Sawa mkuu. Basi ngoja nijitahidi niembe hospitali ya Milembe kule Dodoma.
Usiende mkuu kwani kifo kipo na watu watakufa tu, kuwe na njaa au shibe kufa kupo
Sehemu ninayoishi nimekaa huu mwaka wa 21 bila kuhama na ninajuana na majirani wengine mpaka kwa majina ingawa hatuingiliani
Wengi wetu tumechanja chanjo za mwanzo kabisa na miaka hii tangu tumechanja death rates yetu mitaani nimesikia wazee wanne waliozeeka na chanzo maradhi ya kawaida
Vijana wawili wameuwawa na wenzao jirani pia
Na mwingine alijinyonga kabla ya covid
Ila kuna bibi Kizee mmoja kila wakati ambulance huja kwa sababu ni mgonjwa anahitaji uangalizi wa karibu sana ni mzee sana
Ila hizi takwimu za kusema watu wanakufa kama kuku wenye kideri baada ya chanjo I don't buy it
Doctors ni lazima waandike sababu ya kifo sio kama kwetu mnazika tu Kama kafia home
Nimechanja
Na nina umri zaidi ya 60 na wanangu wana over 30
Last month nilienda kuchanja ya flu
Na miezi minne iliyopita waliomba kinyesi ili waniangalie kama nina Dalili zozote za cancer na majibu yalirudi niko FIT
Nitakufa siku yangu wala haitawahi wala kuchelewa na yeyote anaepinga alete mkataba wa kuishi hapa na mimi niusaini haha
Nina chanjo ya ndui na TB tangu utotoni
Wakitaka kutumaliza wangewauwa wote waliopo hospital maana kuna wengine wana miaka kibao wamelazwa na kuhudumiwa bure vitanda,chakula , dawa na huduma kibao bure ila bado wanapewa na wanakufa kwa siku zao
Serikali inatumia billions of £s kwa kutuhudumia bure sasa mbona hospital bado wamejaa wagonjwa wazee wengine wanaharisha tu miaka kibao wengine cancer na wengine wanawekewa damu kila baada ya siku kadhaa
Najiuliza sana ila kila mtu ana maoni yake
Na mimi nimetoa yangu wala msinishangae