Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Wadau kwani haiwezekani uzi kufutwa maana kusudi lake halijatimiziwa na haielekei kutimizwa zaidi zaidi unatia hasira tu kwa wale wanaotaka kujifunza halafu story inaishia kati bila taarifa yoyote.

Mnaonaje mods wakafuta nyuzi kama hizi wakianza na huu.

NAWASILISHA
 
@konda msafi nadhani bado hajakumbana na changamato za kwenye Maboda, kwa hiyo hawezi kuelewa hii michezo, ila kikubwa mtu mzuri ni yule anayejipa nafasi ya kujifunza na sio kujifanya unajua kila kitu
Sasa je unamaliza story au umalizi
 
Mimi pia natafuta kazi msaada wenu
Naitwa kassim
Naishi dsm mbagala
Yoyote hata kuuza chips na zingine zisizo na elimu

0714945058
 
Mkuu mtoto wa mstaafu, Keagan Paul, naomba uniruhusu nicomment kidogo. Kuna vitu kwenye stori yako havipo sawa kidogo, naelewa huenda labda umeamua kuvifanya visiwe sawa kwa maksudi na si kwa bahati mbaya. Kuna sehemu nimekusoma unasema wale jamaa wanaomuuzia "nyaupe" jamaa Y wanafanya kazi kama punda. Hapo mzee umepindisha ukweli, Dizonga hakuna wabongo wanaokula bata kama wauza nyaupe. Kufanya kazi kama punda kwako wewe labda kuna tafsiri gani? Maana hao jamaa kazi yao ni kupokea simu tu na kupeleka mzigo location unapohitajika na akifika pale ni kitendo cha sekunde mbili keshamaliza kazi, haina hata kuhesabu hela, hela itahesabiwa baada ya kuondoka eneo la tukio, na wale wanunuzi ni waamifu sana hawatoi hela pungufu japo hamuhesabiani eneo la tukio. Zaidi ya yote jamaa wana usafiri hawasambazi kwa miguu, hata kama mtu ameanza kuuza leo haiwezi kumchukua zaidi ya mwezi hajapata usafiri, sasa unaposema wanafanya kazi kama punda kidogo kama umepindisha uhalisia. Pia umesema huwa wanaweka hizo kete mdomoni na polisi wakivamia wanazimeza, mzee hii pia sio kaka. huwezi kumeza madawa kizembe hivyo. Donga ndio zinamezwa wakati wa kuzisafirisha intercontinental lakini sio mzigo umeshafika ndani ya nchi bado mtu ameze. Hiyo risk hakuna mtu wa kuitake, kwanza ufungaji wa hizo kete sio imara sana uimeze halafu ubaki salama. Ufungaji wa donga ndio imara unaweza kumeza na ukasurvive lakini sio kete mkuu. Halafu mademu wa Gauteng yaani Joburg na Pretoria wana attitude flani tofauti na uliyoielezea tena kama hapo Midrands ndio kabisa. Nimekaa Randburg kama miaka 6 au 7, 209 Bellairs Drive, Banbury Cross, North Riding. Randburg nadhani kwa Johannesburg ni sehemu wanayokaa matajiri wa South Africa ukitoa Sandton na Fourways. Ninachotaka kusema hapa mademu wa kishua wa Gauteng nazijua attitude zao maana nimeishi nao. Pia umesema permit (viza) yako iliexpire ukiwa bado kwa bwana Y, sasa uliwezaje kutafuta kazi wakati tayari ulikuwa unaishi kinyume cha sheria maana kitu cha kwanza lazima wakuulize ID yako. Mind you Johannesburg na Pretoria ni miji ambayo kama huna permit ni ngumu sana kusurvive. Joburg hata ukiwa unatembea barabarani unaweza kushitukia tu unasimamishwa na police na kuombwa ID tofauti na miji mingine kama Durban, sasa wewe uliwezaje kutafuta kazi wakati hata permit yenyewe huna? sijui kama umenielewa? Na kwa Johannesburg misako ya kutafuta wahamiaji haramu ipo kila uchwao.
Mkuu hapa Duniani Hakuna linaloshindikana Ni kweli yote hayo yapo but aliyakwepa na sio kila Sheria inakukamata.Fata story hayupo Cort.
 
Mtu unaleta uzi,kwa moyo wako kabisa mweupe tena hatujakuomba wala hata hatujuwi kama una uzi pendwa.

Unashusha episode kadhaa Mungu ni wa wote gafla uzi wako unapendwa watu wanaacha kazi, wanakopa bando, yaani kila dk,wanacheki uzi.

Halafu,gafla speed ya kushusha episode inaanza kupungua mara narudi, mara kesho mara yanapita masaa 24 kimya.


Hii tabia ni ukatali kama yalivyo matendo mengine ya ukatili.

Ukianzisha kitu kimalize kiishe raha ya story,isomwe ikiwa bado ya moto na bando zetu hazijachacha.

Ukileta uzi au,story,hlf usipate watu unajisikia vibaya,watu wakija unapotea mnaoleta uzi mnatuchanganya.

Tunaponunua kubando, tukatenga muda kusoma uzi kati ya hbr kibao zilizo humu JF ni mapenzi na uzi huo.

SAWA TUNAJUWA KUNA DHARULA, SHIDA MATATIZO,,MUDA NA MENGINE, UKIPATA DHARULA UKAHISI HUTAANDIKA KWA MUDA SAHIHI, TOA TAARIFA KUWA WADAU KUNA DHARULA NAOMBA SIKU 2 NIPUMZIKE NIDYO TUTAENDELEA. Huo ndiyo uislamu, na ndiyo ukiristo, na ungwana.

unapoleta kisa chako wazi inamaana kuwa unataka tujifunze jambo na kufurahia pia kulingana na story iliyoletwa.


WANAJF kabla ya kuleta story yako plz kaa tafakari na ufanya maamuzi kuwa naandika hii story,mwanzo mwisho iishe na nimejitolea kwa moyo wangu wote ukimaliza kiapo ndiyo unaanza kuandika.

Ukisubiri sana kitu hata ile radha yake inaanza kuisha.

MLETA UZI,,TUNASHKRU,KWA UZI WAKO, TUNASHKRU,KWA EPISODI 16,

LAKINI kaa tafakari kama tunaendelea basi tuendelee kama imeisha basi sema wazi,,kama una dharula sema wazi pia.

Kutuweka roho juu kama tunaoga njia panda siyo fair kabisa.

NB. wengine pia wenye nia za kuleta story,kabla ya kuleta kaa fanya maamuzi kiwa story hii niwasimulie au nikae nayo daima,, hbr za kusimulia mara mchango wa MB, mara unapotea siyo kitu sahihi.
Poleee umeandika kwa uchungu zaidi ya ule wa Labor
 
Back
Top Bottom