Nilivyomkomesha tapeli wa viwanja Kivule Dar es Salaam

Nilivyomkomesha tapeli wa viwanja Kivule Dar es Salaam

Hakimu gani uyo Ana njaa hivyo,elfu 50?hakimu?
Tuliza rinda kala laki yule bwege,nimemtangulizia 50 bdae uko mbele akamaliziwa,hawa kama marefa tu ushamba wako ndio utatoa kibunda kikubwa,wewe mpya nini mjini? Rushwa kwani inatakiwa utoe bei gani? Nadai M3 nitoe M?
 
Jamaa hadi aliwaelezea wadau wake kule kuwa dah sijawahi kuwa na pambano gumu kama la yule jamaa,nimepiga misumari wee wapi kumbe hajui UCHAWI HAUENDI KWA MENTALI! kuna siku mahakamani alitaka kunichota nyayo mchangani nikamwita nikakanyaga,nikamchotea mchanga nikampa,akawa ananitizama tu MAE!
Hadi hao watu wana hizo mambo zan👽👽👽👽 kumbe ???😳😳!
Duuh!!
 
"Kasangu ndugu unasikia hayo maneno? We unayaona yanatoka tu mdomoni na unadhani kutakuwa hakuna utekelezaji? Please mpe pesa yake tusije kuingia matatizoni wote,"🤣🤣🤣 Muheshimiwa hakutaka fedhehaa😂😂😂😂! Ukute alishakula rushwa kadha wa kadha hapoo khakha!!
Kichaka chao cha upigaji na ndio yule hakimu hadi leo amepigwa ban kwa rushwa!
 
Tm
Loyality, umembebesha rafiki yako zigo zito sana, huo ni ubinafsi, ungeweza pata matokeo mazuri kwa kuwa civil tu
umesoma mpaka mwisho? Nilichokitaka ndicho nilichokipata na huyo mshkaji wangu juzi tu hapa kanitumia mafuta ya alizeti vidumu vi3,hakuna ovu lolote lililotokea,adui ni yule hakimu wa pale Madafu ndugu soma mpaka mwisho haki yangu imepatikana hayo unayoyahubiri sasa ndio yangenigharimu,
 
Loyality, umembebesha rafiki yako zigo zito sana, huo ni ubinafsi, ungeweza pata matokeo mazuri kwa kuwa civil tu
Ebu shauri katika hujuma zote nilizokuwa natendewa ungekuwa wewe ungefanyaje? Tena nilimshirikisha kabla sijamfata yule hakimu,mwanangu yule yuko peace sana tena kuna deal ananipa yeye hadi sasa,napiga pesa na maisha yanaenda! Yule wa dar hakutakiwa kutendewa wema na kama umesoma hadi mwisho hv sasa kasimamishwa kazi kwa tatizo hilo hilo je kisa ni mimi?
 
Kweli matapeli wapo wengi ila unaongeza risk kwa kusainia saiti na mihuri hapo hapo.

Sainisha mikataba kwenye ofisi inayoeleweka ya mtendani nk itakusaidia hata ukiwa na kesi....
Usijidanyanye ndugu, nunua surveyed plot na uhakiki arthi hiyo ndio solution
 
Tuliza rinda kala laki yule bwege,nimemtangulizia 50 bdae uko mbele akamaliziwa,hawa kama marefa tu ushamba wako ndio utatoa kibunda kikubwa,wewe mpya nini mjini? Rushwa kwani inatakiwa utoe bei gani? Nadai M3 nitoe

Tuliza rinda kala laki yule bwege,nimemtangulizia 50 bdae uko mbele akamaliziwa,hawa kama marefa tu ushamba wako ndio utatoa kibunda kikubwa,wewe mpya nini mjini? Rushwa kwani inatakiwa utoe bei gani? Nadai M3 nitoe M?
Namuongelea hakimu kua na njaa,Tena Hadi anakufuata,Tena unamrushia kwenye simu,uyo hakimu njaa yake ni hatari ,siongelei rushwa ,usijione mjanja hakuna asiyejua hayo,una tabia za kishoga ,jiangalie ,usijibu ambavyo ujaulizwa ,unless umedanganya ndio maana unajishtukia.scumbarg
 
Ndugu zangu majina yote niliyoyataja humu hakuna hata la kutunga yote majina ya wahusika sahihi na kama nadanganya nenda pale kivule njia panda ya shule ulizia huyo jamaa JUMA KASANGU! Ni mbwa ni mbwa ni mbwa sana Hakuna kilichoongezwa hapa thats why umeona thread imekwenda smooth ,nawashukuru sana kwa mshikamano wenu na ntaleta nyingine kuelezea safari yangu ya kwenda South 2008,hatari na nusu na robo
 
NILIVYOMKOMESHA TAPELI WA VIWANJA KIVULE


Sehemu ya 6


UTAJUA HUJUI

Yule mshkaji wangu wa Singida dah nilimuonea huruma kwani alijuta kuniunganisha katika lile jambo na akawa amemueleza mshkaji na mshkaji akawa anajitetea kuwa mara nyingi ninapompigia anakuwa kwenye maombi au bize kupitia kesi ambazo yeye akiwa kama mkuu wa mahakama pale aweze kuzitolea ripoti,nikamtumia ule ujumbe wa tigo pesa na yeye nikamwambia sikublack mail ila tambua simamia tulichopatata na najua umekula pesa wewe na wazee wako wa baraza sasa mimi ntakuja kuitoa kesi hapo kuipeleka mbele kwakuwa sina imani na mwenendo mnaoupeleka dah jamaa akaniomba sana msamaha ndio nikawaza inawezekana mtu akisema hana imani na mahakama husika waliopo pale kunawaletea picha chafu basi sasa ule mramaha wake ndio kama ulimponza sasa nikawa hakimu mimi yeye ndio mshtaki😂😂 na nikamwambia nataka siku ya date mshtakiwa awepo sijui utampataje na akubali kosa na alipe changu (hapo nshaclaim gharama zote zimefika M3.3) we bwana pema hapa ninapohadithia siku ya siku nimekaa benchini mtuhumiwa kaja na ndugu zake wawili wakike na wakiume wakaniita nje wakaniomba sana sana nikawambia nyie wekeni m3.3 ubaoni mi nabwaga kesi wakawa wanataka wanipe kwa awamu tena kianzia laki 5 nikawaambia kampeni hakimu hiyo pesa mi ninataka nipoteze tu wakatoka wamelowa! Muda wa kesi tukaitwa na alipoulizwa alipokuwepo akadai alikuwa anaumwa nikanyoosha mkono naomba kupata vielelezo vya hospitali akasema alipelekwa kwa mganga! Dah dunia hii nyie acheni,mheshimiwa akapotezea akaendelea na kesi mara mtuhumiwa akanyoosha tena mkono akamawambia hakimu yeye amekubali kosa na yuko tayari kunilipa ila sio hiyo pesa yote kwani mimi nilimpa yeye M2 tu (alijichanganya wakati mimi nimempa M1.3 na vichenji,sikuwa nimemalizia) na ananiomba twende mimi na yeye kule site kuhesabu gharama zangu za ujenzi kujua gharama halisi nikakubali na kesho yake nikatakiwa kwenda nae kule kwa mama Anna Mkapa.
Asubuhi nampigia kujua tunakutanaje akanambia wala nisiende yeye kaamua atalipa tu hayo madai yangu anaona tutasumbuana,nikaendelea na shughuli zangu kusubiria siku ya kwenda kule mahakamani.Siku ikafika na muda wa kuingia tukaitwa wakati hakimu anatuuliza natoa maelezo akanikana na kusema yeye hajaniona wala sijampigia dah kama mtu ameiona ile sinema ya kihindi ANDHAL KANOON ndio nilikuwa natamani pale Amita Batchan alipomshindilia bisu yule mzee ndio nilitamani nifanye pale yaani nilitoa maneno ambayo wote pale walibutwb nikamwambia "mheshimiwa naona danadana zimekuwa nyingi sasa nasema mbele ya mahakama hii nikijua wazi kama kutamka maneno ya kutishia kudhuru ni kosa kisheria ila hadi muda huu huyu jamaa keshaharibu maisha yangu,utu wangu,muda wangu na anaendelea kuniletea dharau sasa kwakuwa kadhamilia kuharibu maisha yangu basi ingawa sijawahi kuua ila huyu jamaa familia yake haitokaa salama nipo tayari kwa lolote kutoka sasa na wewe nakuachia ukumbi hukumu hii kesi kwa mizani yako unayoona sawa" dah hakimu jasho linamtoka na yule bibi akadakia unatishia mbele ya mahakama,kiujasiri nikamjibu simtishi na hii kesi ndio itakuwa yake ya mwisho kuja hapa wakati huo sio yeye wala mimi tunaojua litakalotokea! Bibi ananitizama huku natetemeka nasema kama mbwai iwe mbwai!
Hakimu akawa ananiplease kaka acha hasira,acha hasira haki yako utaipata ndugu haya yanazungumzika nikamjibt mimi sitaki huruma ya mahakama wewe toa hukumu tu,akawa anamwambia Kasangu ndugu unasikia hayo maneno? We unayaona yanatoka tu mdomoni na unadhani kutakuwa hakuna utekelezaji? Please mpe pesa yake tusije kuingia matatizoni wote,Kasangu akawa kakaa kimya na mheshimiwa akapiga date ndefu kama mwezi kamili!
Sasa wakati tunatoka ukiwa unaelekea pale kituoni kupanda daladala mimi na ndugu yangu yule Juma Kasangu akawa nae anakuja na ndugu zake akawa ananiambia "mtani mtani we mtani wangu bwana usikasirike ebu njoo tuyajenge bwana" haloo ilinitoka ngumi hiyo Juma chini! Nikamtimba kifuani yule ndugu yangu akanipush nikamponyoka nikawa namfata tena kuendelea kumchapa akanyanyuka akawa anakimbia kurudi kule mahakamani yeye mbele mimi nyuma hadi kati viunga vya mahakama akadumbukia ndani mimi nikageuza nikaondoka zangu wale ndugu zake wananitizama tu wanaogopa hata kufunua midomo yao.
Usiku hakimu akanipigia ooh kaka usifanye hivyo punguza hasira nikamwambia kavukavu nyie kuleni pesa ila mtajua tu siku moja uchungu tunaoupitia tunaodhulumiwa, akaniomba sana nikamwambia haki isipotendwa ama zake ama zangu na huyo fala.
Baada ya mwezi tukaenda tena mahakamani Juma hajaja,ikapigwa date hajaja tena,date ya tatu ndio kama alafu sasa anasema atalipa kwa awamu sita nikasema pesa yangu haikuwa mkopo nataka yote kila mtu akaendelee na hamsini zake na hakimu akamsisitizia kama amekubali kulipa alipe yote kikubwa atoe tamko ni muda gani,nikadakia iwe ndani ya mwezi (natamba mie tena hakimu na mtuhumiwa wote wapo kiganjani)wakakubali hivyo nikapewa tarehe kama ile kwa mwezi unaofuata,tukatakiwa twende kwa mhasibu wa mahakama kwenda kuandikishiana kumbe wakati wote huyo mama mhasibu alikuwepo pale mlangoni anafatilia tena ile kesi ikawa ikifika muda wa kusomwa ingawa ilikuwa inasomwa chumbani watu wengi walikuwa wanajaa hadi hakimu anawaomba wapungue pale mlangoni.
Tulipofika pale yule mama mhasibu akawa ananiambia "wewe mjinga badala ya kuchukua hata kidogo kidogo unakataa,utasumbuka" nikamjibu "mama fanya kazi yako kitengo chako cha hesabu pesa hauna shea nayo mama yangu"
Akakaa kimya akatuandikia maelezo nikaondoka zangu.
Mwezi uliofata nikatimba eneo la tukio na mwanangu tukahesabiwa mpunga wetu alafu yule mama mhasibu akawa ananambia "sinywi hata soda" nikamjibu "mama we nisamehe tu mimi sidili na upande wa upinzani" akanipa makaratasi nikasaini nikatia pesa kwenye begi nikaenda na kwa hakimu kuna makaratasi nikasaini nikatoka na mwanangu hao,nikampigia Chacha nikamuukiza nikulindaje akasema wewe usijali nipe 50 kibingwa na yule Marwa nikamtia 50 nae nikasepa zangu

IMEISHA HIYO

NB:Yule hakimu miaka michache mbele alikamatwa kwa kesi ya rushwa na hadi leo hajarejeshwa kazini kwakuwa malakamiko yalikuwa mengi sana juu yake tena ni rafiki yangu fb eti nae anaweka nyimbo za mapambio kujifanya mwema😂😂 kuna siku nikacomment katika moja ya post yake "PRACTICE WHAT YOU PREACH!" Ila kitambo sijamcheki kama bado anapost post na akiendelea kupost kujifanya mwema mtamuweka hadharani NWAMA YULE! MLA RUSHWA NA MPOTEZA HAKI ZA WATU! (nilitaka kuandika za wanyonge nikajipima nikagundua simo kundi hilo)

IMEISHA WANDUGU!
Hongera sana mkuuu! Ungekubali kupokea kidogo kidogo ingekua mlolongo tena!!
Big up 💪👍👍👍👍!
 
Ndugu zangu majina yote niliyoyataja humu haktwna hata la kutunga yote majina ya wahusika sahihi na kama nadanganya nenda pale kivule njia panda ya shule ulizia huyo jamaa Juma Kasangu! Hakuna kilichoongezwa hapa thats why umeona thread imekwenda smooth ,nawashukuru sana kwa mshikamano wenu na ntaleta nyingine kuelezea safari yangu ya kwenda South 2008
Namuongelea hakimu kua na njaa,Tena Hadi anakufuata,Tena unamrushia kwenye simu,uyo hakimu njaa yake ni hatari ,siongelei rushwa ,usijione mjanja hakuna asiyejua hayo,una tabia za kishoga ,jiangalie ,usijibu ambavyo ujaulizwa ,unless umedanganya ndio maana unajishtukia.scumbarg
soma uelewe usinilazimishe nitukane,hakimu wapi kanifata? Kaja mtaa Arusha gym hapo kanifata? Dah ebu kaa kimya soma thread uinjoy achana na mambo madogo madogo ndugu
 
Ndugu zangu majina yote niliyoyataja humu hakuna hata la kutunga yote majina ya wahusika sahihi na kama nadanganya nenda pale kivule njia panda ya shule ulizia huyo jamaa JUMA KASANGU! Ni mbwa ni mbwa ni mbwa sana Hakuna kilichoongezwa hapa thats why umeona thread imekwenda smooth ,nawashukuru sana kwa mshikamano wenu na ntaleta nyingine kuelezea safari yangu ya kwenda South 2008,hatari na nusu na robo
Duhh nadhani hio ya kutaja majina halisi haijakaa vizuri mkuu bora ungefucha majina!
 
Hilo eneo nimeishi sana , nadhani ni miongoni mwa maeneo ambayo watu wengi wamedhulimiwa viwanja kwa hapa Dar ila siku hizi mambo safi.
 
Niliuziwa kiwanja kwa njia za utapeli, nikaitafuta haki yangu polisi mpaka mahakamani na hatimaye niliipata haki yangu licha ya rushwa iloyotamalaki katika vyombo husika.


The whole story in few words .😊
 
Back
Top Bottom