Nilivyomkomesha tapeli wa viwanja Kivule Dar es Salaam

NILIVYOMKOMESHA TAPELI WA VIWANJA KIVULE

Sehemu ya 3

KAMA NOMA NA IWE NOMA

Siku ya jumatatu asubuhi na mapema nikiwa na akili zangu za usiku nikatoka zangu Magomeni kuelekea pale Staki shari mapema tu moja kasoro kadhaa niko pale nikawakuta maaskari wanajipanga kwa ajili ya lokoo ya kuanza siku mpya na kulikuwa na kiongozi wao yeye akiwa amevaa combat kama za wale field force mtu mzima hivi mfupi na mweupe kiasi nikamngojea awakague wale maaskari na nikamwendea nikidhani ndio mkuu wa kituo nikamsalimu na kumuelezea changamoto zangu na akanambia yeye sio mkuu ila nipite pale kolidoni na nikate kulia nisome vibao juu ya milango na nikae nje ya mlango ulioandikwa MKUU WA KITUO,nikamshukuru na nikaingia ndani kufata maelezo niliyopewa,nilipofika kaunta askari aliyekuwepo akaniuliza ninapoenda na nikamuelezea ninapoenda,nikasoma vibao na nikafika eneo husika uzuri wake kulikuwa na kibenchi nikakaa pale kimya,sasa wakati nimekaa pale kumbuka maaskari wengi si wananifahamu wakawa wananiuliza kulikoni nikawa namngojea mkuu na nadhani katika wale maaskari walionikuta pale wakaenda kumtonya yule mpelelezi mzee Juma akaja pale anajifanya kama anaongea peke yake kuwa najisumbua tu uko ninapotaka kwenda nami wala sikumjibu kwani ilibidi nijiusie mwenyewe moyoni kwani nilikuwa na donge limenibana sana nikifikiria nadai changu naonekana msumbufu? Tena mtuhumiwa nimemkamata amempa dhamana alafu ananambia nikakae nyumbani hadi atakapopatikana eti ndio atanipigia,leo ananiona mimi ndio tatizo,nikajiambia nisifungue mdomo acha alopoke tu.
Mara akafika askari aliyekuwa amevaa kiraia na akatoa ufunguo na kufungua kile chumba na nyuma yake akiwa ameongozana na kundi la watu kama watano hivi na yule kiongozi akanisalimu huku akiwa ameshafungua mlango nami nikajibu salamu yake na akaniuliza tatizo langu maana yeye hakuwa na muda kwani alitakiwa kwenda uwanja wa ndege kusimamia msafara kuna ugeni unakuja kwahiyo lazima awepo eneo la tukio ila kwakuwa ni jumatatu anataka kufanya kikao kidogo na watendaji wake kupata details za yaliyojiri kwa wiki nzima iliyopita,wakati huo ananipa maelezo hayo tukawa yeye na mimi na wale wenzake tumeshaingia ndani ya kile chumba na akanitaka kama sitojali nimngojee hadi atakapotoka uwanja wa ndege ila nikamuomba sana anipe japo dakika 5 tu kwangu zingenitosha kujua hatima ya shauri langu naye akanipa!
Nikajitambulisha na kumueleza suala langu na aliyekuwa na faili na matukio yote toka kumkamata na hadi kuachiwa na kutakiwa nijae nyumbani hadi atakapopatikana mtuhumiwa na nikahitimisha kwa kumuomba kuwa "yeye ndio mtu wa mwisho katika kituo ambacho faili la kesi yangu lipo naomba kauli yako kuwa kituo kimeshindwa kutatua tatizo langu na unanipa ruksa ya kwenda mbele kusaka haki yangu" tena yule mzee Juma aliwa ameitwa na miongoni mwa waliokuwa pale kumbe kulikuwa na mkuu wa upelelezi wa kituo na maofisa wengine,yule mzee Juma anaulizwa hana analosema lenye mashiko na mkuu akawauliza "toka mmeanza kufanya kazi kwenu mmeshakutana na mwananchi mwenye uthubutu wa kudai haki yake katika mfumo huu? Huu ni mtego kwani kama ameweza kuja hadi kwangu je anashindwa kwenda wapi? Mtuhumiwa kamleta mmemtoa,mwendelezo hamtoi je afanyaje?" Yule mzee Juma akajitdmtea kuwa nitoe pesa ya mafuta ya gari ili waende kumsaka na yule mkuu akaniuliza je nipo tayari kutoa pesa ya mafuta? nikamjibu pale pale nishapoteza pesa na mtuhumiwa nishamleta sina hiyo pesa na huyu mpelelezi yeye kama kutoa ndio atoe kwani alijiridhisha akampa dhamana,sina hiyo pesa,yule mkuu akaona huu mziki sasa akanambia sara naomba japo siku 3 nitakupatia jibu nikamwambia poa ntakuja ijumaa na nikatoka zangu huyooo!
Ile ijumaa mimi sikuenda nikakaa kama wiki kadhaa ndipo huo msemo wa MUNGU SI ATHUMAN ukachukua nafasi tena kwani yule bwana Juma Kasangu akawa anaendelea na utapeli wake sijui walimtapeli mama gani uko waliuza nyumba yao ya familia uko Buguruni na yule mama akaenda kununua kiwanja na kwakuwa alikuwa na pesa tayari ujenzi ukaanza mara moja na mama ujenzi umefika kwenye rinta akaja kuelezwa kuwa eneo analojenga sio lake na kule jirani na eneo ambalo mimi nimeuziwa kulikuwa na eneo kubwa sana lilikuwa linamilikiwa na taasisi flani inaitwa UVIKIUTA sijajua wanajihusisha na nini na hawa kina Kasangu wakawa wanaenda kuwauzia watu viwanja kule na wale jamaa uwa wakifanya operesheni inakuwa kama vita wanakwenda kamili na field force na mabomu ya machozi kutokana na historia ya eneo lenyewe na asilimia kubwa ya wakaazi wa maeneo yale walikuwa Wakulya na kama unavyojua hawa ndugu zetu,tatizo kule mpaka wa wale Uvikiuta hakukuwa na mipaka yenye kuonekana wazi sasa unaweza kuwa hapa ukaambiwa upo nje pale ukaambiwa upo ndani yaani wanaweza kuja awamu hii ukaachwa na wakaja awamu nyingine ukatolewa mkukumkuku sasa wale kina Kasangu ndio wakawa wanatumia huo kutokuwepo na mipaka ya wazi kama njia ya kuwapiga wananchi.
Sasa kumbe yule bwana Juma Kasangu akiwa na vijana wake waliuza sijajua eneo gani na nasikia walipata kama milioni 8 hivi yule bwana akawa amewadhulumu wenzake na kati ya aliowashirikiana nao kuna jamaa anaitwa Chacha[emoji23],huyu bwana nadhani alipewa namba yangu na yule Marwa kwani alinipigia siku hiyo sina hili wala lile akataka kuonana nami nikamuelekeza na akaja mara moja Ilala tulikutania pale Ilala mtaa wa Kigoma na Moshi kulikuwa na duka la Mangi,akanieleza mikasa mingi na kueleza waziwazi kuwa amesikia kuhusu ishu yangu na yule wamefanya tukio pamoja na amewazika yeye na wenzake sasa hasira zake anataka kuzihamishia kwa kumkomoa kupitia mimi,ule msemo wa "adui wa adui yako ni rafiki yako" ukachukua nafasi na akanambia jinsi tunatakiwa tufanye na yeye atafanya yake kadri ya uwezo wake na kazi alitaka ifanyike mapema iwezekanavyo nami nikimshirikisha mshkaji wangu mmoja anaitwa Kindamba na Kindamba akampigia Kasangu na kumwambia anataka eneo kwani amepewa namba kupitia rafiki yake,Kasangu akamuuliza kuwa anakaa wapi naye akamjibu kuwa anakaa Mwananyamala A na akamwambia atakuja jioni akitoka kazini ili aje aone maeneo (tulipanga iwe jioni kwa sababu mbalimbali nazo ni kuweza kufika eneo wakati ofisi za serikali ya mtaa kumefungwa,mimi kutoonekana kwakuwa giza litakuwa lishashuka na kuepusha wambea kuwa wengi na kupata kujipanga vyema)

Itaendelea...
Daah! Story nzuri sana
 
NILIVYOMKOMESHA TAPELI WA VIWANJA KIVULE

Sehemu ya 6

UTAJUA HUJUI

Yule mshkaji wangu wa Singida dah nilimuonea huruma kwani alijuta kuniunganisha katika lile jambo na akawa amemueleza mshkaji na mshkaji akawa anajitetea kuwa mara nyingi ninapompigia anakuwa kwenye maombi au bize kupitia kesi ambazo yeye akiwa kama mkuu wa mahakama pale aweze kuzitolea ripoti,nikamtumia ule ujumbe wa tigo pesa na yeye nikamwambia sikublack mail ila tambua simamia tulichopatata na najua umekula pesa wewe na wazee wako wa baraza sasa mimi ntakuja kuitoa kesi hapo kuipeleka mbele kwakuwa sina imani na mwenendo mnaoupeleka dah jamaa akaniomba sana msamaha ndio nikawaza inawezekana mtu akisema hana imani na mahakama husika waliopo pale kunawaletea picha chafu basi sasa ule mramaha wake ndio kama ulimponza sasa nikawa hakimu mimi yeye ndio mshtaki[emoji23][emoji23] na nikamwambia nataka siku ya date mshtakiwa awepo sijui utampataje na akubali kosa na alipe changu (hapo nshaclaim gharama zote zimefika M3.3) we bwana pema hapa ninapohadithia siku ya siku nimekaa benchini mtuhumiwa kaja na ndugu zake wawili wakike na wakiume wakaniita nje wakaniomba sana sana nikawambia nyie wekeni m3.3 ubaoni mi nabwaga kesi wakawa wanataka wanipe kwa awamu tena kianzia laki 5 nikawaambia kampeni hakimu hiyo pesa mi ninataka nipoteze tu wakatoka wamelowa! Muda wa kesi tukaitwa na alipoulizwa alipokuwepo akadai alikuwa anaumwa nikanyoosha mkono naomba kupata vielelezo vya hospitali akasema alipelekwa kwa mganga! Dah dunia hii nyie acheni,mheshimiwa akapotezea akaendelea na kesi mara mtuhumiwa akanyoosha tena mkono akamawambia hakimu yeye amekubali kosa na yuko tayari kunilipa ila sio hiyo pesa yote kwani mimi nilimpa yeye M2 tu (alijichanganya wakati mimi nimempa M1.3 na vichenji,sikuwa nimemalizia) na ananiomba twende mimi na yeye kule site kuhesabu gharama zangu za ujenzi kujua gharama halisi nikakubali na kesho yake nikatakiwa kwenda nae kule kwa mama Anna Mkapa.
Asubuhi nampigia kujua tunakutanaje akanambia wala nisiende yeye kaamua atalipa tu hayo madai yangu anaona tutasumbuana,nikaendelea na shughuli zangu kusubiria siku ya kwenda kule mahakamani.Siku ikafika na muda wa kuingia tukaitwa wakati hakimu anatuuliza natoa maelezo akanikana na kusema yeye hajaniona wala sijampigia dah kama mtu ameiona ile sinema ya kihindi ANDHAL KANOON ndio nilikuwa natamani pale Amita Batchan alipomshindilia bisu yule mzee ndio nilitamani nifanye pale yaani nilitoa maneno ambayo wote pale walibutwb nikamwambia "mheshimiwa naona danadana zimekuwa nyingi sasa nasema mbele ya mahakama hii nikijua wazi kama kutamka maneno ya kutishia kudhuru ni kosa kisheria ila hadi muda huu huyu jamaa keshaharibu maisha yangu,utu wangu,muda wangu na anaendelea kuniletea dharau sasa kwakuwa kadhamilia kuharibu maisha yangu basi ingawa sijawahi kuua ila huyu jamaa familia yake haitokaa salama nipo tayari kwa lolote kutoka sasa na wewe nakuachia ukumbi hukumu hii kesi kwa mizani yako unayoona sawa" dah hakimu jasho linamtoka na yule bibi akadakia unatishia mbele ya mahakama,kiujasiri nikamjibu simtishi na hii kesi ndio itakuwa yake ya mwisho kuja hapa wakati huo sio yeye wala mimi tunaojua litakalotokea! Bibi ananitizama huku natetemeka nasema kama mbwai iwe mbwai!
Hakimu akawa ananiplease kaka acha hasira,acha hasira haki yako utaipata ndugu haya yanazungumzika nikamjibt mimi sitaki huruma ya mahakama wewe toa hukumu tu,akawa anamwambia Kasangu ndugu unasikia hayo maneno? We unayaona yanatoka tu mdomoni na unadhani kutakuwa hakuna utekelezaji? Please mpe pesa yake tusije kuingia matatizoni wote,Kasangu akawa kakaa kimya na mheshimiwa akapiga date ndefu kama mwezi kamili!
Sasa wakati tunatoka ukiwa unaelekea pale kituoni kupanda daladala mimi na ndugu yangu yule Juma Kasangu akawa nae anakuja na ndugu zake akawa ananiambia "mtani mtani we mtani wangu bwana usikasirike ebu njoo tuyajenge bwana" haloo ilinitoka ngumi hiyo Juma chini! Nikamtimba kifuani yule ndugu yangu akanipush nikamponyoka nikawa namfata tena kuendelea kumchapa akanyanyuka akawa anakimbia kurudi kule mahakamani yeye mbele mimi nyuma hadi kati viunga vya mahakama akadumbukia ndani mimi nikageuza nikaondoka zangu wale ndugu zake wananitizama tu wanaogopa hata kufunua midomo yao.
Usiku hakimu akanipigia ooh kaka usifanye hivyo punguza hasira nikamwambia kavukavu nyie kuleni pesa ila mtajua tu siku moja uchungu tunaoupitia tunaodhulumiwa, akaniomba sana nikamwambia haki isipotendwa ama zake ama zangu na huyo fala.
Baada ya mwezi tukaenda tena mahakamani Juma hajaja,ikapigwa date hajaja tena,date ya tatu ndio kama alafu sasa anasema atalipa kwa awamu sita nikasema pesa yangu haikuwa mkopo nataka yote kila mtu akaendelee na hamsini zake na hakimu akamsisitizia kama amekubali kulipa alipe yote kikubwa atoe tamko ni muda gani,nikadakia iwe ndani ya mwezi (natamba mie tena hakimu na mtuhumiwa wote wapo kiganjani)wakakubali hivyo nikapewa tarehe kama ile kwa mwezi unaofuata,tukatakiwa twende kwa mhasibu wa mahakama kwenda kuandikishiana kumbe wakati wote huyo mama mhasibu alikuwepo pale mlangoni anafatilia tena ile kesi ikawa ikifika muda wa kusomwa ingawa ilikuwa inasomwa chumbani watu wengi walikuwa wanajaa hadi hakimu anawaomba wapungue pale mlangoni.
Tulipofika pale yule mama mhasibu akawa ananiambia "wewe mjinga badala ya kuchukua hata kidogo kidogo unakataa,utasumbuka" nikamjibu "mama fanya kazi yako kitengo chako cha hesabu pesa hauna shea nayo mama yangu"
Akakaa kimya akatuandikia maelezo nikaondoka zangu.
Mwezi uliofata nikatimba eneo la tukio na mwanangu tukahesabiwa mpunga wetu alafu yule mama mhasibu akawa ananambia "sinywi hata soda" nikamjibu "mama we nisamehe tu mimi sidili na upande wa upinzani" akanipa makaratasi nikasaini nikatia pesa kwenye begi nikaenda na kwa hakimu kuna makaratasi nikasaini nikatoka na mwanangu hao,nikampigia Chacha nikamuukiza nikulindaje akasema wewe usijali nipe 50 kibingwa na yule Marwa nikamtia 50 nae nikasepa zangu

IMEISHA HIYO

NB:Yule hakimu miaka michache mbele alikamatwa kwa kesi ya rushwa na hadi leo hajarejeshwa kazini kwakuwa malakamiko yalikuwa mengi sana juu yake tena ni rafiki yangu fb eti nae anaweka nyimbo za mapambio kujifanya mwema[emoji23][emoji23] kuna siku nikacomment katika moja ya post yake "PRACTICE WHAT YOU PREACH!" Ila kitambo sijamcheki kama bado anapost post na akiendelea kupost kujifanya mwema mtamuweka hadharani NWAMA YULE! MLA RUSHWA NA MPOTEZA HAKI ZA WATU! (nilitaka kuandika za wanyonge nikajipima nikagundua simo kundi hilo)

IMEISHA WANDUGU!
Jasiri haachi asili,,Wakurya wa kivule na madalali wao ni jau sana
 
Muda wa kesi tukaitwa na alipoulizwa alipokuwepo akadai alikuwa anaumwa nikanyoosha mkono naomba kupata vielelezo vya hospitali akasema alipelekwa kwa mganga! Dah dunia hii nyie acheni
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sema Mkuu ungekuwa na muda huyo hakimu ungeendelea kumtisha na ungeendelea kumdhalilisha mjinga sana .
Hivyo vitisho pekee havitoshi.
 
Nilivyoisoma hii story nimeona wewe ndio ulikomeshwa na nina uhakika urudii tena kuingia kichwa kichwa kununua kiwanja bila kujiridhisha mmiliki halali.
 
Hapo yenyewe tu amshukuru yule mwanangu wa Singida
 
Nilivyoisoma hii story nimeona wewe ndio ulikomeshwa na nina uhakika urudii tena kuingia kichwa kichwa kununua kiwanja bila kujiridhisha mmiliki halali.
Sina tusi la kukupa ninachokujibu ni "haya"
 
Uvikiuta ni taasisi ya Muda sana

Ni taasisi inayo shughulika na maswala ya kujitolea kufanya kazi mbalimbali maeneo mbalimbali ya nchi na nje ya nchi

Hawa wapo kama VSO International, Raleigh International na nyingine nyingi ila hii ni taasisi ya wazawa wakishirikiana na taasisi za nje kama ufaransa, ubelgiji, ujerumani, uswizi, Uk nk kupeleka watu wa kujitolea mwaka mzima na wao wana pokea watu wa kujitolea kutoka nchi hizo

Hawa uvikiuta wana ofisi huko mbagala, hiyo njia ya Magengeni chamanzi...

Vijana tembeleeni hizi taasis kupata hizi fursa...
Geti la kuingilia UVIKIUTA lipo Chamazi maalufu UVIKIUTA.

Ila eneo lao linaanzia Chamazi pembeni ya mto wa maji ya chai mpaka Kivule huko.

Maofisi Yao na kila kitu Chao wamewekeza chamazi na Hostel.
 
Kama hujawahi kununua kiwanja, utaona kila aliyetapeliwa ni mjinga
Issue sio kumuona mjinga ila nashangaa anaposema alimkomesha huyo tapeli wakati yeye ndio kaangaishwa hadi kuja kuipata hela yake jasho limemtoka ndio maana naona yeye ndio kakomeshwa.
 
Sina tusi la kukupa ninachokujibu ni "haya"
Na ungetukana wala nisingekuacha bila kukutukana maana sioni kwanini utukane au kwakuwa ulivyoona wewe imekuwa tofauti na mimi! au ungependa kila mtu anayesoma hii riwaya yako akusifu! Ni lazima uwe mvumilivu pale mtu mwingine anapokuwa na fikra tofauti na zako.
Narudia tena jamaa amejua kukukomesha maana kukomeshwa ni kule kufanywa kutorudia tena jambo ulilolifanya na likakuletea matatizo kwahiyo utajitahidi kuepukana nalo lisijirudie tena, lakini nina uhakika huyo tapeli tabia yake haikuishia kwako itakuwa aliendelea na michezo yake,sasa je umemkomeshaje?
 
Geti la kuingilia UVIKIUTA lipo Chamazi maalufu UVIKIUTA.

Ila eneo lao linaanzia Chamazi pembeni ya mto wa maji ya chai mpaka Kivule huko.

Maofisi Yao na kila kitu Chao wamewekeza chamazi na Hostel.
Duh unajua nilikuwa najiuliza hawa UVIKIUTA wana maeneo mengi? Kumbe ni eneo moja ambalo limetapakaa hadi kule? Basi eneo lao ni kubwa sana na wasipoliwekea uzio litaleta migogoro mingi ya ardhi
 
Issue sio kumuona mjinga ila nashangaa anaposema alimkomesha huyo tapeli wakati yeye ndio kaangaishwa hadi kuja kuipata hela yake jasho limemtoka ndio maana naona yeye ndio kakomeshwa.
Sawa bwana Sanze nimekubali nimekomeshwa
 
Na ungetukana wala nisingekuacha bila kukutukana maana sioni kwanini utukane au kwakuwa ulivyoona wewe imekuwa tofauti na mimi! au ungependa kila mtu anayesoma hii riwaya yako akusifu! Ni lazima uwe mvumilivu pale mtu mwingine anapokuwa na fikra tofauti na zako.
Narudia tena jamaa amejua kukukomesha maana kukomeshwa ni kule kufanywa kutorudia tena jambo ulilolifanya na likakuletea matatizo kwahiyo utajitahidi kuepukana nalo lisijirudie tena, lakini nina uhakika huyo tapeli tabia yake haikuishia kwako itakuwa aliendelea na michezo yake,sasa je umemkomeshaje?
Mimi ni wajibu wangu kuendelea kumfata kujua kama aliacha au aliendelea? Je haya maandishi yanatakiwa yaishie katika burudani ya kusomwa tu? Je wajibu wa fanani kwa hadhira yake ni nini? Inawezekana bwana Sanze wewe haujapata somo katika mkasa husika ila natumai kuna nufaiko kubwa limepatikana kupitia mkasa huu iwe hasi au chanya
 
Nisaidie ndugu yangu maana hata sijui lakumjibu
Kuna jamaa mmoja alikuwa anajiona mjanja sana wa kununua viwanja na wanaotapeliwa ni wajinga na hawajui kufanya uchunguzi.

Siku moja akataka kununua kiwanja kilichopimwa.

===

Kuna Mzee mmoja alikuwa anauza eneo lake zuri tu, milioni 24 wakaongea sana na manunuzi wakakubaliana aliuze kwa Tsh 20M.

Sasa baada ya makubaliano, kabla yule mnunuzi hajatoa pesa muuzaji akamwomba jamaa kuwa kwenye masuala ya mikataba, waandike milioni 8 ili wapunguze kiwango Cha malipo kwa mwanasheria na serikali za mitaa.

Mnunuzi akakubali.

Baaada ya manunuzi, akajitokeza mke wa muuza kiwanja anadai Mume wake kauza kiwanja bila kumshirikisha ( kumbe ni mchongo 😂).

Baada ya kupelekana kwenye vyombo vya sheria, ikaamuliwa mnunuzi arudishiwe pesa yake maana kiwanja tayari kina mgogoro.

Pesa ya manunuzi iliyoandikwa kwenye mkataba ni milioni 8 na mnunuzi jamaa alitoa milioni 20.
 
Back
Top Bottom