Nilivyomkomesha tapeli wa viwanja Kivule Dar es Salaam

Nilivyomkomesha tapeli wa viwanja Kivule Dar es Salaam

Mambo yakukatakata tamaa ni tatizo hapo utaokoa na wengine wengi

Yule mkuu wa kituo nae au ndio mambo mengi kinachouma watu kama hawa wanafahamika kabisa ila..
Mkuu wa pale Staki shari hakuwa tatizo katika suala langu,tatizo walikuwa watendaji wake wa chini ndugu
 
NILIVYOMKOMESHA TAPELI WA VIWANJA KIVULE


Sehemu ya 5


Baada ya kutoka pale nikamvutia uzi mwanangu yule hakimu kule Singidani nikamwambia hakimu aliyesimamia show ndio huyo huyo mwanao akasema poa nitampigia jioni tumpange tuone jambo linakuwaje,dah jioni mwana akapigiwa na nikapewa namba yake tukafanya conference call tukayajenga maana nilimpa sakata lote kuanzia pale Staki shari wakati wakufungua hadi kufikia ile siku akasema poa ntakusaidia na kwa kuwa yule mwanae ni mshkaji wangu nimlinde tukakubaliana kukutana weekend kwani alikuwa anakuja pale Ilala mtaa wa Arusha kwenye mafremu ya kanisa la Anglikana floor ya juu kulikuwa na gym (kwa wale wenyeji wa maeneo hayo watakuwa wamepafahamu) so jumamosi angekuja tupange zaidi nami nikamwambia poa.
Jumamosi akafika na tukayajenga nami nikamwambia hiyo laki ntakupa ila kwa awamu mbili na ile siku pesa yote nilikuwa nayo ila nikaiweka katika tigo pesa na nikamwambia nakutumia 50 leo maana siko vizuri akasema poa,nikamuwekea muhamala wake na tukaacha na baada ya wiki mbele ndio ikawa siku ya kwenda tena kule Madafu (kumbuka ile siku hadi mahakama inafungwa Kasangu wadhamini wake hawakuwa wametimiza vigezo ila wakati wa maongezi yale ya jioni kati yangu,mshkaji wa singida na hakimu,hakimu alisema alidhaminiwa).
Nimefika zangu kama kawaida na siku hii nilikuwa nimeongozana na yule mwanajeshi mwenye eneo ambaye ndio nimeuziwa kiwanja chake na ndugu yangu ambaye alisimama kama shahidi wakati wa mauziano,muda wa shauri ulipofika yule Kasangu hakuwepo na mheshimiwa akasema ameambiwa anaumwa akaahirisha tena wiki 2 tukaondoka zetu.
Udhulio la tatu nikaenda tena nikiwa na yule ndugu yangu bila ya yule mjeshi mtuhumiwa alifika na wakati tunangojea kuingia ndugu zake wakanifata eti tuyamalize pembeni nikawatukana tena nikawaambia wasinisogelee (natamba tena si najua hakimu mwana ndugu yao namkomesha) dah nilijidanganya kwani aliposomewa tena shtaka akakana hivyo tukatakiwa date inayofuata tuje na mashahidi wetu,tukandoka zetu na ilipofika jioni nikampigia mheshimiwa inakuwaje? Kwa maana apeleke jambo mpela mpela nitoke nikafanye yangu,hakimu akanambia niwe mpole kesi imekaa vizuri upande wangu na yule jamaa ana kesi kama 15 pale zote za mambo ya viwanja ila atamkomesha safari hii nikasema sasa hakimu si ndio huyu,ndugu yangu kama unaweza kumalizana na mtuhumiwa wako uko uko kitaani malizana nae hawa mahakimu hawa,hawa wazee wa baraza hawa we acha tu.
Siku ya siku nimewabeba mashahidi wangu mtuhumiwa hola hajafika,goma likalala,date nyingine kimya goma likalala tena nikimuuliza mheshimiwa ananipiga sound nikasema wewe utafurahi na wana Sikinde!
Siku hiyo nafika mahakamani na mshkaji wangu mshtakiwa kaja namuuliza mheshimiwa huyu mtu kafika lakini sioni akiulizwa alikuwa wapi,sioni wakiitwa wadhamini wake kutoa maelezo kwani mimi ni muhathirika wa hili shauri je nieleweje kuhusu hilo? Hakimu ananiambia mahakama inazo taarifa nikamuuliza je sipaswi kuzijua? Wale wazee wa baraza wakawa wananikaripia eti sioneshi utii kwa mheshimiwa niwawajibu siulizi ya mtu mwingine hapa napigania haki yangu,hakimu akanisoma kama nimepaniki na akajua huyu anapoelekea anaweza kumwaga mbona akapiga tarehe ya kuleta mashahidi,nikamstua mjeshi na yule ndugu yangu kuhusu hiyo date.
Siku ya siku mtuhumiwa kaja na mashahidi wangu wakaja na wakatoa ushahidi wao na walipomaliza akiulizwa kama ana maswali kwao akasema hana ila sasa wale wazee wa baraza ndio wakawa wanauliza maswali kibao,hatimaye siku ikaisha tukala date.
Date mpya tulipofika yule jamaa mtuhumiwa akawa hajaja kama mara 3 na hakuna lolote ninaloelezwa nikihoji wale wazee wa baraza hasa yule bibi dah alikuwa hanipi pumzi kama mie ndio mwizi kumbe nimeumizwa mie ilifika hatua nikifika pale namuona kama nini sijui,namuomba Mungu anisamehe tu ila yule mja wake najua yeye ni mjuzi zaidi anajua lakumfanya🙏🏼.Hakimu nikawa sasa nikimpigia mara anakata na ujumbe unakuja ule "i'll call you back" mara "on meeting" na mengineyo nikasema huyu hanijui sasa ndio atajua joto ya jiwe,nikamtumia ule ujumbe wa muhamala wa tigo pesa yule mwanangu wa Singidani kwani niliusave kwenye draft then nikampigia nikamwambia mwanao anajifanya mjanja pesa yangu lala,wazee wake wa baraza wananizingua,simu zangu hapokei,mtuhumiwa hafiki na anamtetea sasa wewe unanijua kinagaubaga najua ANAYETOA NA ANAYEPOKEA RUSHWA WOTE NI WAKOSAJI sasa mie kuku wa kienyeji napeleka TAKUKURU huu ujumbe twende jela mimi na yeye tuone watoto wa nani watakaoteseka na mshkaji akaniplease sana,nikamwambia tatizo sio mimi tatizo mwanao ama arudishe changu apeleke kesi anavyotaka ama afate atende haki kinyume na hapo ni UPALESTINA TU (Najitoa mhanga nae)


Itaendelea!
Iko wapi? Uwe unanitagia hapo chini yake 😂💃
Unataka niwe nakuletea kabisa eehhh
 
Back
Top Bottom