Nilivyokutana na Mzee Sued Kagasheki katika mazungumzo na Dossa Aziz 1980s

Nilivyokutana na Mzee Sued Kagasheki katika mazungumzo na Dossa Aziz 1980s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NILIVYOKUTANA NA MZEE SUED KAGASHEKI KATIKA MAZUNGUMZO NA DOSSA AZIZ 1980s

Mmoja katika marafiki zangu ameniletea picha kadhaa za wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Kanda ya Ziwa, Bukoba.

Moja ya picha hizi ni picha ya Sued Kagasheki mmoja wa viongozi wa TAA na muasisi wa TANU Kanda ya Ziwa, Bukoba.

Namkumbuka Mzee Sued Kagasheki siku alipokuja Msikiti wa Shadhly hapa Dar es Salaam.

Sikumbuki siku ile kulikuwa na hafla gani lakini ninachokumbuka ni kuwa alipofariki palifanyika kisomo chake pale msikitini na Sheikh Aboud Maalim alimzungumza Mzee Kagasheki baada ya dua.

Sheikh Aboud Maalim akaeleza ile hadhira kuwa Mzee Kagasheki alikuja kusali Msikiti wa Manyema wakati ule unajengwa.

Kwa kuona kuwa pale pana ujenzi Mzee Kagasheki alitoa fedha kumpa Sheikh Aboud zisaidie ujenzi.

Baada ya utangulizi huu nataka nieleze jinsi nilivyokuja kukutana na mzalendo huyu wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes.

Tulikuwa tumekaa barazani kwa Dossa Aziz nyumbani kwake Mlandizi nyakati za asubuhi kama saa nne mimi, Ally Sykes na mama mmoja Mmarekani Mweusi mwandishi wa Washington Post.

Pembeni ya mabaki ya landrover mbele ya nyumba wa Dossa Aziz, Ally Sykes alikuwa ameegesha Mercedes Benz yake rangi ya bluu iliyokoza, yaani ‘’dark blue.’’

Dossa Aziz akanyoosha kidole chake cha shahada akaniambia, "Nimetembea Tanganyika nzima na Nyerere kwenye Land-rover hii."

Miaka mingi sana Ally Sykes na Dossa Aziz walikuwa hawajaonana.

Walikumbatiana kwa mapenzi makubwa mimi nikiwaangalia na kuvuta hisia watu hawa walikuwaje katika ujana wao wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Tofauti baina yao ilikuwa kubwa sana.

Wote walikuwa watoto kutoka familia kubwa mashuhuri na tajiri katika Dar es Salaam ya miaka ile na wote walikuwa wafadhili wakubwa wa TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Dossa alikuwa amepigwa na ufukara.

Hayo hapo chini ndiyo niliyoelezwa na Dossa Aziz siku ile na akanifikisha na kunikutanisha ndani ya mazungumzo na Sued Kagasheki kama alivyokuwa miaka ya 1950:

‘’Mwaka wa 1951 Kenyatta kwa mara nyingine aliitisha mkutano mwingine baina ya KAU na TAA mjini Arusha (mwaka wa 1950 Abdul Sykes alifanya mkutano wa siri na Kenyatta Nairobi).

Katika ujumbe alioutuma kwa TAA, Kenyatta alisisitiza kuwa uongozi wa chama cha TAA uende mkutanoni na silaha.

TAA iliwateua Abdulwahid, Dossa Aziz na Stephen Mhando kuhudhuria mkutano huo.

Abdulwahid alikuwa na bastola aliyopewa wakati wa vita na ofisa mmoja mzungu kama zawadi.

Ilitokea kuwa siku ya kuzaliwa ya Mzungu yule ilikuwa sawa na yake na kwa sababu yule mzungu akampa bastola yake kwa ukumbusho.

Dossa Aziz alikuwa na bunduki iliyokuwa ikipiga risasi tano kwa mfululizo.

Haijulikani kama Mhando alikuwa na silaha.

Wajumbe wa TAA walisafiri kila mtu peke yake kupoteza lengo.

Dossa Aziz alikuwa wa kwanza kuondoka kuelekea Arusha kupitia Dodoma.

Siku zile kulikuwa hakuna barabara ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha.

Wasafiri waliotaka kwenda Arusha ilibidi wasafiri wapitie Dodoma.
Dossa Aziz alifungasha ile bunduki yake ya risasi tano.

Mjini Dodoma, Dossa Aziz alipokelewa na Mwalimu Ali Juma Ponda, katibu wa TAA Central Province.

Baada ya kuelezwa na Dossa kuhusu ule mkutano wa TAA na KAU uliopangwa kufanyika Arusha, Ponda aliwaarifu Dossa Aziz kuwa kulikuwa na mapigano makali kati ya Mau Mau na vikosi vya Waingereza yaliyosababisha viongozi wa KAU kusakwa na kukamatwa.

Ponda alimfahamisha Dossa kuwa ingelikuwa vigumu katika hali kama hiyo kwa Kenyatta na ujumbe wake kuja Arusha.

Dossa Aziz aliamua kuvunja safari ya Arusha na kuelekea Mwanza kwa gari la moshi kukagua matawi ya TAA.

Mwanza, Dossa Aziz alipokewa na Dr Joseph Mutahangarwa, makamu wa rais wa TAA katika kanda ya ziwa.

Dr Mutahangarwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kufuzu udaktari.

Baada ya kuelezwa kuhusu ule mkutano wa Arusha, Dr Mutahangarwa alimwonya Dossa kuhusu hatari ya mwenendo aliokuwa akichukua Abdulwahid kama katibu na kaimu rais wa TAA.

Dr Mutahangarwa alimweleza Dossa hatari ambazo TAA na uongozi wake ungezikabili pindi serikali ikigundua kwamba TAA ilikuwa ikijaribu kuunganisha mapambano ya TAA na yale ya KAU.

Hofu hii aliyoonyesha Dr Mutahangarwa ilikuwa bila wasiwasi wowote hofu ya kweli kabisa kwa sababu KAU ilikuwa inaunga mkono harakati za Mau Mau na Waingereza waliamini kuwa uongozi wa mapambano yale ulikuwa ukitoka KAU na Kenyatta wakiwa na Kaggia walishukiwa kuwa kati ya viongozi hao.

Kutoka Mwanza Dossa alipanda meli hadi Bukoba ambako alipokewa na Chifu Rutinwa pamoja na mwanasiasa mkongwe, Ally Migeyo na Suedi Kagasheki na wanachama wengine wa TAA katika tawi la Bukoba.

Aliporudi Dar es Salaam, Dossa alikamatwa katika stesheni ya gari moshi na kupelekwa Central Police.

Kituo hiki kilikuwa mkabala la lango kuu la steshini ya treni.
Dossa alipelekwa pale na kuhojiwa.

Ofisa wa Polisi Mzungu alitaka kujua kwa nini Dossa alikuwa akisafiri na bunduki.

Baba yake Dossa, Aziz Ally aliingilia kati na Dossa akaachiliwa huru
bila ya kufunguliwa shtaka lolote.

May be an image of 1 person
1630606783420.png
 
..naona hujamuelezea vya kutosha Alhaji Suedi Kagasheki muasisi wa Tanu kanda ya Ziwa.
 
JK,
Hakika hajaelezwa vya kutosha kabisa.

Aliyeniletea picha hiyo ana mswada wa harakati za kupigania uhuru Kanda ya Ziwa.

Huyu ndugu yangu anaweza kutueleza historia ya akina Kagasheki.
Kuna mzee mmoja huko Bukoba anaitwa Mzee King, anayo hazina kubwa ya Historia ya wapigania Uhuru kule BuKoba na West Lake Region kwa ujumla kama ilivyojulikana hapo zamani.
 
Kam
Kama sikosei balozi anaitwa Khamis Sued Kagasheki, labda kama Abdallah ni jina lake lingine.
Khamis ni mjukuu wa Mzee Sued Kagasheki. Khamis Kagasheki na Abdallah Kagasheki ni watu wawili tofauti. Abdallah Kagasheki ndie aliwahi kuwa Balozi. Huyu tunayemuita Balozi Khamis Kagasheki sina hakika kama alipata hadhi ya ubalozi bali alikuwa mkuu ya Idara fulani kule Geneva kwenye Shirika la Kazi Ulimwenguni.
 
Asante sana Mkuu Maalim Mohamed Said, unapotoa hoja kama hizi, "Mwafrika wa Kwanza kufuzu udakitari", you have to qualify this statement, huyo Dr Mutahangarwa ni Muafrika wa kwanza kufuzu udaktari gani, wapi?, labda ni Muafrika wa kwanza Mhaya, kufuzu udakitari, Mtanzania wa kwanza, Muafrika Mashariki wa kwanza, Muafrika wa kwanza bara zima la Afrika?.
  1. Kidunia Daktari wa kwanza mweusi ni Dr. James McCune Smith, MD (April 18, 1813 to November 17, 1865), was America's first African university-trained physician. He graduated from the University of Glasgow in Scotland.1 Apr 2019
Dr. Mutahangarwa mhitimu wa kwanza wa udaktari (medical doctor) Tanganyika. Sina uhakika na Zanzibar.
 
Asante sana Mkuu Maalim Mohamed Said, unapotoa hoja kama hizi, "Mwafrika wa Kwanza kufuzu udakitari", you have to qualify this statement, huyo Dr Mutahangarwa ni Muafrika wa kwanza kufuzu udaktari gani, wapi?, labda ni Muafrika wa kwanza Mhaya, kufuzu udakitari, Mtanzania wa kwanza, Muafrika Mashariki wa kwanza, Muafrika wa kwanza bara zima la Afrika?.
  1. Kidunia Daktari wa kwanza mweusi ni Dr. James McCune Smith, MD (April 18, 1813 to November 17, 1865), was America's first African university-trained physician. He graduated from the University of Glasgow in Scotland.1 Apr 2019
Pascal,
Naandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na nawazungumza madaktari watano katika siasa za TAA.

Hayo uliyosoma nimenyambua kutoka kitabu cha Abdul Sykes.

Nitachekesha ikiwa nitawaeleza wasomaji wangu kuwa hawa madaktari wote wanachama wa TAA ni Watanganyika.

Hapana haja.

Mswada ulisomwa na wahariri wanne watatu Watanzania na wa mwisho Muingereza na hilo "kosa," uliloliona wewe wao wote hawakuliona.

Labda tuchukulie liliwapita.
Ahsante kwa mchango wako.
 
Kam

Khamis ni mjukuu wa Mzee Sued Kagasheki. Khamis Kagasheki na Abdallah Kagasheki ni watu wawili tofauti. Abdallah Kagasheki ndie aliwahi kuwa Balozi. Huyu tunayemuita Balozi Khamis Kagasheki sina hakika kama alipata hadhi ya ubalozi bali alikuwa mkuu ya Idara fulani kule Geneva kwenye Shirika la Kazi Ulimwenguni.
Nlishawai kusikia Sued Kagasheki na baba mdogo wa Balozi Khamis Kagasheki
 
Back
Top Bottom