Tatizo la watu humu JF wanapenda kusikia kile wanachotaka kusikia. Mtu ukiwa na mawazo kinzani kidogo japo ya kuwasaidia wanakuona kama umekuja kuharibu stori wakati hayo mawazo huenda yakawasaidia vijana ambao wengependa kujaribu bahati zao nje ya nchi. Story ya bwana Keagan Paul ni nzuri sana na inatoa darasa kwa vijana wenye ndoto za kutaka kusaka maisha nje.
Tatizo kuna details ambazo kuna watu humu huenda wakazichukua kama zilivyo bila kuchanganya na za kwao wakajikuta matatani. Naweza kusema bwana Keagan alikuwa na bahati sana tena sana, nadhani waliokaa South Africa watakubaliana na mimi kuwa alikuwa na bahati sana. Kitendo cha kuishi bila permit halafu unajiachia hivyo ni bahati sana kusurvive.
Kwa hiyo vijana wale mnaotaka kwenda huko muwe makini, bwana Keagan kama aliweza kujiachia bila permit msidhani maisha ndio yako hivyo, utadakwa dakika moja tu na kupelekwa sehemu inaitwa Lindela kusubiria kuwa deported. Kama nilivyosema kitendo cha kusafiri kwenda Lesotho wakati viza imeexpire ni bahati ya mtende na pia nampongeza sana kwa huo ujasiri.
Viza ikiexpire ukiwa ndani ya nchi ni kesi kubwa sana halafu akaamua kusafiri kwenda nchi nyingine wakati anajua hata kibali cha kuwemo nchi husika hana, huo ni ujasiri mkubwa sana na nachelea kumpa pongezi maana alikuwa kama anajiweka kwenye mazingira ya kurahisisha ukamatwaji wake.
Kwanza najiuliza walifikaje boarder ya Lesotho bila kukutana na roadblock hata moja na kukaguliwa ID zao? Pili yule immigration officer wa upande wa South Africa aligongaje exit stamp bila kumkamatisha kwa kosa la kuishi nchini illegally, najua amesema aliweka rand 300 kwenye passport.
Haya wakati wa kurudi aliwezaje kuingia tena SA wakati viza ilishaexpire? Bwana Keagan ukipata muda naomba uelezee kidogo kuhusu issue ya kutoka na kuingia tena South Africa wakati viza imeisha ili vijana wajifunze maana kuna wengine wanaweza kudhani kuishi bila vibali South Africa sio tatizo wakati ni tatizo kubwa sana linaloweza kuwapeleka jela.
Viza ikiexpire kisheria huwezi kurenew ukiwa ndani ya ardhi ya South africa hata kama unatoka SADC lazima utoke nje, na utapata misukosuko sana.