Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

SEHEMU YA TATU

Nikafanya research kidogo nikaambiwa Benki inayopatikana kwa urahisi huko South afrika ni First National Bank (FNB), Kwa hapa Dar es Salaam hii Bank ilikuwa na Tawi lake Posta. Nikaenda mpaka Posta, Nikafungua Account, Nikaweka Akiba Kama ya Milioni Moja. Huyo Nikasepa zangu na ATM Card yangu. Niliona ni Salama zaidi kwenye hii Safari kutembea na ATM Card mfukoni kuliko kutembea na Million Moja Mfukoni ukizingatia safari yenyewe ni ndefu na niendako sipajui na wala simjui mtu.

Siku ya Safari ikawadia, Huyo mpaka Ubungo. Ukweli ile hofu ya kwenda mahali nisipopajua, na sina Rafiki wala ndugu ilinitawala sana, sema nilikuwa nimechoka sana kuishi Bongo mpaka nikasema liwalo na Liwe. Unajua katika maisha kuna wakati mtu unachoka kuishi sehemu moja, kupiga story zile zile kila siku na watu wale wale.

Hivyo safari ya kutoka Ubungo kuelekea South Africa ikaanza. Kwenye Bus Watanzania tulikuwa kama nusu ya Bus zima, Abiria waliobaki walikuwa Wakenya, Waburundi walikuwa wengi, wanawake kwa wanaume. Pia kulikuwa na Wazambia na Waangola waliokuwa wakirudi Makwao.

Ukweli kabla ya Safari hii, Sikujua kama pale Ubungo huwa kunapokea wageni wengi kiasi hichi. Sikujua kama Tanzania ni njia kubwa sana ya kuelekea kusini mwa Bara la Africa. Sikujua kama tunapokea Waburundi wengi hivi, Kila kitu kilikuwa kigeni kwangu.
Nimejifunza katika maisha unapaswa kuwa na uthubutu na pia uwekezaji[emoji123][emoji3590][emoji1666][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mm sikua najua raha yakr aisee siku 1 nilijaribu toka ifakara to rock city acha kbs yaani..raha mno! Sema inataka mapene

Afu Roadtrip inakua tamu kama hamjazidi watatu hivi, huku mko kwenye hata defender ina tent lenu juu, ndani mna soft drinks plus maboksi ya ceres kibao, unagonga huku unachungulia grants zako kwa jicho la mafanikio, maji katoni kadhaa, ngoma inaanzia songea inapumua kidogo makambako unachoma kuku kizushi then inajaza mafuta, gari inawekwa kwa mexisons inapigwa povu kiaina, ikikamata highway inakuja kusimama Dom kidogo, inanunua wine za bei ya jumla, inaamsha kwenye nyama bahi kidogo unakula mbuzi na whisky funda mbili tatu, ngoma inaenda kulala manyoni kuna lodge za maana, hapo asubuhi inakamta supu ya kuku wa kienyeji then inatembea vumbi vumbi inakuja kula Tinde hapo unapumzika gari unafungua milango yote ipate hewa vizuri, baadae. Ikitoka tinde ngoma inasound hadi kahama unashangaa phantom kidogo unapita masumbwe, Ushirombo, Runzewe ngoma inapandisha Bwanga, inakula geita unaenda kulala hapo kwanza unasoma upepo haya mbele utaendelea mwenyewe
 
SEHEMU YA NANE

Ukweli ndugu zangu moja ya kitu nilichojifunza kwenye Safari hii sio kwamba ukifika kila boda basi unakimbilia kutoa pesa. Unatakiwa kusoma kwanza upepo wa Boda husika.

Kwenye hii boda ya BeitBridge tulikosea kwa sababu pale Kaunta kulikuwa na Mkaburu. Wazoefu wanasema ukikuta pale Kaunta amekaa Mkaburu basi usikimbilie kutoa rushwa. Sababu wanasema Mkaburu hapendi sana watu weusi, hivyo ukianza tu kutoa rushwa ndo anapata sababu ya kutokukuruhusu kuingia nchini mwao.

Basi Mimi namshukuru mungu yule Mkaburu akaniangalia kisha akanigongea mhuri. Nakumbuka alinipa Mwezi mmoja tu wa kukaa South Africa. Wenzangu walipewa Wiki mbilimbili. Jamaa zangu waliniambia Mimi nilipewa Mwezi mmoja sababu yule Mkaburu aliona Passport yangu haijawai kugongwa Mhuri wa Africa Kusini. Wao walipewa siku chache kwa sababu Passport zao zishagongwa sana Mihuri ya Afrika Kusini.

Mpaka tunarudi kwenye Bus yule Jamaa etu walikuwa bado wamemshikiria. Tuliondoka tukamuacha pale, tena hata namba za simu tulikuwa bado hatujapeana. Mpaka kunakucha tulikuwa bado tupo njiani.

Ahamad aliniambia kama sina sehemu ya kufikia basi nishuke nae Pretoria. Kwa sababu Bus kabla ya kufika Joberg linafika kwanza Pretoria. Ahamad akasema tushuke wote hapo atanitafutia sehemu ya kukaa kwa jamaa zake ambae ni wabongo. Matlida yeye alikwenda kushukia Mwisho wa Bus kule Power House Karibu na Park Station Joberg.

Mimi na Ahamad tulishuka pale Pretoria kama saa Nane mchana. Ukweli nchi ya wenzetu ni nzuri sana.

Nilikuwa natembea huku najiuliza "Kama hapa pako hivi huko Ulaya na Marekani patakuwa vipi?" Watu wanajua kujenga nchi zao.

Ahamad alikuwa na miaka kama mitano toka atoke South hivyo tulivyoshuka tu tukawa tunapita mitaa Fulani ya washkaji zake anakwenda kuwasalimia. Mimi nipo nyuma yake tu. Nakumbuka tulikwenda mpaka mitaa Fulani kuna Wazanzibar wengi wana maduka. Tukaacha hapo mabegi yetu. Mimi nilikuwa sina imani kuacha hapo Begi langu lakini kwa kuwa ATM Card yangu ilikuwa mfukoni nikasema sio mbaya, kilichokuwa kinanipa wasiwasi peke yake ni vyeti vyangu vyote vilikuwepo ndani ya Begi. Ukishaamua kujilipua inabidi uwe na roho ngumu.

Tulivyofika hapo Pretoria ndo nikajua kuwa kumbe Ahamad alikuwa anaendelea na Safari ya kwenda Capetown. Hapo alikuja kukutana na Dada yake ambae wangekwenda wote Capetown kwa ndege. Huyo Dada yake alikuwa ameolewa huko Capetown na Tajiri mmoja. Maelezo yote hayo alinipa Ahamad mwenyewe.

Tukaenda mahali kukutana na Huyo Dada yake, naye ni Mtanzania. Nakumbuka alikuja na Range Rover mpyaa, tukaingia ndani, kisha Ahamad akanitambulisha kwa Dada yake. Dada yake akasema kwa kuwa wao walikuwa wanawahi kupanda ndege basi Mimi ataniacha kwa rafiki yake.

Hao mpaka kwa huyo rafiki yake, tulivyofika kwa huyo rafiki ake, Dada yake na Ahamad akaniuliza "Unamjua huyu". Mimi nikamjibu hapana simjui. Nikawa namwangalia vizuri yule Mrembo ambae nimepelekwa kwake. Nikajiridhisha kuwa simjui.

Dada yake na Ahamad akasema "Huyu ni Vailet, yule Video Queen kwenye Wimbo wa Matonya, ule wimbo wa Vailet, huyu ndo Vailet mwenyewe"

Duh nikabaki nimeduwaa tu, demu amekuwa mrembo kinoma noma. Kumbe Alishakimbiliaga South Afrika Kitambo sana. Wakuu ukitaka kumkumbuka vizuri huyu demu unaweza kuingia YouTube, Video ya Matonya wimbo wa Vailet, ndo huyo demu mule ndani. Mimi nikaachwa pale. Ahamad na Dada yake hao wakaondoka kuchukua mabegi wakaniletea Begi langu kisha wenyewe wakasepa Capetown.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Hahah imagine kati ya mambo yote wameona pajama tu. Nafahamu sana walichokuwa wanataka nami sijataka kuwapatia!

Mpigie simu keagan aje basi.....
keagan kasusa sijui........


em endelea na story yako bana tusimulie mazuri ya huko kitu gani ulikipenda sana huko??


kitu gani kilikuboa huko......???


tuende na sisi kihisia....Bwana keagan anatuchelewesha

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
keagan kasusa sijui........


em endelea na story yako bana tusimulie mazuri ya huko kitu gani ulikipenda sana huko??


kitu gani kilikuboa huko......???


tuende na sisi kihisia....Bwana keagan anatuchelewesha

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Utaniponza kwa hakika 😀 Tuvute subira tumsubiri Mtoto wa mstaafu arudi.
 
Mkuu endelea basi na mambo ya pajama, maana keagan kakimbia, wewe endelea tu pale mlipopishana umevaa pajama lako mwenyewe unaenda dukani hauna habari vipi ulivuka barabara na pajama lako au ilikuaje?
Hahah msubiri keagan atakuja, kuwa mvumilivu ndugu. Halafu mimi sikwenda dukani, sikwenda mbali wala sikutoka nje, nilikwenda floor ya chini. Nachelea kusema haukunielewa.
 
keagan kasusa sijui........


em endelea na story yako bana tusimulie mazuri ya huko kitu gani ulikipenda sana huko??


kitu gani kilikuboa huko......???


tuende na sisi kihisia....Bwana keagan anatuchelewesha

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Hawa jamaa huwaga wakisifiwa wanakula kona...
inatakiwa wamwage story kama bujibuji....
bujibuji akilianzisha mpaka mnakoma na story
 
Back
Top Bottom