Jamani hv hawa wanaojiita Global Alliance wanatoa mafunzo ya Afya,uchumi na ujasiriamali nao vip wapo salama? unakuta watoto wanatoka mikoa mbalimbali kuja kupata mafunzo hayo ya kimtandao kiingilia sh35,000 ada 600,000 ukishalipia ada tu unaambiwa wewe ndo msimamizi mkuu kuanzia leo hvo unatakiwa umtafute mwingine, ukimpata akilipia utapata mgao wako hapo..hawajamaa wanakodi sehem ya ukumbi wanageuza ndo chuo unakuta wanafunzi wapo kama wanachuo vile.Mliopata ujuzi wa hv vyuo vya uchochoroni mtujuze kabla wazazi hatujamalima mifugo yetu.