Mtu unaleta uzi,kwa moyo wako kabisa mweupe tena hatujakuomba wala hata hatujuwi kama una uzi pendwa.
Unashusha episode kadhaa Mungu ni wa wote gafla uzi wako unapendwa watu wanaacha kazi, wanakopa bando, yaani kila dk,wanacheki uzi.
Halafu,gafla speed ya kushusha episode inaanza kupungua mara narudi, mara kesho mara yanapita masaa 24 kimya.
Hii tabia ni ukatali kama yalivyo matendo mengine ya ukatili.
Ukianzisha kitu kimalize kiishe raha ya story,isomwe ikiwa bado ya moto na bando zetu hazijachacha.
Ukileta uzi au,story,hlf usipate watu unajisikia vibaya,watu wakija unapotea mnaoleta uzi mnatuchanganya.
Tunaponunua kubando, tukatenga muda kusoma uzi kati ya hbr kibao zilizo humu JF ni mapenzi na uzi huo.
SAWA TUNAJUWA KUNA DHARULA, SHIDA MATATIZO,,MUDA NA MENGINE, UKIPATA DHARULA UKAHISI HUTAANDIKA KWA MUDA SAHIHI, TOA TAARIFA KUWA WADAU KUNA DHARULA NAOMBA SIKU 2 NIPUMZIKE NIDYO TUTAENDELEA. Huo ndiyo uislamu, na ndiyo ukiristo, na ungwana.
unapoleta kisa chako wazi inamaana kuwa unataka tujifunze jambo na kufurahia pia kulingana na story iliyoletwa.
WANAJF kabla ya kuleta story yako plz kaa tafakari na ufanya maamuzi kuwa naandika hii story,mwanzo mwisho iishe na nimejitolea kwa moyo wangu wote ukimaliza kiapo ndiyo unaanza kuandika.
Ukisubiri sana kitu hata ile radha yake inaanza kuisha.
MLETA UZI,,TUNASHKRU,KWA UZI WAKO, TUNASHKRU,KWA EPISODI 16,
LAKINI kaa tafakari kama tunaendelea basi tuendelee kama imeisha basi sema wazi,,kama una dharula sema wazi pia.
Kutuweka roho juu kama tunaoga njia panda siyo fair kabisa.
NB. wengine pia wenye nia za kuleta story,kabla ya kuleta kaa fanya maamuzi kiwa story hii niwasimulie au nikae nayo daima,, hbr za kusimulia mara mchango wa MB, mara unapotea siyo kitu sahihi.