchukia yule rafiki kuwa kaniuza mwanae

Nilisota na kutembea hadi soli za viatu zikaisha na sikupata mtu nikaamua nirudi kwnye harakati zangu za ice cream na zile kahawa nilikunywa zote na yale madawa nikayauza kwa hasara nikarudisha kama laki na thelathini tu.

Tukio lile limenifanya nihisi dar kila mtu tapeli🎯
Ndefu MNO
 
Tathmini ya haraka isiyo rasmi ya wanaJF

30% wamewahi kutapeliwa
30% ni wasukuma
20% waalimu
10% wanaishi Goba/Mbezi
10% bado naendelea kufuatilia, lakini ni either waArusha au wachagga...hapa sijajua lakini wanaweza kugawana
Mie naona nipo kwenye hiyo asilimia kumi unayofuatilia ..maana sijioni kwenye hizo nyingine
 
Good observation.
Miaka ile QNET imeingia Tanganyika sikuwa nikifahamu kuwa home town wapo tayari.

Sasa siku moja nikakutana na dada mmoja ni mtumishi wa umma kwenye taasisi ambayo niliwahi kunyia kazi pale. Alivyoniona tu akamuambia boda asimamishe pikipiki ili tuzungumize.

Neno la kwanza aliniambia umekuwa vyema tumeonana maana kuna fursa ni muhimu nami nihusike. Akaniomba tuonane kesho mitaa flani ila niende nikiwa nimevaa kiofisi.

Kesho yake asubuhi akanikumbusha tena.
Muda ulipofika nikaenda,ile nafika maeneo husika nikampigia simu aje anipokee simu haikupokelewa.

Sasa kwa nje kulikuwa na kijana mmoja kavaa kiutanashati,nikaona nimuulize yeye.
Jamaa akanishika mkono akaniambia umefika na huyu dada anakupenda sana kwani vinginevyo asingeli kujulisha.

Basi buana,tukaingia ndani na watu wote waliokuwemo mle ndani wakakusaxnyika pale sebuleni,nikamuona mwenyeji wapi na dada mwingine ambaye pia ni work met wa huyu mwingine.

Basi kila mmoja akanipa taarifa fupi ya mafanikio aliyonayo mara baaada ya kujiunga.
Sasa wakieleza ni kama hawafananiii kabisa.
Mtu anasema amewatoa ndugu zake wanne kazini na kweli maisha yao yamenyoooka lkn mkishikana mikono unagundua kua huyu anapiga kokoto.

Suti zao ni km wanazilazimisha tu.
Nikaelekwa chumba kingine nikapewa seminar na kucholewa hiyo michoro yao ya mafanikio,nikaoneshwa.

Mara baada tu ya kumaliza hiyo seminar tulikusanyika tena sebuleni.
Wakaja wooote waliokuwemo mle ndani nakuanza kutoa shuhuda zingine lkn baada ya utafiti wangu niligundua kuwa ni matapeli.
Njaa kali πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Kuna classmate wangu aliingia akaanza na kutamba mwisho wa mwaka ananunua gari, kilichomtokea hasahau maishani mwake.

Kuna wa hawa wanaojiita LBL nae naona kasi yake si nzuri.
Nimejiunga mbona napiga mafekeche ya kutosha, na mamiradi nafungua na kupanua miradi
 
Mkuu, kiukweli sijasoma uzi wako zaidi ya title
Sijui umeandika nini,nimeona tu uzi ni mrefu nitausoma wakati mwingine

Hata hivyo comment yangu haikuwa na lengo la marumbano...wala sijachekeshwa na uzi wako(kama nilivyokwambia nimesoma title tu)
Nachekaje mtu akitapeliwa?
Na wewe pia? Malumbano
 
Watu wa Qnet wanaongea sana.


Hivi ni vipaji ingefaa watumike kwenye siasa.
 
Back
Top Bottom