Siasa tu ndugu yangu. Kuna watu wanakomaa na legacy ndio wapanda miiba.
Hawa wanaosita kuchanja tunahitaji kufanya utafiti juu yao ili kufahamu shida yao ni nini, haiwezekani ulaya na marekani wamechanja watu wao kwa zaidi ya 60% wakati sisi hata zile dozi 1.5mil bado hazijapata watu zote kwenye taifa la watu 60 mil. Hii ni kuonyesha kuwa ama
1. elimu yetu haitoshi kwa kiwango kikubwa bado watu ni wajinga hata kama wamesoma, kama shida ni hii mitaala na walimu viangaliwe upya, au
2. Wananchi hawawaamini tena viongozi wao wa serikali kabisa baada ya kuwadanganya wananchi kwa muda mrefu kwa mambo mengi. kama shida ni hii serikali lazima ijitathimini, au
3. Wananchi wengi bado hawafuati hata njia nyingine za kuzuia maradhi kama vile kutoa vyoo, kuchemsha maji ya kunywa, kutumia kondom, kufanya mazoezi, kupanga uzazi, au
4. Elimu ya chanjo hii na ugonjwa huu haijatolewa vya kutosha, au
5. Serikali amekosea sana kuficha ukubwa wa covid kwenye jamii na kuwaruhusu wananchi wawasafirishe na kuwazika hata waliokufa kwa covid kwa njia za kawaida tu, hivyo wananchi wanashindwa kuhusianisha (clue) vifo kwenye familia, ukoo na mitaani na covid 19. Kama shida ni hii serikali imekosea sana kuruhusu maziko ya waliokufa kwa covid kufanyika kwa njia za kawaida.
Hatuoni aibu kukutana na viongozi au kwenda kwenye mataifa ambayo viongozi wao wamewachanja wananchi wao kwa zaidi 60% wakati sisi hata dose 1,500,000 hazijakwisha bado. Viongozi wetu wanashindwa hata kusafisha mitaa ya miji na kuachia machinga wanachafua kila pahala, wanaogopa kuwaondoa sehemu walizovamia.