SEHEMU YA NANE
Ukweli ndugu zangu moja ya kitu nilichojifunza kwenye Safari hii sio kwamba ukifika kila boda basi unakimbilia kutoa pesa. Unatakiwa kusoma kwanza upepo wa Boda husika.
Kwenye hii boda ya BeitBridge tulikosea kwa sababu pale Kaunta kulikuwa na Mkaburu. Wazoefu wanasema ukikuta pale Kaunta amekaa Mkaburu basi usikimbilie kutoa rushwa. Sababu wanasema Mkaburu hapendi sana watu weusi, hivyo ukianza tu kutoa rushwa ndo anapata sababu ya kutokukuruhusu kuingia nchini mwao.
Basi Mimi namshukuru mungu yule Mkaburu akaniangalia kisha akanigongea mhuri. Nakumbuka alinipa Mwezi mmoja tu wa kukaa South Africa. Wenzangu walipewa Wiki mbilimbili. Jamaa zangu waliniambia Mimi nilipewa Mwezi mmoja sababu yule Mkaburu aliona Passport yangu haijawai kugongwa Mhuri wa Africa Kusini. Wao walipewa siku chache kwa sababu Passport zao zishagongwa sana Mihuri ya Afrika Kusini.
Mpaka tunarudi kwenye Bus yule Jamaa etu walikuwa bado wamemshikiria. Tuliondoka tukamuacha pale, tena hata namba za simu tulikuwa bado hatujapeana. Mpaka kunakucha tulikuwa bado tupo njiani.
Ahamad aliniambia kama sina sehemu ya kufikia basi nishuke nae Pretoria. Kwa sababu Bus kabla ya kufika Joberg linafika kwanza Pretoria. Ahamad akasema tushuke wote hapo atanitafutia sehemu ya kukaa kwa jamaa zake ambae ni wabongo. Matlida yeye alikwenda kushukia Mwisho wa Bus kule Power House Karibu na Park Station Joberg.
Mimi na Ahamad tulishuka pale Pretoria kama saa Nane mchana. Ukweli nchi ya wenzetu ni nzuri sana.
Nilikuwa natembea huku najiuliza "Kama hapa pako hivi huko Ulaya na Marekani patakuwa vipi?" Watu wanajua kujenga nchi zao.
Ahamad alikuwa na miaka kama mitano toka atoke South hivyo tulivyoshuka tu tukawa tunapita mitaa Fulani ya washkaji zake anakwenda kuwasalimia. Mimi nipo nyuma yake tu. Nakumbuka tulikwenda mpaka mitaa Fulani kuna Wazanzibar wengi wana maduka. Tukaacha hapo mabegi yetu. Mimi nilikuwa sina imani kuacha hapo Begi langu lakini kwa kuwa ATM Card yangu ilikuwa mfukoni nikasema sio mbaya, kilichokuwa kinanipa wasiwasi peke yake ni vyeti vyangu vyote vilikuwepo ndani ya Begi. Ukishaamua kujilipua inabidi uwe na roho ngumu.
Tulivyofika hapo Pretoria ndo nikajua kuwa kumbe Ahamad alikuwa anaendelea na Safari ya kwenda Capetown. Hapo alikuja kukutana na Dada yake ambae wangekwenda wote Capetown kwa ndege. Huyo Dada yake alikuwa ameolewa huko Capetown na Tajiri mmoja. Maelezo yote hayo alinipa Ahamad mwenyewe.
Tukaenda mahali kukutana na Huyo Dada yake, naye ni Mtanzania. Nakumbuka alikuja na Range Rover mpyaa, tukaingia ndani, kisha Ahamad akanitambulisha kwa Dada yake. Dada yake akasema kwa kuwa wao walikuwa wanawahi kupanda ndege basi Mimi ataniacha kwa rafiki yake.
Hao mpaka kwa huyo rafiki yake, tulivyofika kwa huyo rafiki ake, Dada yake na Ahamad akaniuliza "Unamjua huyu". Mimi nikamjibu hapana simjui. Nikawa namwangalia vizuri yule Mrembo ambae nimepelekwa kwake. Nikajiridhisha kuwa simjui.
Dada yake na Ahamad akasema "Huyu ni Vailet, yule Video Queen kwenye Wimbo wa Matonya, ule wimbo wa Vailet, huyu ndo Vailet mwenyewe"
Duh nikabaki nimeduwaa tu, demu amekuwa mrembo kinoma noma. Kumbe Alishakimbiliaga South Afrika Kitambo sana. Wakuu ukitaka kumkumbuka vizuri huyu demu unaweza kuingia YouTube, Video ya Matonya wimbo wa Vailet, ndo huyo demu mule ndani. Mimi nikaachwa pale. Ahamad na Dada yake hao wakaondoka kuchukua mabegi wakaniletea Begi langu kisha wenyewe wakasepa Capetown.