Ndugu zangu mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35. Niliumizwa sana na mwenzangu baba wa mtoto wangu na nimeachana nae miaka 12 iliyopita.
Mtoto yuko Form One, baba hana hata habari nae, lakini nashukuru mungu nimejitahidi na nitajitahidi apate elimu. Tatizo ni kwamba kila nikiingia kwenye uhusiano mpya nakuwa muoga na sana imefikia hatua sihitaji tena kuwa na mwanaume. Yaani naogopa vitu vilivyonitokea mwanzo na mwisho nahisi sijui kumpenda mtu yaani kuubwaga moyo nakuwa na wasiwasi na kushindwa kujiachia.
Naombeni ushauri nifanyeje ili niwe sawa na wanawake wengine
single mothers wamekua wakisema wamesuswa na walio wazalisha,inaweza ikawa sawa ila chanzo hamki weki wazi.inatokea mwanaume anakuja kumjulia hali mwanae na matumizi ila mama(single mother)ananza drama na kukumbushia ya kale bila kujali haki ya mtoto wake anaeitaji malezi ya pande mbili.
sijamaanisha alieomba ushauri anahusika na baba kumtelekeza mtoto ila namaana muwe pia mnasema unahisi nini itakua sababu ya baba kumtelekeza mwana.
mwanaume aliepitia hali hii anajua nataka kusema nini.
unakuta mwanaume kajiludi kwa mzazi mwenzake walee mtoto ila mwanamke anavo anza drama oooh uliniacha nimesha zoea ntamlea peke angu mwanangu,namaneno mengi ya shombo na kudhalilisha.unakuta mwanamke anamwekea ugumu baba kumsaidia mwana ila kwa watu huyo mama atatangaza ametelekezwa Na analea pekeee....ili iweje?
mwanamke unaumri 35 na umepata mtoto mkubwa yupo sekondari,bado unatafuta mpenzi kweeeli! mbona unamtia aibu mwanao ni aibu kumtambulisha mwanao baba mpya kila mwaka.
kwanini usifanye kazi nikipi ujakifanya adi umothers.
samahani kwanilicho kiandika kinaweza kisieleweke hasa kwa mtu ambae hakuwa kuona lawama za uongo za hawa single mothers
mpaka Leo nimekutana na single mothers wengi kwahiyo na kiamini nacho kiandika .kwangu Mimi kati ya single mothers kumi wanaodai wametelekezwa, mmoja kati yao yeye ndio sababu(hasa single mothers wenye vipato)
kwanini wanafanya ivi?subili yakufike.
#tuwe wakweli tunapo changia hoja kama hizi tuangalie sana katika jamii zetu ukweli upo,tusiwe tunangalia keyboard ilete maneno
mwisho nawaonea huruma sana single mothers waliotelekezwa Mungu awape riziki muwalee watoto.
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]