Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Umenikumbusha jinsi wazanzibar walivopiga pesa dubai, ilikua inaenda kununuliwa gari used dubai, mule ndani siti zinatolewa zote kama ni corola inajazwa mzigo unapangwa vizuri laptops, tv flat screen, na makorokoromengine vioo vinapigwa tinted milango inakua locked kabisa, ngoma ikifika bandarini kinacholipiwa ushuru ni ile gari bidhaa nyingine zote zile zinapita free soko la unguja likawa na vitu vya electronic kibao wapemba wakakuza mitaji then wakaona wahamie kariakoo jamaa walipiga bingo enzi zile basi tu,
Dubai UAE pesa still upo ukiwa na mtaji , Connection na uaminifu..
Biashara ya magari used,manunuzi ya scrap cars kukata na kuuza vipuri bado yanalipa bongo /Africa.
Kuna bidhaa nyingi Sana kule Abc ninazo ninasubiri kujilipua tuuuu...
 
Ila wewe umezidi kusafiri au unauza ngada mkuu[emoji850][emoji850]..mara niko india mara abudhabi[emoji1787][emoji1787]! Uje kwangu sasa...nikienda sana naishia sirari .hahha..nipe uzoefu wa Kampala mkuu...nzuri sana kutembea aisee

Chelewa kupata pesa, pata faida kidogo, usijaribu habari za unga au kutapeli, wauza ngada na matapeli mwisho wao hua ni mbaya sana sana,
 
Chelewa kupata pesa, pata faida kidogo, usijaribu habari za unga au kutapeli, wauza ngada na matapeli mwisho wao hua ni mbaya sana sana,
Unga kibongo bongo sio ukiotewa unakula nyundo nyingi,Unga inchi Za ulaya kidogo afadhali.
 
Hapana kabisa hizo...hatari sanA..namfikiriaga shamim nakosa raha

Mwisho wa hao watu hua ni mbaya mno, wakati wabongo wengi wanaanguka kwenye unga ilikua sababu hawana mitaji, ni afadhali ukifika south wewe tafuta apple zipo wapi, komaa hata na mzigo wa kuja kuuza khmamwala zambia unapiga kwa mwezi trip mbili unaju kingine kipi cha kufanya, watu sijui hawaonagi hizo fursa wakati hua zipo nje nje tu
 
Unga kibongo bongo sio ukiotewa unakula nyundo nyingi,Unga inchi Za ulaya kidogo afadhali.

Afadhali ukachukue nguruwe sumbawanga ukawauzie watu wa mbeya wala viti moto kuliko hayo madude, mwisho wake hua ni mbaya sana, utatamba kwa muda tu wana kibao wanatumikia vifungo nchi mbali mbali na zaidi utaanza kua muuzaji, baadae unaanza kutumia unaishia kau teja au jela kabisa
 
Tupate wadhamini kidogo ....

Ama stori/hustle za jamaa angu mnaija Dubai ,day one anaingia,ubaguzi wa Philippines ,Polisi wa Dubai,maisha ya Sharjah na fujairah, kuwekwa kizuizini Qatar airport jijini doha...kupata pesa kuanza biashara ya kuuza spare parts used from Dubai to Zanzibar then mpaka kufungua maduka mawili Dar es salaam ..
Kukutana na Recho msanii ,Prof Jay...na wengineo ...kutapeliwa 250 million na wabongo ...
Kuanza from scratch ...
Mpaka kuja kutoboa kupitia vifaa vya simu from China...
The guy is real struggle...

Sasa nakuwa mkuda likes kumi tuu Tuwasikilize wadhamini 😂😂😂😂😂😂
 
Aisee wapo sema humu sijui kama wapo, kuna Dada mmoja mchaga jina sitomtaja niliwahi kukutana nae hotelin sehemu moja inaitwa Mambasa njia ya kwenda kisangani ilikua safari yake ya kwanza lakini alibeba pea kibao viatu vya kimasai alikua anafuata dhahabu/ Oro mapori ya kisangani huko nilipotea miaka kama sita sijarudi kule siku moja nafika tena kisangani nikamuuliza dreva mmoja wa classic za Butembo kisangani huyu dreva anaitwa aggrey ni mtu wa songea, akanipa story za Dada yetu kumbe alikomaa akatoboa akawa ameshanunua truck Benzi kama nne hivi anafuata mizigo viwandani kenya kupeleka Congo, huyu sister hua napenda angekuja akasimulia siku moja maana hakua mdangaji alikua jasiri kwa mtoto wa kike hawa wa oya oya asingethubutu kukata mbuga moshi, uganda then congo bila kua na ndugu.
UMESHASEMA DADA WA KICHAGA. FULL STOP
 
SEHEMU YA TANO

Wakuu nitajitahidi kuandika kwa urefu na nitajitahidi kuandika kila kitu ili mtu mwengine aweze kujifunza kitu. Hata matukio yangu ya aibu pia nitawaeleza ili mtu ajifunze kitu kupitia story yangu na Kama kuna Makosa nilifanya basi iwe rahisi kwa mtu mwengine kujifunza na kurekebisha.

Nilivyorudi kwa yule Dada wa Uhamiaji, alifungua Passport yangu bila kusema chochote aligonga Mhuri nikaondoka zangu. Nikajua kumbe mwanzoni alisema vile ili kunitengenezea mazingira ya kutoa rushwa.

Nilivyotoka tu pale Kaunta, wale Vishoka wakanifuata ili niwarudishie ile Pesa yao, Kwacha 50. Kumbuka hapo nilikuwa bado sijabadili pesa za Kigeni. Nikawauliza wale Jamaa, Kwacha 50 ni sawa na shilingi ngapi za Kitanzania ili niwarudishie pesa yenu, wakaniambia "Wewe tupe Laki Moja tu"

Nikaona wananiletea Ujinga, nikatoka mpaka nje kwa Jamaa ambae alikuwa anawabadilishia watu fedha, Wale Vishoka wapo nyuma yangu tu. Nikataka kubadilisha Pesa yule Jamaa akakataa akasema "Malizana kwanza na hao Jamaa zako".

Nikamwambia kuhusu hawa Jamaa niachie Mimi, wewe nipe huduma tu ya Kubadilisha Pesa, Jamaa alikataa. Nikamwambia basi niambie Kwacha 50 ni sawa na shilingi ngapi za Kitanzania, Hata hilo nalo alikataa aliendelea kusema " Maliza kwanza na hao Jamaa".

Nikaondoka pale kurudi kwenye Bus ili nimuulize Dereva au Konda, Wale Vishoka wapo tu nyuma yangu. Dereva na Konda nao walikataa kutoa ushirikiano kwa madai ya kwamba nimalizane kwanza na wale Vishoka.

Hapo Vishoka wanatoa maneno yote ya Shombo. Lakini nilijifanya kama Siwasikii vile, mwisho wa siku nikawaambia oya nyie sikilizeni Mimi hiyo Laki Moja sina fanyeni mnachotaka kufanya. Tukaanza kuvutana vutana pale na kurushiana maneno. Abiria wengine wapo kimya wanatusikiliza tu.

Mwisho wa Mabishano nilikubali kuwapatia Elfu 50. Roho iliniuma sana. Nilijua fika hapa nimepigwa. Baadae nilikuja kujua kuwa Kwacha 50 ilikuwa kama Elfu Nane ya Kitanzania. Ndo hivyo nilishapigwa.

Baada ya wale Vishoka kushuka ndani ya Bus niliwauliza Dereva na Konda kwa nini walikataa kunisaidia. Wakaniambia kuwa wao ile njia wanapita kila siku na hao Vishoka wapo hapo Boda ya Tunduma miaka na miaka. Kwa hiyo kama wangenisaidia basi Bus lao lingefanya kazi katika Boda hiyo kwa tabu sana pengine wangeweza kutobolewa matairi kila watakapokuwa wanapita hapo. Kwa kweli niliwaelewa.

Aisee kumbe sikuwa peke yangu niliyepigwa usiku ule. Mara waliingia Abiria wengine na Vishoka wengine wakigombana kama ilivyokuwa kwangu. Moyoni nikasema hapa itakuwa kuna mchezo unachezwa kati ya Maafisa Uhamiaji na hawa Vishoka. Ndo mana wanaruhusiwa kuingia hadi ndani.

Tulilala ndani ya Bus hadi asubuhi ndo tukaendelea na safari ya kuelekea Zambia.
Hahhhhaaa ilishindwa hata kufanya convention kwenye simu kujua kwcha moja sawa na tsh ngapi? Siku nyingine usivuke boda bila kuchange hela mzee watu wale wKiwa upande wao wanKuwa wasumbufu balaa. Ila ungekuwa upande wa tz ungepewa ushirikiana hata na watoa change wa kibongo
 
Back
Top Bottom