Nilitapeliwa mpaka nahisi Dar es Salaam kila mtu ni tapeli

Good observation.
Miaka ile QNET imeingia Tanganyika sikuwa nikifahamu kuwa home town wapo tayari.

Sasa siku moja nikakutana na dada mmoja ni mtumishi wa umma kwenye taasisi ambayo niliwahi kunyia kazi pale. Alivyoniona tu akamuambia boda asimamishe pikipiki ili tuzungumize.

Neno la kwanza aliniambia umekuwa vyema tumeonana maana kuna fursa ni muhimu nami nihusike. Akaniomba tuonane kesho mitaa flani ila niende nikiwa nimevaa kiofisi.

Kesho yake asubuhi akanikumbusha tena.
Muda ulipofika nikaenda,ile nafika maeneo husika nikampigia simu aje anipokee simu haikupokelewa.

Sasa kwa nje kulikuwa na kijana mmoja kavaa kiutanashati,nikaona nimuulize yeye.
Jamaa akanishika mkono akaniambia umefika na huyu dada anakupenda sana kwani vinginevyo asingeli kujulisha.

Basi buana,tukaingia ndani na watu wote waliokuwemo mle ndani wakakusaxnyika pale sebuleni,nikamuona mwenyeji wapi na dada mwingine ambaye pia ni work met wa huyu mwingine.

Basi kila mmoja akanipa taarifa fupi ya mafanikio aliyonayo mara baaada ya kujiunga.
Sasa wakieleza ni kama hawafananiii kabisa.
Mtu anasema amewatoa ndugu zake wanne kazini na kweli maisha yao yamenyoooka lkn mkishikana mikono unagundua kua huyu anapiga kokoto.

Suti zao ni km wanazilazimisha tu.
Nikaelekwa chumba kingine nikapewa seminar na kucholewa hiyo michoro yao ya mafanikio,nikaoneshwa.

Mara baada tu ya kumaliza hiyo seminar tulikusanyika tena sebuleni.
Wakaja wooote waliokuwemo mle ndani nakuanza kutoa shuhuda zingine lkn baada ya utafiti wangu niligundua kuwa ni matapeli.
 
Ndefu MNO
 
Tathmini ya haraka isiyo rasmi ya wanaJF

30% wamewahi kutapeliwa
30% ni wasukuma
20% waalimu
10% wanaishi Goba/Mbezi
10% bado naendelea kufuatilia, lakini ni either waArusha au wachagga...hapa sijajua lakini wanaweza kugawana
Mie naona nipo kwenye hiyo asilimia kumi unayofuatilia ..maana sijioni kwenye hizo nyingine
 
Njaa kali πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Kuna classmate wangu aliingia akaanza na kutamba mwisho wa mwaka ananunua gari, kilichomtokea hasahau maishani mwake.

Kuna wa hawa wanaojiita LBL nae naona kasi yake si nzuri.
Nimejiunga mbona napiga mafekeche ya kutosha, na mamiradi nafungua na kupanua miradi
 
Na wewe pia? Malumbano
 
Watu wa Qnet wanaongea sana.


Hivi ni vipaji ingefaa watumike kwenye siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…