Nilivyoingiza 17.6M ndani ya mwaka mmoja na nusu, kwa biashara ya Mgahawa kwa mtaji wa kawaida kabisa

Mimi sijawahi kwenda kwa mganga na biashara zinaenda vizuri na kuna wakati nilizidiwa na wateja kwa kuwa walikuwa wengi kama nyuki

Hilo la kutopokea hela keshi au mkononi nitalifuatilia kuona kama lina ukweli.

Ila kuhusu kufanikiwa nilishafanikiwa siku nyingi na sikutumia mganga mpaka leo sina wazo la mganga

Biashara ni matangazo na ubunifu, hayo ya mganga bado sana kwangu

Pia tangu nizaliwe sijawahi kubet au kushiriki mchezo wowote wa bahati nasibu
 
Hongera sana mkuu, but sorry hiyo tiba ya mganga kwa namna yoyote ilihusisha kuwawekea wateja kitu/dawa yoyote kwenye chakula ili wazidi kuongezeka labda? Ama alikutibu vipi?. Unahisi kweli baada ya tiba mganga ndiyo ukaanza kupata pesa zaidi? Siyo kwamba kuna kitu ulijirekebisha ulipokua ukikosea mwanzo mfano, proper records management, both cash in and out? Ili kujua ulikua unaspend zaidi ya kinachoingia au pia uliboresha huduma zaidi ikapelekea wateja kumiminika?🤔

Hongera sana.
 
Wewe utakuwa ni mtu wa dhahabu, raia wamekimbilia NYAMISHEGA. Niliwaza kwenda ila nafsi ikasita baada ya kukuta wengine washawekeza huko.
Na kwenyewe kule mkuu ungeenda ungetengeneza fedha nimetokako karibuni watu wenye migahawa ikifika saa 3 usiku huwezi kupata chakula na Ni mgodi mkubwa Sana !! Watu Ni nyomi utasema lowasaa kaitisha mkutano wa kuomba kura
 
Na kwenyewe kule mkuu ungeenda ungetengeneza fedha nimetokako karibuni watu wenye migahawa ikifika saa 3 usiku huwezi kupata chakula na Ni mgodi mkubwa Sana !! Watu Ni nyomi utasema lowasaa kaitisha mkutano wa kuomba kura
Sehemu kama hizo ukienda vizuri, unatoka na mamilioni, ila kwa mtu ambae hajawahi kuona kundi la watu linavyokuwa kubwa anaweza kudhani ni utani.
 
Mhhh kwani kasema ametoboa kisa mganga nadhani aliamua kujitofutisha na wengine ndo maana alitoboa na sio vinginevo
Natamani nikueleze kwa upana ila sijui niazlnzie wapi, kiufupi pamoja na uzoefu wangu katika biashara, elimu na umakini wangu ilifikia hatua nikataka kukata tamaa.

Kwenye biashara kuna mambo mengi mkuu, hivyo ni vyema kuchagua upande mmoja kati ya mbili kisha ushikamane nao haswa. Muombe Mungu bila unafiki ikiwa mengine huwezi kuliko kuishi bila kujua unasimamia wapi, vinginevyo utakuwa msindikizaji siku zote.
 
Kwakua nilikuwa mgeni kwenye hayo mambo na nilikuwa na uoga, sikutaka dawa zihusike moja kwa moja kwenye chakula bali katika mazingira ya biashara na ndivyo ilivyokuwa.

Mkuu nilikuwa makini sana na hela zangu na namna ambavyo nikiusimamia mgahawa haikuwa rahisi hela kupotea, kwanza nilikuwa nanunua vitu kwa bei ndogo maana usafiri wa kuvifata nje ya mgodi nilikuwa nao, mimi ndo nilikuwa cashier na huduma zangu zilikuwa bora always. Unakuta vyakula vinaisha ila wakati wa kufunga unakosa hata mia, chakula kuisha maana yake biashara ni nzuri sasa inakuwaje hela isionekane, kwamba nilikua najiibia? Na kwanini mwanzoni hela ilionekana??

Baada ya kujiuliza hayo maswali bila majibu na kujaribu kila njia kujiokoa, nikajikuta naegamia huko. MAMBO YALINYOOKA.
 
Baada ya Dutwa nimezunguka migodi mingine midogo midogo. Sasa nimepumzika mambo ya dhahabu kidogo, Ila mwezi wa Saba nazianza Tena. Mkuu lile nyomi na mzunguko wa pesa ilikuwa unazidi baadhi ya Halimashauri hapa Tz.
 
Hilo la kupotea kwa cash nimelisikia kwa wafanyabiashara wengine pia baada ya kuuliza, pengine wapo humu pia labda.

Ni sawa mkuu, mimi nimejaribu kuelezea uzoefu wangu juu ya huo mradi bila kuficha kitu na hakuna sehemu ambayo nimejaribu kushawishi watu kupita njia zangu. Hata mimi sikuwahi kufikiria katika biashara nyingine zote nilizowahi kufanya, pengine labda mazingira ya unapofanya nayo yana athari zake. Huenda Bariadi ikawa ni tofauti na huko uliko.

Mwisho wa siku tunaangalia namna ya kufika point fulani, njia zinaweza kutofautiana.
 
Nilifika Dutwa wakati namba 2 imefoka, nikaondoka siku ile ile kutokana na mazingira mabaya kuliko nimewahi yaona duniani
 
Nilifika Dutwa wakati namba 2 imefoka, nikaondoka siku ile ile kutokana na mazingira mabaya kuliko nimewahi yaona duniani
Kule namba mbili palikuwa pachafu sana, watu wengi walikuwa wanakuja kupata chakula namba 1.
 
Jongo kabisa hili. Eti chuma ulete. Karne hii unadhani watu ni wajinga ili waamini ujinga kama huu!
 
Kweli kabisa nakubaliana na wewe kabisa,kuna mtu aliniambia faida inaanzia kwenye kununua yaani ukifeli hapo ujue hata sokoni kuna asilimia kubwa ya kuchemka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…