Aisee wapo sema humu sijui kama wapo, kuna Dada mmoja mchaga jina sitomtaja niliwahi kukutana nae hotelin sehemu moja inaitwa Mambasa njia ya kwenda kisangani ilikua safari yake ya kwanza lakini alibeba pea kibao viatu vya kimasai alikua anafuata dhahabu/ Oro mapori ya kisangani huko nilipotea miaka kama sita sijarudi kule siku moja nafika tena kisangani nikamuuliza dreva mmoja wa classic za Butembo kisangani huyu dreva anaitwa aggrey ni mtu wa songea, akanipa story za Dada yetu kumbe alikomaa akatoboa akawa ameshanunua truck Benzi kama nne hivi anafuata mizigo viwandani kenya kupeleka Congo, huyu sister hua napenda angekuja akasimulia siku moja maana hakua mdangaji alikua jasiri kwa mtoto wa kike hawa wa oya oya asingethubutu kukata mbuga moshi, uganda then congo bila kua na ndugu.