NILIVYOMKOMESHA TAPELI WA VIWANJA KIVULE
Sehemu ya 4
USIKU WA DENI ULIPOFIKA
Ilipofika mida ya saa 10 yule bwana Chacha akiwa ameshatangulia kule Kivule na maskani yao hasa ilikuwa pale Kivule njia panda ya shule kuna kipub yule Kasangu alikuwa amekifungua na mara nyingi amekuwa akipatikana hapo ndipo bwana Chacha alipopapanga kama eneo la kufanyia tukio na sisi huku tukawa tunajipanga na nikamfata ndugu yangu flani ambaye alikuwa anafanya shughuli ya ufundi wa magari anaitwa Meddy ambaye alitutaka kuweka mafuta kwenye gari na tungekwenda sote yaani mimi,Kindamba na Meddy kuelekea Kivule,ilipofika muda wa saa 11.30 tukatoka kuelekea uko na katika majadiliano ikaonelewa mimi nishukie eneo linaloitwa Bambucha na wao wangekwenda wenyewe kupitia mwongozo wa Chacha ambaye alishakuwa tayari ameshafika kule Kivule na walipofika pale wakiwa wanawasiliana na hatimaye kukutana naKasangu wakamtaka awapeleke kwenda kutizama maeneo na kuyakagua na ikiwapendeza ndio wakae chini kujadili bei na namna gani ya kufanya malipo sasa yule Kasangu wakati wa kutakiwa hivyo akawa anataka kuwapa vijana wake ndio wawapeleke wale jamaa zangu na akawa anataka kupanda pikipiki ambayo ilikuwa imepaki pale kwenye pub yake ndipo yule Kindamba akamfata na kama aliyepatwa na machale Kasangu akashuka na kuanza kutoka mbio nasikia wakaanza kumkimbiza na akaenda kujikwaa kwenye kisiki na mguu wake mmoja ukawa umejeruhiwa na damu ikawa zinamtoka sasa yule Kindamba akawa anaact kama yeye ni askari akamwambia kimbia nikumwage ubongo na akawa anaomba msamaha na akawa anagugumia na kuka chini,wakambeba msobemsobe na wale kina Chacha wakawa wanawauliza kina Kindamba imekuwaje tena?[emoji23] wakawaambia kuwa huyu ni tapeli na tunaondoka nae na mtaenda kujulia uko Staki shari,sasa yule Kasangu hadi anakamatwa pale hakuwa anajua amekamatwa kwa kosa alilomtendea nani kwakuwa ni mtu wa matukio sana na akawa anaumiza kichwa hawa ni wa nani niliyemtapeli? Wakamtia garini na kuelekea nae Staki shari na wakanipitia pale Bambucha sasa wakati wanasimama na mimi kupanda dah jamaa alichoka sana akajisemea moyoni kweli huu mziki niliouingia safari hii HAPATOSHI!
Nikapanda garini na akawa ananiomba sana awapigie ndugu zake kujua namna gani tunalimaliza lile shauri nje ya polisi,nikamwambia sina njia yoyote zaidi ya kutaka pesa yangu na kama anaendelea kuzingua polisi itamuhusu tena nikamwambia nataka hao matapeli wenzake salama yake walete M3 kamili ndio nimdamp sasa toka saa 1 usiku hadi saa 3.30 tumepaki gari pale ukivuka reli ya njia panda ya Segerea,ilipofika 3.30 wakiwa wenzake wawili wamekuja mmoja akijitambulisha kama mjomba wake[emoji23] kumbe tapeli mwenzake anajifanya kutoa viapo hapo wee nikawa najiambia wewe apa miungu yako yote huyu atafika eneo la tukio kama hamtatoa pesa yangu,baada ya kuona sound zimekuwa nyingi nikamtuta yule bwana hadi Staki shari na kufika kaunta askari anaanza kunifokea mbona umemuumiza bila ya kuhoji imekuwaje (alikuwa anajuana nae akataka kunitingisha) nikamwambia muulize mwenyewe imekuwaje na Juma akamwambia alikuwa anakimbia akajikwaa ndio akaniuliza tatizo nami nikamueleza akanitaka nimpe RB# nikatoa kitochi changu cha Nokia upande wa meseji kwenye draft uwa nasave baadhi ya vitu vyangu muhimu na namba hizi nilizisave huku,nikampatia atamzungusha na kumuweka selo akanitaka nifike kesho yake asubuhi,nami nikatoka pale na nikamjuza kwa simu yule mzee Juma kuwa mtuhumiwa yupo pale na ninaondoka zangu
Asubuhi na mapema nikafika Staki shari nikamkuta yule mzee amenuna hata sikujua kwanini akawa ananambia nenda Madafu uko ukamalizane na jamaa yako (Madafu ni mahakama ya mwanzo Ukonga inayohudumia maeneo yale yote)mi nikatoka zangu nikaelekea kule mahakamani muda kama wa saa 2 hivi gari la kubeba watuhumiwa likawa limefika na nikawa nimekaa pale niko mwenyewe tu,watu wakawa wanaitwa na wenye kuachiwa kwa dhamana wanaachiwa,wenye kushinda wanaondoka na wenye kufungwa wanafungwa hadi mida ya saa 8.30 ndio tunaitwa kumbe pale utaratibu wao flesh case zote wanaziweka mwisho,njaa inaniuma ila hata kwenda kujiibia kwenda kula naogopa isije akaitwa nami sipo eneo la tukio,wakati naelekea mahakamani asubuhi kutoka Staki shari kuna mshkaji wangu mmoja yeye ni hakimu uko eneo flani mkoa wa Singida (naomba nisitaje eneo kumuhifadhi) huyu ni mshkaji wangu sana tumefanya mambo mengi ujanani ya hatari na mazuri sasa nikamvutia uzi kumpa habari kuhusiana na hii ishu akanambia bob we nenda pale hakimu mfawidhi wa pale mwanae sana wamesoma wote intake moja uko Lushoto mambo ya uhakimu nikamwambia poa Imeisha hiyooo!!
Tumekaa pale mara tukaitwa ndani katika kichumba alikuwepo hakimu na wazee wawili wakike na wa kiume ambao ni wazee wa baraza (walaaniwe wale wazee) na mdada aliyekuwa akichukua maelezo tuliyokuwa tunayatoa pale na mheshimiwa akaletewa faili na yule mdada na akatuita majina kuhakiki kama ndio kesi husika na waliopo mbele ndio wahusika wenyewe na alipojiridhisha akamsomea shtaka yule Kasangu na akakana pale na mheshimiwa akaaghilisha kesi kwa muda wa wiki 2 toka siku ile na wakati anaaghilisha palepale nikamuuliza jina lake akanitajia,kumbe ni yule yule mwanae mwanangu nikajua MBUZI KAFIA KWA MUUZA SUPU! nilijidanganya![emoji23]
Itaendelea!