Niliuza nyumba yangu nikawekeze Kalynda, nikiamini baada ya muda mfupi ningerudi kuinunua tena. Nyumba imeenda, hela imeenda

Kafarijiwe na vibibi viuza gongo aisee!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mshana Jr, nitafutie ndumba ya kuwafuta wote waliosababisha niwe zuzumagic, mpenda miujiza, niliyejawa na tamaa ya fedha na utajiri wa ghafla bin vuu.[emoji23]
Bro tuanue tanga msiba umeshaisha huo
 
Ni wakati sasa wa serikali kuyaondoa mabonanza yote ya mchina yanaharibu jamii sijui mchongo pesa tatu mzuka hayo ndo madhara yake
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mi mwenyewe mke wangu alinambia huo upuuzi wa kujiunga na kunipa maelezo kibao sijui ukiweka pesa hii unapata hii sasa mimi nakuwaga mbishi fulani kwa mambo kama hayo. Nilichomjibu nikamuuliza we umeweka ngapi akanambia kwanza nimewekeza 20 napata faida. Sasa nikamwambia kama umeweka 20 basi komea hapo hapo usije ukaongeza tena hata sent 1 alinisikiliza ama aliongeza kimya kimya atajua mwenyewe. Ila nilichomwambia ni kama vile nilitewa miujiza... Nilimwambia wewe weka pesa yako ila baada ya siku kadhaa atakuja kulia mtu. Siku ya tatu ananiambia mtandao unasumbua ila watarekebisha kesho, nikamjibu tayari dalili za kupigwa zinaanza na kweli hadi leo ananiona mimi mchawi. Maana kuna jirani yetu yeye aliweka laki 4.
 
Kipigo cha mbwa kachoka kinamuhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…