Nilivyoingiza 17.6M ndani ya mwaka mmoja na nusu, kwa biashara ya Mgahawa kwa mtaji wa kawaida kabisa

Ni mawazo yako potofu. JF bwana nini unataka kuleta imani potofu za kishikina hapa. Eti chuma ulete! Hili utawadanganya wajinga tu!
Hata hiyo yako inaweza kuwa imani potofu kwa wengine, hatuwezi kulazimishana maswala ya imani na ndiomaana hata mimi sijalazimisha mtu.

Sina muda wa kubishana, nikutakie mchana mwema.
 
I will apply
 
Bora utoto wenye akili kuliko ukubwa wenye kujaa imani potofu. Hivi kweli karne hii unataka tukuamini eti kuna mtu mwenye uwezo wa kuchukuwa fedha za mauzo ya biashara kwa miujiza? Hili nakupia ni wajinga tu watakaoamini.
Kwakua bado unafugwa kwa shemeji yako huwezi kuelewa, wenye akili hawawezi kupinga uwepo wa hilo swala kwenye niashara, ndiomaana nikasisitiza either kumuomba sana Mungu au njia nyingine.

Sasa kwa haya matusi yako sijui ungechagua upande gani, maana kwa Mungu sikuoni.
 
Umeumba picha isiyo kichwani mwako. Mimi biashara nimezifanya sana sana. Ujinga siyo tusi. Ujinga ni hali ya kutojua. Kudhani kuna chumaulete ni ujinga
 
Huwa niko interested na hiyo biashara ya guest house za machimboni ila taarifa za wadau humu huwa hazijitoshelezi.

Tofauti na guest za mijini ni nyumba kujengwa kwa mabati tu au kuna tofauti zingine mf vitanda,mabafu etc.
 
Na mimi nataka nithubutu kwenye ndizi na piga fuso yangu ya ndizi kutoka kiwira mbeya nauza mabibo sokoni naanza na 3M siku moja nitaleta feedback [emoji2187][emoji2187][emoji2187]
 
Kwenye migodi ya huko kahama maeneo ya kakola,Nyamishiga,nyangalata kote nimepita huko watu ni wengi sana na pesa iko njenje ukiuza hata maji,juice,soda tu unapiga pesa sana mzee watu wanapiga hela laana shida ni hiyo tu ni machimbo ya kuhama hama inabidi na wewe nyumban wakusahau
Madem wanauza K hadi buku mbili na maisha yanaenda ila ukimwi nje nje
 
Sure mkuu biashara ni upepo tu.nishawai ingiza per day 400k hadi 200k .ila now unafukuzia elfu 5 kwa siku.we acha tu

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Sure mkuu biashara ni upepo tu.nishawai ingiza per day 400k hadi 200k .ila now unafukuzia elfu 5 kwa siku.we acha tu

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
na ukipata huo upepo hapo hapo unatakiwa usichezee hela fanya ishu ya maana,kama nyumba jenga ,gari nunua maana baada ya upepo kupita kurudi ni ishu hata kisaikolojia unaweza kuharibika utadhani umelogwa
 
na ukipata huo upepo hapo hapo unatakiwa usichezee hela fanya ishu ya maana,kama nyumba jenga ,gari nunua maana baada ya upepo kupita kurudi ni ishu hata kisaikolojia unaweza kuharibika utadhani umelogwa
Ushauri mzuri sana, nimekupenda bure
 
Bora utoto wenye akili kuliko ukubwa wenye kujaa imani potofu. Hivi kweli karne hii unataka tukuamini eti kuna mtu mwenye uwezo wa kuchukuwa fedha za mauzo ya biashara kwa miujiza? Hili nakupia ni wajinga tu watakaoamini.
Nimewahi kuwa na mawazo haya kwamba huenda kuna chuma ulete anaiba pesa zangu. Nikafunga safari mpaka Tanga sehemu fulani vijijini nikaenda kwa mganga aniague kwanini napata hela lakini sina kitu cha maana, mganga aliniambia anayeniloga ni mke wangu na akanipa dawa kadhaa nikifika Dar Es Salaam nifanye hili na lile na hizo dawa. Nikiwa njiani nilitafakari sana na kuona utapeli fulani yule mganga amenifanyia. Alidai nimetupiwa majini na nimefungwa vifungo 7.

Nikiwa bado njiani natoka Tanga narudi Dar Es Salaam nilitafakari sana na kuja kugundua ni mimi mwenyewe ndiyo nilikuwa na matumizi ya hovyo na sikuwa na nidhamu ya pesa. Nikazitupa zile dawa na kubadilika mimi mwenyewe binafsi bila dawa.

Nilifanikiwa hatimaye japo kwa shida lakini Nilifanikiwa bila mganga wala masharti ya mganga.

Siamini bado mambo hayo ya waganga na biashara.
 
Asante Sana bro kwa mrejesho wa experience yako katika maisha na hasa biashara...
Binafsi nimekuwa nikisumbuliwa Sana na mawazo Kama yako na nimekuwa na ndoto za kufanya mgahawa hasa maeneo hayohayo ya migodi maana nimepitapita huko nikaona maisha ya migodini yanavyokutaka kuspend pesa nyingi kwa huduma ya kawaida kabisa Kama chakula, malazi na mavazi. (Kwa wanaopajua katoro nilikuwa Rwamgasa wakati panahila)
Nilivutiwa na maeneo hayo na nikahamasika kuwekeza kwenye mgahawa, gest , bar na duka la bidhaa pia.
Umenifungua macho, umenipa experience ambayo sikuwahi kuipata kwa mtu yoyete na umeyapa uhai mawazo na ndoto zangu na nakuhaidi mwakani mpaka mwezi wa pili ntakuwa napambana huko kwenye hiyo migodi maana nipo kwenye process za kuhamia geita kabisa (kwa sasa nipo kibondo) nitakutafuta kwa maongezi zaidi [emoji39][emoji39][emoji39].
THANKS ALOT JAMAA
 
Ukisoma historia nyingi za self made millionaires utagundua kitu kimoja kwa wote, nacho ni 'ilikuwa kidogo nikate tamaa na kuacha kila kitu'.

Kwahiyo kwenye biashara mafanikio mara nyingi huja unapokaribia kukata tamaa au pale umekata tamaa tayari ndiyo mafanikio yanakuja.

Biashara chache sana unaweza kuanza na kufanikiwa moja kwa moja bila kukata tamaa kwanza.

Kusali kwa Mungu siyo lazima kutwa nzima ushinde kanisani au msikitini masaa 12. Unaweza kusali dakika 15 tu kila baada ya masaa matatu na bado Mungu atakusikia. Amekupa uhai bure atashindwa vipi kukupa hiyo biashara?
 
Anayekubishia ni yule ambae hajafika maeneo ya migodi hiyo lakini kwa aliyewahi kwenda hata kuona kwa macho tu ame experience hayo yote Tena ndani ya muda mfupi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…