😂😂hakuna taasisi iliyolala, kalynda walikuwa na legal business kwa mjibu wa brela sema walichofanya ni tofauti na kile walichosajilia, mtu anakwenda kufanya investment ya hela kubwa kwa kuambiwa tu bila kujiridhisha kila idara ya uhalali wao
Hata kwenye matangazo yao ukisoma yanatangaza biashara, ni jamaa walikuwa na akili mingi sana, watu wengi walijiunga kwa kupitia marafiki na si matangazo, matangazo yalitumika kama chachu tu ya kukoleza na kujenga uaminifu kwa watapeliwa
Aisee nilidhani ni kitu kidogo kumbe hii dubwasha imetafuna vigogo. unauza nyumba unabaki hola.
Mimi ngoja nibaki mshamba kidogo. Hata siku moja sijawahi kuamini kwamba kuna siku nitapata mafanikio ya pupa. wacha nihangaike na jasho langu maana Mungu alisema mtakula kwa jasho. Sasa watu wanataka kula bila jasho