Mokaze,
SOMA VITABU HIVI UJUE HISTORIA YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA
Hiyo niliyokuwekea ni clip fupi ya mahojiano yangu na Mtangazaji Maureen wa TBC.
Naamini umeshangazwa na mengi uliyoyasikia.
Unajua kwa nini kadi ya TANU No. 3 ni ya Abdul Sykes, No. 2 ni ya Ally Sykes na No. 1 ni ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere?
Unajua Abbas Sykes ndiyo kijana mdogo zaidi kuchukua kadi ya TANU?
Kadi yake No. 7.
Hivi ushajiuliza vipi ndugu watatu wote wawe na kadi za mwanzo za TANU lakini wamefutika katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika?
Unaijua azma ya Hamza Mwapachu (1913 - 1962) katika kuwakusanya vijana wasomi ndani ya TAA baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia?
Unajua sababu ya Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir kuwa mmoja wa wajumbe wa TAA Political Subcommitee mwaka wa 1950?
Unajua Sheikh Hassan bin Ameir ilipokuja kuundwa TANU 1954 alikuwa akiuza kadi za TANU kwenye darsa zake ndani ya misikiti?
Unajua kwa nini Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU alikuwa Sheikh Suleiman Takadir mwaka wa 1954 hadi 1958 alipofukuzwa chama?
Je, unajua historia ya Mzee Iddi Tulio aliyeshika uenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU kuanzia 1958 hadi lilipovunjwa 1963?
Unajua kwa nini hadi leo historia ya TANU bado haifahamiki vyema na kuwa sababu ya kutowaenzi mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika?
Unajua kuwa kuna watu wanaiogopa historia ya kweli ya TANU?
Mokaze,
Usijibu haya maswali.
Silence is golden because it can never be repeated.
Najua unatambua kuwa ninayo majibu yake yote.
Nayajua haya si kwa kusoma vitabu bali nimeishi ndani ya historia hii lau kama nilikuwa na umri mdogo.
Lakini soma vitabu hivi uongeze maarifa yako.
View attachment 1925644
View attachment 1925658
Kulia ni Balozi Abbas Sykes na Mwandishi nyumbani kwake Sea View, 2012.