Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Wahenga walisema tamaa iliua fisi. Nyumba imeenda, pesa imeenda. Sijui niwalaumu Brela, sijui niwalaumu Usalama wa taifa? Sijui nimlaumu yule dada aliyekuja kunishawishi?
Mshana Jr, nitafutie ndumba ya kuwafuta wote waliosababisha niwe zuzumagic, mpenda miujiza, niliyejawa na tamaa ya fedha na utajiri wa ghafla bin vuu.
Kwa kweli nimesoma sana hapa JF, kuwa utajiri ni process, utajiri una principles zake, lakini nadhani nilirogwa sehemu.
Jamani niweke wapi lisura langu hili la kizee lililojaa makunyanzi? Kweli mimi leo ni mtu wa kulala kwenye gari kweli?
Kweli mimi ni mtu wa leo kulala njaa? Nimlilie nani mimi? Ni nani wa kunifariji? Ni nani wa kusimama na mimi kipindi hiki kigumu?
Je, ninene kwa lugha gani muujiza utokee nyumba yangu irudi?
Natamani kuurudisha nyuma muda nikarekebishe pale nilipo kosea.
Dah! Nchi hii Wachina wanashirikiana na Watanzania wenzetu kutuachia majonzi na kilio mioyoni mwetu. Nimlilie nani mimi?
Amesikika akilia mwana JamiiForums mmoja